Hussein Molela wakiwa hai na kuwazika wote watatu katika
kaburi hilo moja.
Baada ya hapo watu hao walikwenda nyumbani kwa ernest s/o
twini molela na kuichoma moto nyumba yake. Kufuatia tukio hilo watuhumiwa
wawili waliokuwa vinara wa tukio hilo wamekamatwa ambao ni 1. Vena s/o ernest
molela [mtoto wa marehemu ernest s/o twini molela], miaka 26, muwanda, mkulima
na 2. Emanuel s/o christopha, miaka 16, muwanda mkulima wote wakazi wa kijiji
cha ivuna. Marehemu wote watatu ni ndugu wa ukoo mmoja. Taratibu za
kufukua kaburi ili miili ya marehemu ifanyiwe uchunguzi zinafanywa.
Aidha taratibu zinafanywa ili watuhumiwa wafikishwe
mahakamani.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi
diwani athumani anatoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria
mkononi na badala yake waheshimu na kutii sheria pasipo kushurutishwa.
Pia anaiasa jamii kuachana na imani za kishirikina kwani
zina madhara makubwa kwa jamii ikiwa ni pamoja na kurudisha nyuma
maendeleo.
Aidha anatoa rai kwa jamii/kikundi cha watu wenye
kero/malalamiko,ushauri ,ujumbe maalum kutafuta njia iliyo halali kufikisha
kero,malalamiko,ushauri ,ujumbe wao kwa njia ya mazungumzo badala ya kutumia
vurugu/fujo na kusababisha mauaji.
No comments:
Post a Comment