Saturday, January 19, 2013

AJARIBU KUJILIPUA KWA PETROL AKIWA NJE YA KITUO KIDOGO CHA POLISI RUNGWE MBEYA

RPC  MBEYA KAMANDA DIWANI


Mnamo tarehe 17.01.2013 majira ya saa 23:00hrs huko katika eneo la kiwira kata ya Kiwira wilaya ya Rungwe mkoa wa mbeya. Joseph s/o Mwaenga, miaka 32, Kyusa, mwendesha pikipiki @ bodaboda na mkazi wa kiwira. Alijimwagia mwilini mafuta aina ya petroli na kisha kumwagia mafuta mengine kituo kidogo cha polisi kiwira na kutoa kiberiti kwa nia ya kutaka kujilipua. Mtuhumiwa alidhibitiwa na askari waliokuwa zamu kwa kumkamata na kumuweka chini ya ulinzi. Hakuna madhara ya kibinadamu wala mali yaliyotokea. Chanzo cha tukio hili ni mtuhumiwa kufanya fujo  katika kijiwe/kituo chake cha bodaboda akiwa amelewa na alipotaka kukamatwa  na wananchi alikimbia hivyo wananchi kuichukua pikipiki yake na kuisalimisha kituo cha polisi Kiwira ndipo mtuhumiwa alikwenda kituo cha polisi akiwa bado amelewa huku akiwa na dumu la mafuta ya petroli. Taratibu za kisheria zinafanywa ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani.  Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi wa polisi Diwani athumani anatoa wito kwa jamii kutokutumia vilevi kupita kiasi kwani inaweza  kusababisha madhara  makubwa pasipo kutarajia.


Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Thursday, January 17, 2013

MUSOMA UTALII YAJENGA CHUO CHAKE TABORA

Shabani Mrutu mkurugenzi wa Chuo Cha Musoma Utalii Tabora

   NA MWANDISHI WETU TABORA
UKOMBOZI wa taifa letu kwa kizazi cha sasa na kijacho,  jambo lamsimngi zaidi ni elimu bora ni suala muhimu sana ambalo litasaidia kuondokana na hali ya umasikini,maradhi na ujinga ambao umekithiri
miongozi mwa watanzania waliowengi kwa sasa.

Chuo cha musoma utalii,kilichopo mkoani Tabora, ni chuo  kilichosajiliwa na “NACTE” kinachoendesha mafunzo ya kozi mbalimbali na kimekuwa kikitoa elimu inayolingana na hali halisi ya sasa ya sayansi na teknolojia.

Aidha chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo ua juu ya kozi kama vile  uongozaji wa  watalii,hotel management,uwalimu wa chekechea, uandishi wa habari na utangazaji, secretarial na Computer hali iliyopelekea kufanikiwa  kutoa wahitimu bora waliofanikiwa kuajiriwa
na kujiairi ili kwenda sanjari na changamoto za soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Mkurugenzi wa chuo cha Musoma Utalii tawi la Tabora, Shabani  Mrutu,alisema hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake alisema chuo kimekuwa ni chuo cha  mfano wa kuigwa,na kimbilio la wengi na hadi sasa chuo hicho kimeanza ujenzi wake.

Alisema ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 80, ambapo kutakuwa na  mabweni yanayoweza kuchukua wanafunzi zaidi 200,vyumba vya madarasa 10,jengo la utawala la ghorofa na maktaba ya  kisasa,jiko la kisasa,ukumbi na sehemu za  mapumziko.

Alisema kuwa mkoa wa Tabora una vivutio vingi vya kitalii lakini  haviendelezwi ipasavyo hivyo ujenzi wa chuo mkoani hapa ni ukombozi mzuri ambao utasaidia vivutio hivyo kuonekana na hatimaye kukuza secta
ya utalii mkoani Tabora.

Mrutu alifafanua zaidi kuwa chuo hicho kilianzishwa mwaka 2004 kikiwa  na wanafunzi 42 na sasa kuna wanafunzi 280,ambapo chuo kilikua chini ya usimamizi VETA.

Aidha mkurugenzi huyo aliongeza kuwa chuo hadi sasa,kimesajiliwa na  kutambulika na NACTE kwa barua ya awali yenye kumb. Namba NACTE/BA/77/465/605/Vol 1/9 usajili ambao ulianza mwaka 2012.

Anabainisha kuwa chuo kina matawi mengi nchini ili kuwafikia vijana  wengi zaidi kwa gharama nafuu sana.

Mafanikio toka 2004 hadi sasa kampasi ya Tabora. Mrutu anabainisha kuwa mafanikio kwa tawi la Tabora,ni kuongezeka kwa  wanafunzi toka 2004 wanafunzi 42 hadi 280 mwaka 2012.

Akizungumzia mafanikio katika utoaji wa elimu katika chuo  hicho,  mkuu huyo wa chuo alisema wamejipanga vyema kutoa elimu bora na zaidi chuo kina kwa kuenmdelea kuongeza walimu ambapo hadi sasa kuna waalimu 18 wenye sifa zinazotambulika kisheria.

Alisema ili kuweza kutoa elimu bora pia wanafunzi wa chuo hicho  wamekuwa wakienda mafunzo ya vitendo kulingana na kozi wanazosoma katika mikoa mbalimbali.

Mkurugenzi huyo anaongeza kuwa wanafunzi hupelekwa katika hotel kubwa  za kitalii,kampuni za uongozaji watalii ,TANAPA na kozi za ufundishaji chekechea hupelekwa katika shule za kiingereza,wengine vituo vya radio kwa wanafunzi wanaochukua masomo ya uandishi wa habari.

Alisema maeneo mengine ya kitalii wanafunzi hao hupelekwa kwenye  makumbusho ya Kwihara nje kidogo ya mji wa Tabora, sehemu ambayo makumbusho hayo yana historia ya kipekee kwa mkoa na taifa kwa ujumla.

Akizungumzia muitikio wa wanafunzi  kujiunga na chuo ni mzuri kwani  kila wanapochukua wanafunzi kila muhula idadi huwa inaongezeka kulingana mahitaji halisi,ambapo sifa zilizowekwa ni wanafunzi
waliohitimu kidato cha nne hadi cha sita.

Malengo na matarajio ya chuo:

Mkurugenzi huyo Shabani Mrutu, alisema chuo hadi sasa kinakamilisha majengo yake tawi la Tabora,ambayo yanatarajiwa kukamilika ndani yamiezi Tisa ujenzi huo unatarajia kukamilika kwa gharama ya zaidi ya sh
milioni 800.

Alisema malengo mengine ni kusajili  kozi nyingi zaidi kwenda NECTA,sanjari na kusajili chuo kiweze kutoa elimu ya juu kutokana na kozi zilizopo.

Aidha malengo mengine ni kuweza kusajili wanafunzi watakaofikia  1000,kuongeza matawi nchini ili chuo kiweze kutoa huduma bora zaidi kwa jamii tena kwa gharama nafuu na kutoa elimu bora yenye ushindani
katika soko la ajira.

Kuhusu changamoto zilizopo:

Kuhusu changamoto zilizopo mkurugenzi huyo alisema chuo kimekuwa  kikikabiliwa na changamoto kadhaa ambazo ni uelewa wa jamii katika vyuo binafsi kwani imejengeka fikra potofu vyuo binafsi wahitimu huwa
hawawezi kupata ajira na kwamba fikra hizo ni potofu kwani vyuo binafsi na vya serikali vina nafasi sawa ilimradi viwe na usajili unaotambulika serikalini. “Ipo dhana ya namna hiyo lakini tumekuwa tukijitahidi sana kutoa elimu kwa wazazi na zaidi ufaulu na ksaidia wanafunzi kujiajiri na kuajiriwa kumekuwa kukitusaidia kuondoa dhana hiyo potofu.” Alisema.

Alitaja changamoto nyingine kuwa uelewa mdogo wa wazazi juu ya kozi ya “Hotel Management,” kuwa ni kozi ya kihuni kiasi cha kuleta wanafunzi kiduchu, ili hali si kweli ni kozi nzuri na ina uwanja mpana wa ajira na uhuni ni tabia ya mtu binafsi.

Aliongeza changamoto nyingine ni hali ya kipato cha wazazi na walezi  na jamii kwa ujumla kwani imekuwa moja ya changamoto ya chuo kushindwa kufikia malengo yake hasa kutokana na ulipaji mgumu wa ada kwa
wanafunzi,kwani “Wakazi wa mkoa wa Tabora wengi wao ni wakulima kwa asilimia kubwa hivyo wengi husubiri kipindi cha msimu kimalipo ama mvua inaponyesha vyema.”alisema.

Alisema hali hiyo hupelekea chuo kutofikia malengo yake ya kujiendesha  hasa ukizingatia chuo hakina ufadhili wowote zaidi ya kujiendesha chenyewe.

Alisema chuo pia kinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vifaa na  hasa vinapopatikana huwa ni vya bei ya juu,huku  vifaa vya kozi za utalii navyo huwa ni tatizo kubwa kupatikana.

Mkurugenzi huyo alitoa wito na ushauri kwa jamii kuendelea kukiamini  chuo cha Musoma Utalii,kwani toka kimeanzishwa kimeweza kutoa wahitimu bora kwa asilimia 90 wamefanikiwa kujiajiri na kuajiriwa kote nchini.

“Tunaomba wazazi na jamii kwa ujumla kuendelea kuleta wanafunzi ili  waweze kupata elimu bora yenye kutambulika kitaifa na kimataifa.” Aliongeza.

Aidha aliomba pia wazazi kuendelea kuchangia fedha za kwenda mafunzo  ya vitendo ,(Study Tour), kwani chuo kina ratiba ya kutembelea Mbuga za wanyama mara tatu (3) kila mwaka ikiwa ni sehemu mojawapo ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watanzania kwa ujumla.

Alisema ana imani endapo chuo kitakamilika ujenzi wa majengo ya yake ana imani mkoa wa Tabora ambao ni mkoa wenye historia ya kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni utapiga hatua ya kimaendeleo na kutoa ajira zaidi.

Mrutu anaongeza kuwa ni dhahiri mkoa wa Tabora una fursa nyingi sana  lakini bado hakuna jitihada za makusudi na hasa elimu kwa vijina wetu kusoma ili kukabiliana na ushindani wa shirikisho la afrika mashariki kwa sasa.

Hata hivyo mkurugenzi huyo amesifu kasi mkuu wa mkoa wa Tabora,Fatma  Mwassa katika usimaizi na kutoa vipaumbele ya elimu mkoani hapa kwani dalili za mbadiliko ya elimu zimeanza kutoa picha ya mafanikio mazuri tuendako.

Mrutu anaongeza kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora,Fatma Mwassa amekuwa  mstari wa mbele zaidi katika kusukuma gurudumu la elimu kwa kuweka mikakati madhubuti ya watoto hasa wa masikini waweze pata elimu itakayosaidia kuondokana na umasikini.

Mkurugenzi huyo anasema kwa sasa chuo cha Musoma Utalii ni kimbilio la  wanyonge kwani kimaonekana ni mkombozi zaidi.

ATOROKA GEREZANI NA KUVUA NGUO ILI ASIKAMATWE

Askari Polisi wa kikosi cha FFU Tabora mjini wakijaribu kumdhibiti kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Jonas Oscar(25)ambaye inadaiwa kuwa alitoroka Gereza la mahabusu Tabora maarufu kwa Zuberi wakati akiwa anatumikia kifungo cha mwaka mmoja. 
Na mwandishi wetu maalumu
 
Mwananchi mmoja kwa kushirikiana na askari wa kikosi cha kuzuia ghasia FFU mjini Tabora wamefanikiwa kumkamata  mfungwa mmoja wa gereza la mahabusu Tabora wakati akifanya jaribio la kutoroka akiwa amevua nguo na kubakia uchi wa mnyama. 

Mfungwa huyo ambaye anafahamika kwa jina la Jonas Oscar(25)imedaiwa kuwa mnamo majira ya mchana siku ya tarehe 14 januari 2013 alifanya jaribio hilo wakati akiwa kwenye kazi za bustanini na wafungwa wenzake.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililokuwa kama mchezo wa kuigiza mfungwa huyo alilazimika kuvua nguo zote(sare za kifungwa) ili isiwe rahisi kumkamata na kuanza kutokomea mitaani.

Hata hivyo wakati akiwa ameanza safari hiyo ya kukwepa kifungo cha mwaka mmoja ambacho ameanza kukitumikia mapema mwaka huu,mfungwa huyo Jonas aliibukia katika kambi ya Jeshi la Polisi iliyoko jirani na gereza hilo la mahabusu hatua ambayo ilisababisha kuonwa mapema kwakuwa alionekana kuwa ni mtu wa ajabu kwa kukimbia akiwa uchi wa mnyama.

"Nilipomuona niliamua kumkimbiza na kutaka kujua anatatizo gani,nilimkamata na kuwaomba msaada FFU waliokuwepo hapo jirani na Kituo chao"alisema mwananchi huyo ambaye alijifahamisha kwa jina la Mapinduzi

Aidha katika hatua nyingine mfungwa huyo amefikishwa mahakama ya wilaya ya Tabora,mbele ya hakimu Mheshimiwa Magori na kukabiliwa  kwa kosa la kutoroka chini ya ulinzi halali kinyume cha sheria namba 16 kifungu cha 116 ya mwaka 2002,ambapo alihukumiwa kutumikia adhabu kwenda jela kwa kifungo cha miezi 16,adhabu ambayo ameanza kuitumikia mara moja.

Awali Jonas Oscar imedaiwa kuwa alikuwa akitumikia kifungo cha mwaka mmoja akiwa ni mfungwa No.02,2013 katika Gereza la mahabusu Tabora mjini baada ya kupatikana na hatia ya kutishia kumuua baba yake mdogo huko katika wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.    
 

CHADEMA SASA WAANZA KULIPUANA


582442 10152382144810063 1077508772 n 8b1ed



Na: Boniface Meena.
 
KATIKA kuonyesha hali si shwari ndani ya Chadema, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha) wa chama hicho, Juliana Shonza amesema ameamua kumshtaki Mwenyekiti wake, John Heche kwa kumuita kuwa ni msaliti wa chama na kwamba anatumiwa na CCM na kuamua kumfukuza nafasi yake bila kutoa nafasi ya kusikilizwa.



Pia, amemlipua Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa akidai kuwa amefanya ufisadi ndani ya chama kwa kujikopesha Sh140 milioni ambazo hajazilipa hadi sasa.
Mbali na hilo, amemshukia Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwa kudai kuwa anatoa kauli za kukurupuka ambazo zinakiyumbisha chama hicho kikuu cha upinzani nchini.


Shonza alitoa kauli hizo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juu ya tuhuma zilizotolewa na mwenyekiti wa Bavicha na kuhusu kufukuzwa kwake ndani ya chama akiwa na wenzake Mtela Mwampamba na Habibu Mchange.


“Heche na Mbowe wamenifedhehesha kwa kauli zao na wamenichafua na kunidhalilisha mbele ya umma wa Watanzania, hivyo nitapambana nao kuhakikisha haki yangu inapatikana,” alisema Shonza.


Shonza alisema kwamba yeye bado ni makamu mwenyekiti wa Bavicha na mwanachama halali wa Chadema kwa kuwa hadi anazungumza hakuwa amepewa barua ya kufukuzwa kwa kuwa kikao kilichotoa uamuzi huo ni batili.


Alisema kikao kilichoitwa ni cha kamati tendaji na kufikia maamuzi ya kumfukuza kilikuwa batili kwa kuwa katiba pamoja na mwongozo wa Bavicha ulikiukwa, kitu kinachosababisha aeleze kuwa uamuzi uliotolewa na kikao hicho yalikwishapangwa na viongozi wa kitaifa.


“Nasisitiza kwamba ni ukweli uliowazi kwamba ajenda na maazimio ya kikao hicho yalikwishaamuliwa hata kabla ya kikao hicho, kwa sababu taarifa za kufukuzwa kwetu zilikwishaanza kusikika kwenye mitandao ya kijamii kabla hata ya kamati tendaji batili,”alisema Shonza.


Alisema mkakati wa Heche na vibaraka wake umejikita kutukuza ukanda ndani ya chama waziwazi, akieleza kuwa watu waliofukuzwa ndani ya chama hicho wanatokea Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini haswa Mbeya wakati vijana wa Kaskazini wameachwa kwa madai kuwa wametoa ushirikiano.


“Natarajia kuomba ufafanuzi wa kikatiba juu ya shutuma zilizotolewa dhidi yangu na Heche kwa kuwaaminisha Watanzania uongo wake,”alisema Shonza.


Kuhusu Mbowe
Alisema kuwa amesikitishwa na kauli ya kiongozi wake huyo katika baadhi ya vyombo vya habari kwamba, madai aliyoyatoa ni ya kitoto kwani ni kitu cha kushangaza kwa kuwa yeye Juliana hayajui ni madai gani hayo.


Alisema kama madai ambayo Mbowe anadai ni ya kitoto ni ya yeye kuhoji kwa nini chama hakiweki akiba kwenye akaunti kwa ajili ya uchaguzi wa 2015 kama ilivyokubaliwa kwenye baraza kuu basi itakuwa ni ajabu.


Kuhusu Dk Slaa
Alisema inashangaza kwa mwenyekiti wa chama anafumbia macho hatua ya Dk Slaa kujikopesha pesa ya ruzuku ya Watanzania zaidi ya Sh140 milioni, kwani ni kinyume na utaratibu uliopo.


 MWANANCHI

WENGINE WAENDE KUJIFUNZA MBOLA .DKT MGIMWA

Na Lucas Raphael,Uyui

Serikali imesema kuwa inaangalia uwezekano wa kusambaza teknolojia na mbinu zilizotumika katika kijiji cha millennia cha Mbola mkoani Tabora, zitumike katika vijiji vyote hapa nchini, ili kuweza  kuutokomeza umasikini kwa haraka na kutimiza malengo 8 ya milenia.

Waziri Fedha Dk. William Mgimwa, aliyasema hayo katika kijiji cha Ilolangulu, wilaya ya Uyui mkoani Tabora, alipokuwa akizungumza na wakazi wa kijiji  16 vya millennia mbola , ambapo aliwapongeza kwa kazi nzuri na jinsi walivyoupokea mradi huo, ambao leo umekuwa wa mfano.
Alisema kwamba ni vema wananchi wakahakikisha miradi yote iliyotekelezwa chini ya mradi wa vijiji vya millennia mbola inatunzwa vizuri ili iwe daraja la kufundishia vijiji vingine nchini katika utekelezaji wa malengo 8 ya milenia .

Waziri Mgimwa, aliyefika kijiji hapo kwa ajili ya kujifunza na kujionea jinsi mradi huo shirikishi wa kijiji cha Milenia unavyooendeshwa na Umoja wa mataifa ulivyoweza kupambana na umasikini kwa wakazi wa vijiji 16 vya wilaya ya Uyui.

Awali Mratibu wa mradi wa kijiji cha Milenia cha Mbola mkoani Tabora, Dk Gerson Nyadzi, alisema kuwa wakazi wa kijiji hicho wameweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo baada ya kuwezeshwa na serikali na mradi wa kijiji hicho kwa kupewa pembejeo ili kuweza kuondokana na umasikini uliokithiri iliyowawezesha wakulima kulima na kuvuna zaid ya maguni 20 hadi 40 kwa heka moja ya mahindi .

Mapema Mwenyekiti wa kijiji cha Ilolangulu Ali Magoha, alisema kuwa mradi wa kijiji cha millennia unaojumlisha vijiji 16 umefanikiwa kwa kutimiza malengo yote 8 yaliyokusudiwa kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 85.
Alitaja manufaa ambayo wameweza kupatikana toka mradi wa vijiji vya milenia mbalo ulipoanza ni pamoja na  ujenzi wa nyumba za kisasa za matofari ya kuchoma na bati ,uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka .

Pia alisema kwamba mradi huo umesaidia kupunguza tatizo la vifo vya watoto chini ya miaka 5 na vifo vya akina  mama wajawazito.
Alisema hapa awali vifo hivyo vilikuwa wastani wa watoto 3 nadi 5katika kipindi cha miezi mitatu na kinamama 5 kwa kila mwezi lakini kwa sasa wastani huo ni kwa kipindi cha miezi 6 na wakati mwingine hakuna kabisa.
Magoha alisema kwamba hatua hiyo imefikiwa baada ya wananchi kupata elimu juu ya kutumia vyandarua na kuua mazalia ya mbuhivyo kupunguza kasi ya maradhi yan malaria katika eneo hilo..
Mwenyekiti huyo wa serikali ya vijiji vya mrai wa vijiji vya milenia mbola akizungumzia swala la elimu alisema kwamba kwa sasa kiwango cha wanafunzi wanaoacha masomo imepungua tangu mradi huo umeanza na kuwa sasa wanafunzi wengi wanamaliza masomo ua darasa la saba .
Alitaja mbinu hizo ni pamoja na kutoa chakula kwa wanafunzi na kuhamasisha michezo mashuleni hivyo wakuwavutia watoto wengi kujiunga na shule .
Kuhusu suala la maji alisema kwamba wanaendelea vizuri ambapo wastani wa asilimia 60 ya wakazi wa eneo hilo wanapata maji safi na salama tofauti na ilivyokuwa awali .
Mwisho


Naye Mbunge wa jimbo la Tabora kaskazini Shaffin Sumar, aliishukuru serikali kwa kuendelea kuchochea maendeleo katika vijiji vyote 16 vya millennia kwa kuanza mchakato wa kupeleka umeme katika vijiji hivyo  vyote ili kusaidia kukua kwa maendeleo ya haraka.
 
Mwisho.
 

SHULE YA MSINGI YA KAB ILIWAA NA UHABA WA MATUNDU YA VYOO .

Na Lucas Raphael.Nzega.


ZAIDI  ya  Wanafunzi  1500  wa  shule  ya  msingi   Nyasa  mbili  iliyopo  wilayan i Nzega  Mkoani  Tabora wanakabiliwa na uhaba wa matundu ya vyoo.


Akizungumza  na   waandishi wa habari ofisini kwake jana mwalimu  mkuu  wa shule  hiyo  George  Alphonce  alisema kuwa  shule  hiyo  ina wanafunzi  1520 huku   ikiwa na  matundu  ishirini  ya  vyoo  ambayo  haya tosherezi  kwa  matumizi  ya  wanafunzi   hao.


Alisema  kuwa  kwa  idadi  hiyo  shule  inaupungufu  wa  matundu  40 ambapo  kwa  sasa  wanafunzi   hao  hutumia  tundu  mmoja  wanafunzi  76  nje  ya  utaratibu  wa  kawaidi ,utaratibu  wa kawaida inapaswa  tundu  mmoja  wanafunzi  20.


Alisema  kuwa  tatizo hilo  ni  la muda  mrefu   kutokana  na  kuongezeka  kwa  wanafunzi  kila  mwaka  tofauti  na  wale  wanao  hitimu  elimu  ya  msingi ya Darasa la saba.


George  alisema kuwa wanafunzi kwa kipoindi hiki wanap[ata shida kujisaidia katika matundu hayo  hali ambayo wanajikuta wakiwa katika wakati mgumu na kusababisha mazingira ya kusoma kuonekana kuwa magumu kutokana na uhaba huo wa matundu.


Alisem,a Jitihada inayofanika kwa kushilikiana na kamati ya shule pamoja na wazazi wapo katika harakati za kukamilisha matundu ya vyoo nane ambayo yatasaidia kupunguza msongamano huo.


Alisema wazazi na walezi wamejitokeza kupambana na tatizo hilo ili kuhakikisha wanafunzio hao wana soma katika mazingira mazuri.


George aliomba serikali kuingilia kati suala hilo kuhakikisha wananfunzi wana soma katika mazingira stahiki ili kuwawezesha kufanya mazuri katika mitihani yao ikiwa na kukarabati miundombinu mbalimbali ya masomo katika shule za msingi.


Aliongeza kuwa wazazi wajitokeze kwa wangi kusaidia serikali katika kuboresha mazingira ya kusoma watoto wao ikiwa na kuchangia michango m,b alimbali ya shule.


Mkuu wa wilaya ya Nzega ,Bituni Msangi alisema kuwa jitihada zinaendelea kuwa hamasisha wazazi na walezi katika kuchangia maendeleo na kutatua matatizo ya wanafunzi ambayo yapo katika uwezo weao ikiwa na kuboresha mazoingira ya masomo pamoja na vyoo.


Mkuu huyo wa wilaya  alisema kuwa taarifa hiyo itafuatiliwa kwa Ofisa Elimu wilaya ili suala hilo liweze kufuatiliwa kwa ukaribu ikiwa na kukagua mazingira mbalimbali ya shule hizo pamoja na vyoo.

Mwisho.

Wednesday, January 16, 2013

WANAPOKUTANA WENYE VITAMBI HUWA NI VITUKO VITUPU

 

JAMAA WAKIFURAHIA UJIO WA NDEGE YA PRICISIONAIR MBEYA LEO HAPA WANAPIGA CHIAZI YA VITAMBI

PICHA NA MBEYA YETU

ANUSURIKA KUUWAWA KWA WIZI WA MOTA ILOMBA MBEYA

JAMAA ANAEHISIWA KUWA MWIZI WA MOTA AMEPATA KIPIGO KIKUBWA NUSURA AUWAWE KWA HASIRA ZA WANANCHI AMEJULIKANA KWA JINA MOJA TU WILLY
JAMAA HUYU INASEMEKANA NI MZOEFU SANA WA WIZI ANATAFUTWA SANA ENEO LA ISYESYE JIJINI MBEYA KWA TUHUMA ZAKE ZA WIZI
HII NDIYO MOTA ALIYOKUTWA NAYO HUYO ANAEHISIWA KUWA MWIZI
JAMAA ASHUKURU POLISI LASIVYO MAUTI YANGEMKUTA


PICHA NA MBEYA YETU

Tuesday, January 15, 2013

WAUAWA NA KUZIKWA KWENYE KABURI MOJA



Hussein Molela wakiwa hai na kuwazika wote watatu katika kaburi hilo moja. 

Baada ya hapo watu hao walikwenda nyumbani kwa ernest s/o twini molela na kuichoma moto nyumba yake. Kufuatia tukio hilo watuhumiwa wawili waliokuwa vinara wa tukio hilo wamekamatwa ambao ni 1. Vena s/o ernest molela [mtoto wa marehemu ernest s/o twini molela], miaka 26, muwanda, mkulima na 2. Emanuel s/o christopha, miaka 16, muwanda mkulima wote wakazi wa kijiji cha ivuna.  Marehemu wote watatu ni ndugu wa ukoo mmoja. Taratibu za kufukua kaburi ili miili ya marehemu ifanyiwe uchunguzi zinafanywa. 

Aidha taratibu zinafanywa ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani.

Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani athumani anatoa  wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake waheshimu na kutii sheria pasipo kushurutishwa. 

Pia anaiasa jamii kuachana na imani za kishirikina kwani zina madhara makubwa kwa jamii ikiwa ni pamoja na kurudisha nyuma maendeleo. 

Aidha anatoa rai kwa jamii/kikundi cha watu wenye kero/malalamiko,ushauri ,ujumbe maalum kutafuta njia iliyo halali kufikisha kero,malalamiko,ushauri ,ujumbe wao kwa njia ya mazungumzo badala ya kutumia vurugu/fujo na kusababisha mauaji.