Saturday, January 5, 2013

MTUHUMIWA WA KESI YA WIZI WA SHILINGI MILIONI 15.6 MALI YA SERIKALI YA WANAFUNZI UDOM KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII SANAA NA LUGHA IDDY MOHAMMED NA WENZAKE WAACHILIWA KWA DHAMANA


Aliyekuwa Raisi wa Kitivo Cha Sayansi Cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM).Idd Mohammed anayetuhumiwa Kuiba Shilingi Milioni 15.6 Mali ya Serikali ya Wanafunzi Wa Kitivo Hiko

Aliyekuwa Raisi Wa Kitivo Cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha Idd Mohammed (Wa Sita kutoka Kulia Waliokaa Kwenye Viti) Alipokuwa Kwenye moja ya Kampeni zake za Kuwania Kiti Cha Uraisi Mwaka Jana Chuoni Hapo

Aliyekuwa Raisi Wa Kitivo Cha Sayansi ya Jamii,Sanaa na Lugha Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)  ambaye pia ni Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 wa Kozi ya Biashara na Akaunti (BCOM Accounting) Idd Mohammed mnamo alhamisi alishikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma katika Kituo Cha Polisi Cha UDOM kwa tuhuma za Wizi wa Pesa Za Kitanzania Shilingi Milioni 15.6 mali ya serikali ya wanafunzi wa kitivo hiko ambazo aliweza kuhamisha kutoka Kwenye Akaunti ya Serikali ya Wanafunzi wa Kitivo Hiko Kwenda kwenye Akaunti Binafsi ya Waziri Wa Fedha Wa Kitivo Hiko Ibrahim Matata.

Raisi huyo pamoja na Waziri wake wa fedha walikamatwa juzi alhamisi na Polisi huku wakikutwa na Pesa taslimu shilingi Milioni 7,224,000 mikononi. Chanzo chetu kilienda kusema kuwa Awali Raisi huyo inasemekana aliwaweka watia saini anaowataka yeye kinyume na taratibu na kuwatoa waliowekwa kwa taratibu na Sheria za Bunge la Serikali ya Wanafunzi wa Kitivo hiko kuwa ndio watu wenye dhamana ya kuruhusu pesa za Serikali ya Wanafunzi kutoka Katika Akaunti hiyo ya Serikali ya Wanafunzi.
Chanzo Chetu kiliendelea Kutupasha kuwa Raisi huyo pamoja na Waziri wake wa Fedha walikamatwa Juzi na kulala katika Kituo Cha Polisi Cha UDOM tayari kwa Uchunguzi na hatua za kisheria Kuchukuliwa dhidi yao kabla hawajaweza kuachiwa jana Kwa dhamana.
Habari zaidi ambazo Lukaza Blog  imezipata kutoka katika Vyanzo tofauti tofauti Zinadai kuwa Raisi huyo pamoja na Waziri wake Wa fedha wanaweza kufikishwa Mahakamani Jumatatu kwaajili ya kusomewa mashtaka yao ikiwemo tuhuma za wizi wa Shilingi Milioni 7,224,000 ambazo walikutwa nazo mkononi na kiasi kingine kubaki kwenye akaunti Binafsi ya Waziri Huyo wa Fedha Ibrahim Matata 
Baada ya Bunge la Serikali ya Wanafunzi wa Kitivo Hiko Cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha kukaa jana Majira ya Saa Kumi Jioni nakuweza Kutoa uamuzi wa Kumvua Madaraka Raisi huyo ambapo imepelekea Baraza zima la Mawaziri kuvunjwa na kupelekea Spika Wa Bunge Kushikilia Serikali Hiyo Kwa Muda.
"Kwenye Majira ya Saa 10 jioni ya leo (Jana) bunge lilikaa na ndipo Spika alipoamua kuchukua uamuzi uliotolewa na wabunge wa kumvua madaraka raisi huyo na kupelekea Baraza la mawaziri kuvunjwa na Serikali kushikiliwa na Spika Wa Bunge hilo" Kilisema Chanzo Chetu.

Kwenye Majira ya Saa Moja Jioni ya jana aliyekuwa raisi wa Kitivo Hiko Idd Mohammed na aliyekuwa waziri wa fedha Ibrahim Matata Waliweza kuachiwa kwa Dhamana na Sasa Wapo Nje Kwa Dhamana

Chanzo Chetu kiliendelea kudai kuwa Kuna fununu zilizozagaa kwa baadhi ya wanafunzi wachache wa kitivo hiko Kuwa Inasemekana Aliyekuwa Raisi Wa Kitivo Hiko ana kashfa ya Kuomba Rushwa ya Shilingi Milioni Moja laki moja na hamsini elfu ( 1,150,000 ) katika Duka lililopo bweni namba 13 (block 13) ambapo chanzo hiko kimedai kuwa kulikuwa na ushahidi wa Sauti ambao ulirekodiwa wakati Mtuhumiwa huyo akiomba rushwa kabla ya kukamatwa hapo juzi kwa tuhuma za Wizi wa Shilingi Milioni 15.6 akiwa na aliyekuwa waziri wake wa fedha Ibrahim Matata.

RAIS KIKWETE AONANA NA MSHAURI WA KIJESHI WA UMOJA WA MATAIFA IKULU DAR ES SALAAM LEO



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja  na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto Mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Juma Maalim, akifuatiwa na Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange, na wa pili kulia ni Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na wengine ni maafisa waandamizi katika JWTZ na Umoja wa mataifa.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto Mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Mahadhi Juma Maalim, akifuatiwa na Mkuu wa Majeshi Tanzania  Jenerali Davis Mwamunyange, na wa pili kulia ni Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na wengine ni maafisa waandamizi katika JWTZ na Umoja wa mataifa.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto ni  Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange. PICHA NA IKULU

Rais Kikwete aongoza Mazishi wa Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) Makaburi ya Kisutu jijini Dar leo

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na baba mzazi wa marehemu Sajuki  wakati wa mazishi ya msanii huyo  leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam
 Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) likiwasili kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam mchana huu tayari kwa Mazishi yaliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye Kaburi la Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) yaliyofanyika mchana huu kwenye Makaburi ya Kisutu,Jijini Dar es Salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya msanii Sajuki leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.Picha Na Othman Michuzi na Ikulu

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA SAJUKI KATIKA MAKABURI YA KISUTU MUDA HUU

 Wakazi wa Jiji La Dar Wakifukia Kaburi la aliyekuwa Msanii wa Bongo Movie Juma Kilowoko maarufu kama SAJUKI
 
 Sehemu ya waliohudhuria msiba wa Sajuki katika makaburi ya Kisutu 
Wadau mabali mbali wakisubiria mwili wa Marehemu Sajuki, huku Profesa Jay akionekana kwa mbali miongoni mwa wanaousubiri mwili.
Umati wa watu ukiwa makaburini Kisutu Dar
 Mwili wa marehemu Sajuki ukiwasili katika makaburi ya Kisutu tayari kwa mazishi.Picha Kwa Hisani ya The Choice Blog

Safari ya Mwisho ya Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) kutokea Nyumbani kwenda mazikoni



 Waombolezaji wa Msiba wa Msanii wa Filamu hapa nchini,Marehemu  Sadick Juma Kilowoko wakibeba jeneza lenye mwili wake tayari kwa taratibu za kwenda Mazikoni,wakitokea Nyumbani kwa Marehemu Tabata Bima.Sasa hivi mwili wa Marehemu upo katika Msikiti wa Sheahk Adhir,Kariakoo kwa ibada ya Kusalia Mwili na baada ya Swala ya Ijumaa,Mwili utazikwa kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mwili ukipakiwa kwenye gari.
Dua ikisomwa kabla ya kuondoka na Mwili wa Marehemu kwenda mazikoni.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba akimpokea Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe alipokuwa akiwasili msibani hapo.
Waombolezaji wakiwa Msibani mapema asubuhi hii.


Pamoja na kwamba kulikuwa na Mvua kubwa lakini hakuna alitaka kuondoka msibani hapo mpaka pale mwili ulipoondoka kuelekea Msikitini kwa Kusalia na baadae kwenye Mazishi.
Mwili ukiondoka nyumbani.Picha Kwa Hisani ya Jiachie Blog

Tuesday, January 1, 2013

"KUKATAA KUWEPO TEN PERCENT KWENYE MIRADI KWANIPONZA"

Na Hastin Liumba,Uyui
 


 
 
SAKATA la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Uyui, kumvua cheo cha ukuu wa idara ya maji, injinia Nestory Nicodemus, kwa tuhuma kadhaa, limechukua sura mpya baada ya injinia huyo kudai anawasiliana na wanasheria wake ili haki itendeke.
 
Akizungumza na waandishi wa habari, injini Nestory Nicodemus, alisema kuwa suala lake limeendeshwa kimajungu na  uonevu na kwamba ametolewa kafara kwa chuki za baadhi ya watu.
 
Nicodemus alisema awali aliundiwa tume ya uchunguzi ambayo haikuzingatia kuwepo kwa changamoto kadhaa katika kile kinachoelezwa kuwa anatuhumiwa kwa uzembe, katika upotevu wa vifaa vya gari, kutokamilika kwa mradi wa maji na ujenzi wa vyoo 6 katika kata ya Kizengi.
 
“Tume niliyoundwa iliegemea upande mmoja na kwamba katika uchunguzi wao hawakuzingatia changamoto zilizoko kwenye miradi ninayotuhumiwa kutoikamilisha kwa wakati…..hii ni uonevu kwangu ikiwa ni kwa maslahi ya wachache wanaopenda ten percent.” Alisema
 
Akifafanua juu ya tuhuma hizo, injinia huyo alisema kuwa kuhusiana na mradi wa Water Sector Development Project-WSDP ulipatiwa kiasi cha sh milioni 20 ili kutekeleza ujenzi wa vyoo 6 lakini baadhi ya vifaa vilitumika kujenga nyumba kadhaa za walimu wa kata ya Kizengi.
 
Alisema licha ya mradi huo kutokamilika kwa wakati, tayari vyoo vitatu vilishakamilika, huku choo kimoja kikijengwa na wananchi, hali hiyo ya ujenzi wa nyumba za walimu na kutumika vifaa kadhaa kwenye ujenzi wa nyumba za walimu ndizo sababu zilizopelekea kutokamilika mradi huo kwa wakati na taarifa zake zipo.
 
Kuhusu tuhuma za kushindwa kukamilika kwa mradi wa maji makao makuu ya wilaya ya Uyui, Isikizya, alisema zipo sababu za msingi kwa mkandarasi aliyepewa kazi hiyo, PET Company Ltd, alipewa miezi mitano katika kazi yake ya uchimbaji wa mtaro lakini kutokana na mtaro huo kupita eneo la mashamba ya tumbaku wananchi waliomba hadi mavuno yao yaishe na mradi huo haukuwa na fedha za fidia.
 
Aliongeza kuwa suala hilo ofisi ya mkurugenzi ilikuwa na taarifa ikiwemo taarifa za mkandarasi kuomba siku 90 zaidi ili kukamilisha mradi huo, huku mradi huo pia ukichelewa kutokana na eneo hilo pia kuwa na mwamba na hivyo kazi hiyo kuwa ngumu na ya muda mrefu.
 
Kuhusu tuhuma za kutakiwa kurejesha kiasi cha sh milioni 4,420,640 ndani ya siku saba, ambazo zingejenga vyoo sita vya kata ya Msimba na Kizenge, inamshangaza kwani fedha hizo zipo kwenye akaunti benki kwani kama fedha hazikutumika ina maana zipo na hakuna wizi.
 
Alisema tuhuma nyingine ni kuhusiana na ununuzi wa mashine ya maji ya Diesel badala ya umeme, injinia Nicodemus alisema alifanya hivyo kutokana na agizo la aliyekuwa waziri wa maji Profesa Mark Mwandosya, kipindi cha mwaka 2010 alipofanya ziara kwani hakuwa na jinsi kutengua agizo la waziri hasa kutokana na kipindi hicho makao makuu ya wilaya hayakuwa na umeme.
 
Alisema maamuzi ya ununuzi wa mashine hiyo pia yalipitia kwenye vikao vya zabuni na taarifa zake zipo, huku suala la upotevu wa vifaa katika stoo ya maji kama mkuu wa idara liliripotiwa kituo cha polisi na uchunguzi unaendelea huku kampuni ya ulinzi ikijulishwa suala la mtumishi wao kuhusika na upotevu wa vifaa hivyo.
 
Aliongeza kuwa alichukua hatua kama mkuu wa idara ambaye anamwakilisha mwajiri wake ambaye ni mkurugenzi.
 
Alimalizia kuwa kutokana na maamuzi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Uyui kuketi kwenye kikao cha baraza maalumu na kumvua madaraka, amewasiliana na wanasheria wake kuangalia hatua za kuchukua ili haki zake kama mwajiriwa zipatikane.
 
Mnamo mwezi desemba 19 mwaka 2012 baraza la madiwani maalumu liliketi na kuazimia kumvua madaraka injini Nestory Nicodemus kwa uzembe wa tuhuma ainishwa.

TUWASA WASHEREHEKEA MWAKA MPYA KWA KUKAMATA WEZI WA MAJI

 Baadhi ya maafisa wa Mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Tabora Tuwasa wakiwa katika oparesheni ya kuwasaka watu wanaodaiwa kuiba maji ambapo walimkamata mkazi mmoja wa Kata ya Ipuli mtaa wa Nyerere anayefahamika kwa jina la Faston Byaba ambaye alikutwa amejiunganishia huduma ya maji kinyume cha sheria.

Mmoja kati ya mafundi wa Tuwasa akiwa amemkabidhi kifaa cha kuunganishia maji  mama aliyekutwa amejiunganishia huduma hiyo ya maji. 

WATANZANIA SASA WAFIKIA IDADI YA MIL.44.9 KUTOKA MIL.34.4



Rais Jakaya Kikwete ametangaza matokeo ya sensa ya watu na makazi, Watanzania waongezeka kutoka watu milioni 34.4 hadi kufikia watu milioni 44.9.

Monday, December 31, 2012

MAGHALA YA KUHIFADHIA BIDHAA ZA WAFANYA BIASHARA WA MWANJELWA JIJINI MBEYA YATEKETEA KWA MOTO USIKU

Maghala ya kuhifadhia bidhaa mbali mbali za wafanya biashara wa mwanjelwa Mbeya yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo maghala hayo yapo maeneo ya uwanja wa ndege wa mwanjelwa
Wanausalama wakiwa makini na vibaka ambao walitaka kuvamia eneo hilo la moto kutaka kupora mali kujifanya wanaokoa mali hizo
Hakika kikosi cha zimamoto cha jiji la mbeya wakishirikiana na kikosi cha zimamoto uwanja wa ndege wa songwe walijitahidi kuuzima moto huo ingawa mara kwa mara waliishiwa maji kutokana na uwezo mdogo wa magari hayo kubeba maji ya kuzimia moto
Moja ya gari ya kampuni ya jambo ikiungua moto katika maghala hayo
Moja ya wafanyabiashara hao ambaye anamizigo yake katika maghala hayo akikatazwa na mwanausalama kwamba asiende kuokoa mali zake kwani moto ni mkubwa awaachie kikosi cha zimamoto kifanye kazi yake
Mfayabiashara huyo haamini mcho yake huku akilia akiona bidhaa zake zikiteketea kwamoto
Hakika jeshi la polisi linastahili pongezi kwa kazi kubwa ya kuokoa mali za wafanyabiashara ambao bidhaa zao zilikuwa katika maghala hayo hapa polisi wakiwa wamemshika kibaka aliyetaka kuiba mafuta ya kupikia
Kwakweli ilikuwa hatari kwani vibaka walikuwa wanarusha mawe kwa polisi na kwa baadhi ya magari hapa hili gari ikitoka katika ghala hilo likiwa limevunjwa kioo cha mbele
Baadhi ya wananchi wengi wakiwa katika tukio hilo
Haya si maji bali ni mafuta ya kula ambayo yamemwagika baada ya blastiki kuyeyuka kwa moto
Asubuhi hii moto ndiyo unaishia
Hali halisi baada ya kuungua kwa maghala hayo hili si tope mali ni mafuta ya kula yaani mafuta ya kupikia
Baadhi ya wafanyabiashara wakijaribu kuokota baadhi ya mabaki ya bidhaa zao zilizopona katika moto huo
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Athuman Diwani akiongea na waandishi wa habari leo amesema anawapongeza sana wakazi wa Mbeya hasa wale wa maendeo yanayozunguka maghala yalioteketea kwa mtoto kwa ushirikiano wao kuwezesha kuokoa baadhi ya bidha za wafayabiashara licha ya vijana wachache kutaka kuiba na kutupa mawe askari wake ili wafanye uhalifu wa kupora bidhaa zilizokuwa zinaokolewa hapo mpaka sasa vijana wawili wamekamatwa kwa kutupiaaskari mawe na kuiba bidhaa zilizokuwa zinaokolewa
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kamanda diwani.PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG