Tuesday, December 18, 2012

TASWIRA YA NDEGE YA TANAPA ILIYOANGUKA MKOA WA KATAVI, RUBANI ANUSURIKA KIFO

 

Ndege ya shirika la hifadhi ya taifa (TANAPA) yenye namba za usajili 5H-PZS aina ya C182 ikiwa imeanguka katika eneo la nsemulwa mjini Mpanda muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa mjini mpanda ikiwa inaendeshwa na rubani Adam kajwa aliepata majeraha sehemu ya uso. Ajali hiyo imetokea majira ya saa 10:55 jioni wakati ndege hiyo ikielekea hifadhi ya taifa ya katavi wilayani mlele mkoa wa katavi. picha na Walter Mguluchuma
*****
Na Walter Mguluchuma,Mpanda     
 
Ndege ya hifadhi ya taifa ya TANAPA   imepata  ajali  ya kuanguka  wilayani Mpanda mkoa wa Katavi    na rubani wa ndege hiyo  kunusurika  kifo  baada ya kupata majeruhi. Meneja wa uwanja wa ndege wa Mpanda  Mahamud Muhamed  alisema  ajari  hiyo  ilitokea jana  majila ya  saa 10  na dakika 55 jioni  katika  kijiji  cha Nsemlwa   wilayani hapo 
 
Ndege hiyo  iliyo  anguka  ilikuwa namba za usajiri  5H--  FZS aina  ya  C182  ndege ndogo  ya abiria  mari ya hifadhi ya taifa ya  TANAPA iliyo  kuwa ikiendeshwa na rubani   Adamu  Athumani  Kajwaa yenye uwezo  wa kuchukua abiria  wanne 
 
Muhamed  alieleza kuwa  ndege  hiyo   ilikuwa imetoka  katika uwanja wa ndege wa mpanda     ikielekea  katika hifadhi ya wanyama pori  ya Katavi   wilayani Mlele  Ajali  hiyo  ilitokea   umbali wa  kilometa  moja na  nusu  kutoka uwanja wa ndege wa Mpanda  mara  baada  ya  kuondoka  katika uwanja huo ambapo imeharibika sana sehemu ya bawa lake na upande wa injini.
 
 Meneja wa uwanja  huo wa ndege  alisema  taarifa za awali   zinaonyesha  chanzo   cha ajali  hiyo  kilitokana na    injini  ya ndege  hiyo  kufeli wakati ikiwa angani. Rubani wa ndege hiyo   alipata msaada  wa kuokolewa na  wananchi  waliokuwa  wakifanya  shughuli  za  kilimo  kwenye  mashamba  yao .Mmoja wa  walioshuhudi tukio  hilo  Credo Mwanisenga   alieleza  kuwa wakati   akiwa  anafanya shughuli  zake  za kilimo  ghafla  aliona  ndege  iliyokuwa  angani  ikizimika  na baada ya  muda  mfupi   ikaanguka   jirani  na mti wa mwembe 
 
Na mara  walifika katika eneo hilo  kwa lengo la kutoa msaada  hata hivyo  iliwachukuwa muda  kuanza kutoa msaada  kwa  rubani huyo  aliye kuwa ndani ya ndege  peke yake  kutokana  na eneo hilo kuwa na nyuki wengi  ambao walianza kuwashambulia waokoaji hao 
 
Hata hivyo  walieweza  kufanikiwa kumtoa  rubani  huyo   huku akiwa  amepata  majeruhi makubwa sehemu ya  uso  wake  na maumivu  sehemu ya kifua  huku akiwa anakohoa damu  na  aliewza kukimbizwa  haraka katika hosptali ya wilaya ya mpanda baada ya kupata  msaada wa gari la meneja wa uwanja wa ndege aliye fika kwenye eneo   la tukio 
 
Rubani   wa ndege hiyo aliweza kupatiwa matibabu  katika hospitali ya wilaya ya mpanda  kwa kushonwa nyuzi  nane katika  paji la uso wake  na kIsha kupewa ruhusa.

No comments:

Post a Comment