Tuesday, December 18, 2012

SERIKALI YASITISHA UCHIMBAJI DHAHABU SIKONGE



                                        ‘‘ILI KUDHIBITI UCHIMBAJI USIO NA TIJA’’
 

Na Lucas Raphael, Sikonge

SERIKALI wilayani Sikonge, mkoani Tabora, imepiga marufuku uchimbaji wa madini ya dhahabu, unaofanywa kiholela na wachimbaji wadogo wadogo na wakubwa.

Wachimbaji hao wametoka maeneo mbalimbali,mikoa ya Mwanza,Tabora, Mbeya na Singida, ambao wamevamia maeneo ya machimbo bila kufuata taratibu za kisheria zinazoongoza rasilimali za nchi kwa manufaa ya wananchi wa eneo husika na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa wilaya ya Sikonge, Hanifa Selengu alitoa amri hiyo jana baada ya kutembelea machimbo mapya ya dhahabu yaliyoko katika kijiji kipya cha Kapumpa, kata ya Kitunda, wilayani humo, na kubaini kuwa wachimbaji wote walioko hapo hakuna hata mmoja aliyefuata sheria na taratibu zote zinazotakiwa ili kupata kibali cha kuchimba madini hayo.

Akizungumza na viongozi wa serikali ya kijiji, watendaji wa kata,watendaji wa vitongoji, wadau na wachimbaji wa madini hayo jana, mkuu huyo wa wilaya, alihoji juu ya taratibu zilizofuatwa mpaka wachimbaji hao wakaruhusiwa kuanza kuchimba dhahabu hiyo wakati halmashauri ya wilaya hiyo na ofisi yake, hawana taarifa zozote na
hakuna mtu yeyote aliyeleta barua ya maombi ya uchimbaji katika eneo hilo.

Selengu alifafanua kuwa eneo lolote lenye madini ama rasilimali, yanayochimbwa chini ya ardhi mwenye mamlaka kisheria ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete,ambapo kwa utaratibu ulivyo wachimbaji walitakiwa waanze michakato ya uchimbaji ngazi ya halmashauri ya kijiji,na baadaye kamati ya maendeleo ya kata, WDC,kabla ya kufika wilayani,lakini hayo hayakufuatwa  huku afisa
madini mkazi akitoa kibali bila taratibu zilizopo kisheria kufuatwa.

Wakijibu hoja hiyo watendaji wa kijiji na kata walisema kuwa wao hawajatoa kibali chochote cha uchimbaji wa dhahabu katika eneo hilo ila wanachofahamu ni kuwa hawa wachimbaji walikuja na leseni na barua toka ofisi ya madini mkoani Tabora, na kutuandikia barua ya utambulisho wa kuja kufanya kazi hiyo ya uchimbaji hapa kijijini.

‘Kwa kweli sisi kama serikali ya kijiji na halmashauri ya kijiji, hatukuwapa kibali chochote cha kuchimba hayo madini, wao walikuja na vibali toka mkoani.
Mheshimiwa mkuu wa wilaya…… tunashauri wachimbaji wote wasitishwe kwanza ili utaratibua ufanyike vizuri kwa manufaa ya serikali ya kijiji na wilaya yetu’’, alisema afisa mtendaji wa kata ya Kitunda Julius Ndege.

Wakitoa utetezi wao, wadau na wachimbaji hao walidai kwamba wamefuata taratibu zote halali na ndio maana serikali ya kijiji imeruhusu wachimbe madini hayo, japo walikiri kutopeleka maombi yao halmashauri ya kijiji, ofisi za halmashauri ya wilaya,mkuu wa wilaya hiyo, ili watambulike rasmi kisheria na ofisi ya mkurugenzi na mkuu wa wilaya hiyo.

Baada ya kupata maelezo toka pande zote mbili zinazohusika ili kujiridhisha,mkuu wa wilaya ya Sikonge,Hanifa Selengu, alipongeza nia njema ya hawa wachimbaji na kubainisha wazi kuwa sheria na taratibu zimekiukwa, hayumkini hawakujua kuwa ni muhimu kufuata taratibu zote kuanzia ngazi ya chini ya serikali ya kijiji, kata na hatimaye kupata kibali toka halmashauri ya wilaya husika.

‘‘Kwa kuwa taratibu zote halali zinazoweza kulinda usalama wenu ninyi wachimbaji, wanakijiji, serikali ya kijiji na wilaya kwa ujumla hazikufuatwa, natangaza rasmi kusitisha zoezi zima la uchimbaji wa dhahabu katika eneo hili la Kapumpa Kitunda Misheni,  mpaka hapo taratibu zote zinazotakiwa kufuatwa zitakapokamilika’’, alisema mkuu huyo wa wilaya.

Aidha baada ya tamko hilo,Selengu, aliagiza serikali ya kijiji na baraza la maendeleo ya kata,WDC, kuanza vikao mara moja na kuweka utaratibu mzuri ili wananchi wote wajue taratibu zinazotakiwa kufuatwa kabla ya kuanza kuchimba dhahabu hiyo.

‘‘Kuanzia leo mpaka kesho jioni, wachimbaji wote ondoeni vifaa vyenu vyote mlivyokuwa mkitumia katika eneo la machimbo, na mchimbaji yeyoye haruhusiwi kuonekana katika eneo hilo, mpaka awe amefuata taratibu zote zinazotakiwa kisheria, nashauri mchakato huu ufanyike haraka iwezekanavyo’’, aliongeza Selengu.

Awali, Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya hiyo Richard Unambwe, akifafanua taratibu na sheria zinazosimamia ardhi na madini hapa nchini, alisema, kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya Ardhi na. 5 (sura ya 114) ya mwaka 2002, umiliki na udhibiti wa madini yaliyoko ardhini uko chini ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha Unambwe aliongeza kuwa kifungu Na.6. (1) cha sheria hiyo kinazuia mtu yeyote kufanya shughuli ya uchimbaji wa madini pasipo idhini ya mamlaka husika, na kifungu cha sheria ya Ardhi Na.8(1) sura ya 114 kinaipa mamlaka serikali ya kijiji ya kusimamia ardhi hiyokupitia kamati ya ushauri ya halmashauri ya kijiji hicho.

‘‘Ndugu zangu sheria hii ya matumizi ya ardhi, kifungu  Na.8.(6) b imesisitiza kuwa matumizi ya ardhi husika yatapitishwa na WDC, pamoja na hamashauri ya wilaya husika, hivyo ni lazima wilaya ihusishwe katika suala zima la uchimbaji wa dhahabu na huu ndio utaratibu’’,alishauri Unambwe.

"TUNAMSUBIRI DR.ULIMBOKA ATOE TAARIFA KUHUSU ALIVYOTEKWA"JESHI LA POLISI



DR. STEVEN ULIMBOKA KATIKA PICHA TOFAUTI.
 
 
JESHI la Polisi nchini limesema linamsubiri Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka kufika polisi na kutoa taarifa yake rasmi kuhusu tukio lililomtokea Juni 26, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Mwananchi , msemaji wa jeshi la Polisi Advera Senso amesema wanamsubiri Dk Ulimboka afike polisi na kutoa taarifa yake rasmi pamoja na ushirikiano ili wapate kujua nini kilichotokea.

“Wakati ule hatukumhoji kwa kuwa alikuwa anaumwa tokea hapo, hatujapata taarifa yake hivyo, sisi tunamsubiri aje kutoa taarifa yake na atupe ushirikiano katika suala hilo, tunataka kujua hali yake, lakini sisi tunamsubiri aje ili tupate ushirikiano wake.”

Kabla ya polisi kutoa taarifa hiyo, Oktoba 28, mwaka huu, Dk Ulimboka aliibuka na kusema yuko imara na anajiaanda kuanika waliomteka, kumtesa na kisha kumtupa katika Msitu wa Mabwepande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Dk Ulimboka alisema kuwa kamwe hajanunuliwa na kuwa kwake kimya kwa muda mrefu kumetokana na kufuatilia kwa karibu masharti ya matibabu yake na si vinginevyo.

“Sijanunuliwa, sijawaogopa watesi wangu, wala sijanyamazishwa kwa lolote lile. Hata hao wanaoeneza taarifa kuwa nimenunuliwa, wanajua kuwa hawana ubavu wa kuninunua. 
 
Bali kimya changu kimetokana na kufuata masharti ya daktari wangu,” ameeleza Dk Ulimboka kujibu swali iwapo kimya chake kimetokana na kununuliwa.

Dk Ulimboka alikiri kuwa amewahi kusikia taarifa za yeye kununuliwa na kwamba huwa anajisikia vibaya anapoona kuna kundi la watu linahaha kutaka kupotosha ukweli na kuchafua jina lake.

“Huo ni uzushi mtupu. 
 
Hata walionitesa wanajua kuwa hawawezi kuninyamazisha au kuninunua. 
 
Wanajua sina bei katika kutetea masilahi ya Umma. Ndiyo maana wakaamua kutumia njia ile ya kinyama kutaka kunitoa roho yangu. Siwaogopi wanaodhuru mwili bali yule awezaye kutoa roho. 
 
Nakuhakikishia, muda si mrefu nitaanika kila kitu juu ya kutekwa kwangu, kuteswa na kutupwa kwenye msitu wa Mabwepande,” ameeleza.

Juni 26, 2012, Dk Ulimboka alitekwa na kuteswa vibaya ambapo alinyofolewa kucha na kutolewa meno na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande.

Mwenyekiti huyo wa Jumuia ya Madaktari Tanzania , aliokolewa asubuhi yake na wasamaria wema karibu na msitu huo, Bunju nje kidogo ya Dar es Salaam.

Akizungumza kwa sauti ya kujiamini, Dk Ulimboka, ambaye bado hajahojiwa na polisi wa Tanzania juu ya aliowataja, amesisitiza kuwa alipokamatwa alikuwa na akili timamu na kwamba waliopanga mkakati wa kumteka anawafahamu.

WANAWAKE WANAONGOZA KWA BIASHARA YA MIHADARATI.

POLISI Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya nchini, wamekamata dawa za kulevya za aina mbalimbali zenye uzito wa kilo 55,285 katika maeneo tofauti ya nchi tangu Januari hadi Desemba 15, mwaka huu.


Kukamatwa huko kumekwenda sambamba na kunaswa watu 6,929 kwa tuhuma za kujihusisha na biashara hiyo ya mihadarati, huku idadi kubwa ikiwa ni wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 25 hadi 40.
 
“Hali hii inaonyesha wazi kuwa, wanawake wanashiriki kikamilifu katika kusafirisha dawa hizi,” alisema Mkurugenzi wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP), Godfrey Nzowa na alisema na kuongeza:
 
“Sitaki kuzungumzia mtandao kama ni wa vigogo au watu wa kawaida, kikubwa ninachokifanya ni kuwakamata wahusika na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.”
Akizungumza ofisini kwake Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamanda Nzowa alisema dawa za kulevya aina ya cocaine zilikamatwa kilo 151, heroine (260), bangi 48,658 na mirungi kilo 6,216. Zinavyoingizwa nchini.

Kamanda Nzowa alisema baadhi ya dawa hizo zinaingizwa na Watanzania wenyewe kutoka nchi za nje na nyingine na raia wa kigeni kwa ajili ya kuziuza au kuzipeleka katika masoko mengine ya nje.
 
Alisema maeneo yanayotumika kusafirishia dawa hizo ni katika Bandari za Dar es Salaam na Tanga, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Pia alisema, wahusika wamekuwa wakitumia njia mbalimbali za panya kuingiza dawa hizo nchini.
 
“Tumefanikiwa kudhibiti maeneo mbalimbali ikiwamo viwanja vya ndege na bandari, lakini hawa jamaa ni wajanja na wamebadilisha njia za kuingiza dawa hizo nchini.
“Tunaendelea kupambana kwani baada ya kubana huku (bandari na viwanja vya ndege), tukabaini wanatumia bandari ndogo ya Bagamoyo, Mnazi Bay ya Mtwara kwa kuingiza au kusafirisha.”
 
Kamanda Nzowa alisema mpaka sasa kuna kesi 29 zilizopo Mahakama Kuu na watu 138 wanatuhumiwa kukutwa na cocaine, wakati 400 walikutwa na heroine. Alisema, kesi nyingine ziko katika Mahakama za kawaida ambako watu 5,544 wanatuhumiwa kukutwa na bangi na 847 mirungi.
 
“Tumejipanga kikamilifu kwa mwaka 2013 na zaidi ni kuhakikisha tunadhibiti maeneo yote yanayotumika kuingiza au kupitisha dawa hizo. Tumeweka mitego katika njia zote za panya na tukiwakamata wahusika tutawafikisha mahakamani,” alisema.

DC SIKONGE ANUSURU CHAMA CHA MSINGI KUSAMBARATIKA



Na Hastin Liumba,Sikonge

SERIKALI wilayani Sikonge,mkoa wa Tabora,imenusuru chama cha msingi

Mgambo kilichopo kata ya Kitunda,kusambaratika kufuatia wanachama
kutoridhishwa na uongozi wao wakidai ni wabadhirifu na wazembe.

Mkuu wa wilaya ya Sikonge Hanifa Selengu,ndiye aliwasihi wakulima wa

zao la tumbaku kuachana na mawazo ya kuvunja chama hicho chenye
wakulima zaidi ya 349 kugomea kulima zao la tumbaku.

Akizungumza na wanachama wa chama hicho katika viwanja vya shule ya

sekondari Kiwele,Selengu aliwataka wakulima hao kutofikiwa hatua hiyo
kwani ushirika una manufaa makubwa kwao.

“Tafadhalini nawaomba msikifie maamuzi ya kuvunja chama chenu kwani

eneo lolote lile ushirika una manufaa makubwa na kama kuna badhi ya
viongozi wabadhirifu serikali imefika na matatizo yenu
yatashughulikiwa hapa bila uonevu.

Hatua hiyo ya wakulima na kumuomba mkuu wa wilaya kuja kuwasikiliza

kilio chao,inatokana na kutoridhishwa na utendaji wa viongozi wao,huku
mtuhumiwa mkubwa ni mtunza stoo wa chama hicho,Stanford Meshack,
ambaye anadaiwa kudanganya kuwa mbolea ya pembejeo iliyosalia ghalani
imeoza wakati siyo kweli.

Aidha ukali wa wakulima hao unatokana na taarifa ya ukaguzi toka ofisi

ya ushirika wilaya ya Sikonge ya mwezi septemba 30,2012 hadi mwezi
agosti 2012 ikiwemo matumizi ya mkopo na pembejeo toka benki ya CRDB.

Katika ukaguzi huo imeonyesha kuwa daftari la mklima katika madeni yao

halikuandaliwa na taarifa hizo kupotea,huku madeni ya wakulima
kuhusiana na mkopo wa pembejeo nao hawakufuatiliwa.

Aidha kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosomwa mbele ya mkuu wa wilaya

chama kilikopa benki dola 329,427 huku marejesho ya mkopo ni dola
364,985.11 pamoja na riba,huku chama kikizalisha kilo 273,879 sawa na
mauzo dola 501,277.94 huku faida ya chama ikibaki kuwa dola
136,291.94.

Aidha taarifa ya ukaguzi toka ofisi ya mrajisi halmashauri Sikonge

imeonyesha pia kuwa malipo kwa mkulima yalistahili kuwa dola 197,398
hali ambayo inaonyesha kuwa kuna upungufu wa dola 61,106.05.

Taarifa hiyo pia inaonyesha kuwepo upotevu wa pembejeo wenye thamani

ya dola 7,848.19 yalisababishwa na mtunza stoo Stanford Meshack
aliyedai pembejeo kadhaa zilioza,madeni yaliyolazwa ni dola 12,805.47
kwa mwaka 2012,pembejeo zilizobaki kwenye mkopo ni dola 50,495.03.

Hatua hiyo ilimfanya mkuu wa wilaya ya Sikonge Hanifa Selengu,kutamka

kuwa mtunza stoo Stanford Mshack akamatwe na kufikishwa mahakamani,na
wakulima wote waliolaza madeni yao walipe mara moja,huku akiwaonya
wakulima baadhi wanaotorosha tumbaku kuwa dawa yao iko jikoni
inachemka na atawashughulikia.

Mkuu huyo wa wilaya aliagiza pia baadhi ya amdeni ya kizembe bodi ya

chama hicho itawajibika kuyalipa,huku mengine karani wa chama hicho
atalipa na mengine wanachama walipe.

Aidha umauzi wa mkuu wa wilaya ulipelekea wakulima hao kadhaa kusimama

na kumhakikishia mkuu wa wilaya kuwa mgogoro huo umeisha na wanarudi
mashambani kuzalisha mzao yote ya chakula na biashara ikiwemo tumbak
u.

SERIKALI MKOANI TABORA YASHINDWA KUSAIDIA MCHEZO WA NETBALL

 Baadhi ya wachezaji wa Netball wakipita kwa maandamano wakitoa heshima katika ufunguzi wa tamasha la kuibua vipaji kupitia mchezo huo kwa mkoa wa Tabora.
 Kabla ya kuingia katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora wachezaji walifanya maandamano na kupita mitaa kadhaa ya mji wa Tabora ikiwa ni sehemu ya hamasa.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa tamasha hilo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini Moshi Abraham maarufu Nkokota akisalimiana na wachezaji.

Uzinduzi wa tamasha la mchezo wa Netball mkoani Tabora umefanyika huku kukiwa hakuna dalili zozote kwa serikali ya mkoa wa Tabora kushiriki kusaidia mchezo huo ambao umetajwa kuwa na lengo kubwa la kuibua vipaji kwa vijana wa kike.


Mwenyekiti wa chama cha Netball manispaa ya Tabora, Zinduna Kambangwa amesema hadi kufikia hatua ya kukamilisha maandalizi ya tamasha hilo wamejitokeza wadau wachache ambao wameweza kusaidia huku akiwataja kuwa ni pamoja na Emmanuel Mwakasaka, Kisamba Tambwe,Mwanne Mchemba na Musoma Batteries.


Hata amekiri pamoja na kupeleka maombi mara kadhaa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora lakini hadi sasa hakuna majibu wala dalili zozote zinazoonesha kusaidia katika kukamilisha tamasha hilo huku hali hiyo ikiendelea kuwatia unyonge wachezaji na wadau wa mpira huo wa pete.


Aidha Zinduna amesema chama chake kitajitahidi kuendelea kutafuta wafadhiri ili waweze kufanya tamasha la aina hiyo kila baada ya miezi mitatu lengo likiwa ni kutafuta namna ya kuibua vipaji kwa wachezaji wa mchezo huo.

Tamasha hilo ambalo limewajumuisha wachezaji wa timu nne za mpira wa pete za hapa manispaa ya Tabora lilianza kwa maandamano yaliyoanzia Shule ya msingi Isike na kupita mitaa kadhaa ya mjini Tabora na kuishia katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ambapo yalipokelewa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora Moshi Nkokota.

HAFLA YA UZINDUZI WA BODI YA MFUKO WA BARABARA NA BODI YA WAKALA WA BARABARA

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiongea wakati  akizindua  Bodi ya Mfuko wa Barabara na Bodi ya Wakala wa Barabara (TANROADS) Dec 17,12,2012 jijini dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Uchukuzi na Mjumbe wa Bodi yaMfuko wa Barabara aliemaliza muda wake Mhandisi Omar Chambo akishukuru
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Dr, James Wanyancha akizungumza wakati wa  hafla ya uzinduzi wa Bodi ya mfuko wa Barabara na Bodi ya Wakala wa Bararabra (TANROADS) jijini Dar es salaam , Dec, 17, 2012.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kulia) akimpa zawadi Mjumbe wa Bodi ya mfuko wa Barabara aliemaliza muda wake kwa mujibu wa sheria za Bodi Mhandisi Omar Chambo (kushoto) ,Waziri Magufuli amemshukuru Mhandisi Omar Chambo. ambae pia  ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi pamoja na wajumbe wengine waliomaliza muda wao kwa mchango mkubwa walioutoa katika mfukona kuleta ufanisi,
Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hizo Dec,17, 2012 jijini Dar es salaam , ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (hayupo pichani)
Bodi ya Wakala wa Barabra (TANRROADS) (chinin ya mwenyekiti Hawa Mmanga ( waliokaa mwanamke)
Bodi ya Mfuko wa Mfuko wa Barabara chini ya mwenyekiti wake Dkt. James Wanyancha walioka (mbele kutoka kushoto).Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.

MEYA WA DAR MASSABURI AFURAHISHWA NA DAR METRO GAZETI JIPYA LA MATANGAZO LITAKALOGAWIWA BURE KWA WASOMAJI



 Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Mstahiki Didas Massaburi (kushoto) akikabidhiwa gazeti jipya la Dar Metro na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited inayochapisha gazeti hilo, Juma Pinto (kulia), ofisini kwake Karimjee, Dar es Salaam leo. Gazeti hilo maalumu kwa matangazo linalotolewa mara mbili kwa mwezi, hugawiwa bure kwa wasomaji.
 Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Massaburi (kushoto) akisoma gazeti jipya la Dar Metro alilopelekewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited inayochapisha gazeti hilo, Juma Pinto (kulia), ofisini kwake Karimjee, Dar es Salaam leo. Gazeti hilo maalumu kwa matangazo linalotolewa mara mbili kwa mwezi, hugawiwa bure kwa wasomaji.Kampuni hiyo huchapisha pia magazeti ya Jambo Leo, jarida la Jambo Brand Tanzania na Staa Spoti. 
 Massaburi akilipitia vizuri gazeti hilo litakalokuwa linaandikwa kwa lugha za Kiswahili na Kiingereza.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA.

SIKU YA WANAFAMILIA WA NBC ILIVYOFANA


  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (katikati) akizungumza na wafanyakazi na familia zao katika sherehe za Siku ya Wanafamilia ya benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi. Wengine
ni viongozi wa ngazi za juu wa benki hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru akiwania mpira pamoja na mfanyakazi wa benki hiyo, katika sherehe ya Siku ya Wanafamilia wa benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi.
 Watoto wa wafanyakazi wa Benki ya NBC Tanzania wakishindana kufukuza kuku ili kumpata mshindi katika sherehe ya Siku ya Wanafamilia wa benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi.
 Wafanyakazi na familia zao wakiselebuka katika sherehe za Siku ya Wanafamilia wa NBC jijini Dar es Salaam juzi.
Hapa watoto wakionyeshana nani ni mkali katika kusakata muziki kwa kutumia mtindo maarufu ujulikanao kwa jina la ‘Kiduku’ uliofanya sherehe hizo kunoga zaidi.
 Wafanyakazi wa Benki ya NBC Tanzania wakishindana kuvuta kamba ili kumpata mshindi katika sherehe ya Siku ya Wanafamilia wa benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi.
‘Father Christmas’ akigawa zawadi kwa watoto wa wafanyakazi wa benki ya NBC Katika sherehe ya Siku ya wanafamilia wa benki hiyo jijini Dar es Salaam

TASWIRA YA NDEGE YA TANAPA ILIYOANGUKA MKOA WA KATAVI, RUBANI ANUSURIKA KIFO

 

Ndege ya shirika la hifadhi ya taifa (TANAPA) yenye namba za usajili 5H-PZS aina ya C182 ikiwa imeanguka katika eneo la nsemulwa mjini Mpanda muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa mjini mpanda ikiwa inaendeshwa na rubani Adam kajwa aliepata majeraha sehemu ya uso. Ajali hiyo imetokea majira ya saa 10:55 jioni wakati ndege hiyo ikielekea hifadhi ya taifa ya katavi wilayani mlele mkoa wa katavi. picha na Walter Mguluchuma
*****
Na Walter Mguluchuma,Mpanda     
 
Ndege ya hifadhi ya taifa ya TANAPA   imepata  ajali  ya kuanguka  wilayani Mpanda mkoa wa Katavi    na rubani wa ndege hiyo  kunusurika  kifo  baada ya kupata majeruhi. Meneja wa uwanja wa ndege wa Mpanda  Mahamud Muhamed  alisema  ajari  hiyo  ilitokea jana  majila ya  saa 10  na dakika 55 jioni  katika  kijiji  cha Nsemlwa   wilayani hapo 
 
Ndege hiyo  iliyo  anguka  ilikuwa namba za usajiri  5H--  FZS aina  ya  C182  ndege ndogo  ya abiria  mari ya hifadhi ya taifa ya  TANAPA iliyo  kuwa ikiendeshwa na rubani   Adamu  Athumani  Kajwaa yenye uwezo  wa kuchukua abiria  wanne 
 
Muhamed  alieleza kuwa  ndege  hiyo   ilikuwa imetoka  katika uwanja wa ndege wa mpanda     ikielekea  katika hifadhi ya wanyama pori  ya Katavi   wilayani Mlele  Ajali  hiyo  ilitokea   umbali wa  kilometa  moja na  nusu  kutoka uwanja wa ndege wa Mpanda  mara  baada  ya  kuondoka  katika uwanja huo ambapo imeharibika sana sehemu ya bawa lake na upande wa injini.
 
 Meneja wa uwanja  huo wa ndege  alisema  taarifa za awali   zinaonyesha  chanzo   cha ajali  hiyo  kilitokana na    injini  ya ndege  hiyo  kufeli wakati ikiwa angani. Rubani wa ndege hiyo   alipata msaada  wa kuokolewa na  wananchi  waliokuwa  wakifanya  shughuli  za  kilimo  kwenye  mashamba  yao .Mmoja wa  walioshuhudi tukio  hilo  Credo Mwanisenga   alieleza  kuwa wakati   akiwa  anafanya shughuli  zake  za kilimo  ghafla  aliona  ndege  iliyokuwa  angani  ikizimika  na baada ya  muda  mfupi   ikaanguka   jirani  na mti wa mwembe 
 
Na mara  walifika katika eneo hilo  kwa lengo la kutoa msaada  hata hivyo  iliwachukuwa muda  kuanza kutoa msaada  kwa  rubani huyo  aliye kuwa ndani ya ndege  peke yake  kutokana  na eneo hilo kuwa na nyuki wengi  ambao walianza kuwashambulia waokoaji hao 
 
Hata hivyo  walieweza  kufanikiwa kumtoa  rubani  huyo   huku akiwa  amepata  majeruhi makubwa sehemu ya  uso  wake  na maumivu  sehemu ya kifua  huku akiwa anakohoa damu  na  aliewza kukimbizwa  haraka katika hosptali ya wilaya ya mpanda baada ya kupata  msaada wa gari la meneja wa uwanja wa ndege aliye fika kwenye eneo   la tukio 
 
Rubani   wa ndege hiyo aliweza kupatiwa matibabu  katika hospitali ya wilaya ya mpanda  kwa kushonwa nyuzi  nane katika  paji la uso wake  na kIsha kupewa ruhusa.

MKUU WA MKOA WA MWANZA ENG EVARISTNDIKILO ANENA KWENYE AMANI NA UTULIVU KUNA MAENDELEO

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo alipokuwa akifungua Mkutano wa RCC tarehe 14 Dec. 2012 Kwenye Ukumbiwa Chuo cha Benki Mwanza
Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Bibi Isabela Marick akisoma Muhtasari wa kikao kilichopita cha RCC.
Mada kutoka Mamlaka ya Usuluhishi na Upatanishi kuhusu masuala ya kazi nayo iliwasilishwa.
Mhe. Mbunge Ndassa wa Jimbo la Sumve akichangia moja ya mada kwenye Mkutano wa kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mwanza.
 Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa RCC wakiwa wamesimama, kukumbuka kifo cha aliye kuwa Kamanda wa Polisi wa MKoa wa Mwanza kabala
--
Na: Atleya Kuni- Mwanza.
Kikao cha kamati cha Ushauri cha Mkoa wa Mwanza (RCC),  mwishoni mwa juma hili wamekutana katika Ukumbiwa Chuo cha Benki jiji Mwanza nakujadili mambo kadha wa kadha yahusuyo maendeleo ya Mkoa Mwanza, Akifungua kikao hicho Mkuu wa Mokoa wa Mwanza Eng. Evaristi Ndikilo, Alisema lengo la kikao hicho ilikuwa kutahmini ni kwa jinsi gani wameweza kutekeleza yale yote walio azimia katika kikao  kilichopita cha tarehe 03 June 2012.

 Sambamba na kuangalia mambo mengine Mkuu wa Mkoa hakuacha kuendelea kuhubiri suala la Amani, alisema mtu anapo fikiria kuanzisha vurugu ajiulize anaanzisha vurugu kwa manufaa ya nani kwani tunapokuwa na vurugu hata shughuli za maendeleo haziwezi kufanyika kwa ufasaha.

Alihimiza juu ya kila halmashauri kuongeza vyumba vya Maabara kwa kila shule ilikufanya wanafunzi kupenda masoma ya sayansi, alisema kila Shule ihakikishe inajenga maabara tatu za sayansi yaani Baiolojia, Fizikia na Chemistry.

Kwa upande mwingine Mkuu huyo wa Mkoa alihimiza Ufugaji nyuki, Alisema suala la ufugaji nyuki halihitaji Mtaji Mkubwa kama wengine wanvyo fikiria, bali unapokuwa na Msitu tu basi nyuki wenyewe watakuja kuwekeza hapo, anachopaswa kufanya nikuandaa mizinga yako basi nyuki watakuja kuingia lakini pia tutakapofuga nyuki itasaidia katika utunzaji wa Mazingira.

Kufuatia tishio la njaa kwa baadhi ya Wilaya za MKoa huo Mkuu huyo wa Mkoa aliwahimiza wakulima na Viongozi wa Halmashauri kuhakikisha wanawahiza wakulima kutilia mkazo katika kilimo cha Mtama, kwani kitasidia sana katika kuepukana na njaa.

Wakichangia katika kikao hicho baadhi ya wajumbe wa Kikao hicho walipendekeza, Maghala ya Chakula yaliopo Wilayani Kwimba, yatumiwe na Serikali katika kuhakikisha yanakuwa ni sehemu mojawapo yakuhifadhia chakula cha Njaa, na kuacha kutegemea Bohari ya Shinyanga pekee kwani Imekuwa na usumbufu sana pindi njaa inapotokea.

Katika kikao hicho mada mbalimbali ziliwasilishwa, mada hizo ni pamoja na Hali ya kilimo na muelekeo wa Msimu wa ulimaji na upandaji, ambapo mtoa Mada katika mada hiyo, katibu Tawala Msaidizi wa Uchumi Bw. Ndaro Kulwijira alisema kwa Mkoa wa Mwanza Msimu wa Kilimo huanza Mwezi wa Nane hivyo ni vema wakulima wakalijua hilo na wakaanza maandalizi ya mapema katika kilimo.

Kwa uapande wake Afisa Mipango wa Sekretariti wa Mkoa wa Mwanza Matia Levi, mabye alitoa mada juu ya zozi la Sensa, alisema kwaujumla zozi hilo katika MKoa wa Mwanza lilienda vizuri, nakwamba Wananchiwasubiri kusikia Matokeo yatakayo tolewa na Rais wa Jamuhuri mwishoni mwa Mwezi Desemba.
 
Akifunga mkutano huo, Mkuu wa MKoa wa Mwanza ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Kikao hicho, alionya baadhi ya wajumbe wanao kimbia kuhudhuria kikao hicho na akasema kwamba kama kuna mtu anashindwa kuhudhuria vikao halali namna hii, basi kuna kila haja yakuangalia kwa upya nakutahmini sheria zinataka nini, Ndugu zangu haiwezekani mtu tu kwa sababu zake aache kuhdhuria Vikao hivi vya Kisheria tena bila hata ya taarifa halafu kesho na kesho kutwa aje atusumbe kwamba haelewi kilicho jadiliwa.

Akashauri pengine kanuni zipitiwe na Sheria ziangaliwe kwa upya ili kama ni hatua za kinidhamu dhidi ya mtu huyo ziweze kuchukuliwa RCC ndicho kikao kikubwa kabisa cha maamuzi katika ngazi ya mkoa na kipo kwamujibu wa sheria namba 19 ya mwaka 1997 juu ya uanzishaji wa Sekretarieti za Mikoa na kuhuishwa na tangazo la Novemba 2011 lililo sainiwa na Mhe. Rais.

HAWA NDIO WALIZI WETU NA MALI ZETU JE UMEGUNDUA NINI

BARABARA ITIGI ,TABORA NI BALAA TUPU


Baadhi ya wasafiri wa mabasi ya NBS na SABENA kutoka Dar-es-salaam kuelekea Tabora wakisaidia kuyang'oa magari hayo yaliyokuwa yamezama kufuatia ubovu wa barabara ya Itigi - Tabora kuharibika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo hayo.

Monday, December 17, 2012

MH LOWASSA ASHIRIKI HARAMBEE YA KANISA LA AKYERI MERU


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokelewa na viongozi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha kwa ajili ya kuongoza harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ukarabati wa kanisa hilo,iliyofanyika leo Mkoani humo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (wa tatu kushoto) akiongozana na Askofu wa Kanisha hilo la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha,Askofu Akyoo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia muda mfupi kabla ya kuanza kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea ahadi ya mchango kutoka kwa mmoja wa wamini wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiondoka kanisani hapo baada ya kumalizika kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
===========     =========   =========
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa amesisitizia tena kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni jambo la hatari kwa usalama wa nchi,wakati alipokuwa katika harambee ya kuchangia ukarabati wa kanisa la kilutheri usharika wa Akyeri Meru mkoani Arusha, Mh lowassa ameonya kuwa suala hilo lisiposhughulikiwa haraka litasababisha hali ya hatari.

''tunashuhudia maandamano katika mataifa ya ulaya vijana wakidai hali bora ya maisha pamoja na ajira.hali hiyo tusipoangalia inaweza kutokea hapa nchini kwetu.

huko nyuma niliwahi kusema kuwa makanisa, mashirika na watu binafsi wasaidie juhudi za serikali kutatua suala hilo''alisema Lowassa.

Lowassa ambaye katika harambee hiyo aliongozana na marafiki zake, ambapo yeye na familia yake pamoja na marafiki zake wamechangia kiasi cha shilingi millioni 33.2.

Zaidi ya shilingi millioni 160 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana katika harambee hiyo.

Kwa upande wake askofu Akyoo wa jimbo la Meru alimsifu Lowassa kwa uchapakazi wake popote alipokuwa.''Wakati ulipokuwa Waziri Mkuu ukimsaidia rais tulishuhudia uwezo wako mkubwa katika kufuatilia majukumu yako''alisema na kuongeza kuwa Lowassa ni mtu wa ibada