Friday, August 24, 2012

WALIOCHUKUA FOMU KUWANIA NAFASI YA KITI MKOA NA WILAYA TABORA

Kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya wenyeviti wa mkoa na wilaya kimepamba moto baada ya wananchma wa chama cha mapinduzi kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa chama hicho.

Waliojitokeza kuchukua fomu hizo ni wale waliokuwa wakishikilia nafasi zao za uongozi na wengine kujitokeza kwa mara ya kwanza kuwania uongozi wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari katibu msaidizi wa mkoa wa Tabora ,Elia Kimaro alisema kwamba hadi kufikia jana ni mwenyekiti anayemaliza muda wake Hassani Wakasuvi ndiye alikuwa amechukua fomu kwa ajili ya kutetea kiti chake hicho.

Alisema kwamba muda bado hupo hadi angasti 28 mwaka huu ambayo itakuwa ndio siku ya mwisho kuchukua na kurudisha fomu hizo kwa nafasi ya mwenyekiti na wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (nec)

Katika wilaya za Uyui waliojitokeza kuchukua fomu kuwani nafasi ya mwenyekiti wa wilaya hiyo ni Mussa Ntimizi ,Hamisi Bundala na Abdallla Kazwika ambaye natetea nafasi yake ya kiti.

Katika wilaya Igunga katibu wa wilaya hiyo Mary Maziku aliwataja waliochukua fomu hizo kwa nasafi ya wenyekiti wa wilaya hiyo ni Costa Olomi na Felix Mkunde.

Nzega aliyekuchukua fomui hizo ni Patric Bulubuza pekee hadi leo hiyo sikonge aliyechukua nafasi hiyo fomu za kuwania nafasi ya wenyekiti Abed Malifedha  ambapo kwa Tabora mjini aliyechukua fomu hiyo ni Simon Madolu .

Mwisho

Wednesday, August 22, 2012

SITTA AWASHAURI WANA-CCM KUHESHIMU MAAMUZI YA MAHAKAMA




WAZIRI WA Ushirikiano wa Africa mashariki na mbunge  wa jimbo la Urambo mkoani Tabora (CCM)  Samwel Sitta amewataka wana-CCM kuheshimu maamuzi yaliyotolewa na mahamaka kuu kanda ya Tabora ya kutengua ubunge jimbo la Igunga.

Sitta alisema kwamba mahakama imefanya kazi yake kwa kutoa uamuzi huo kwani hiyo ndio ilikuwa uamuzi ila alitaka chama cha mapinduzi kujipanga upya kama itakata Rufaa ama laa

Aliyasema hayo jana mjini Tabora wakati akikabidhi vifaambalimbali ikiwemo  Kompyuta mbili na printa zake kwa Vijana wakatoliki (VIWAWA) vyenye thamani ya shilingi milioni mbili na nusu ambazo aliwataka kuzitumia kwa makini na uadilifu mkubwa ili viweze kudumu.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo alisema, kwa kuwa Mahakama inamamlaka yake kisheria wana CCM hawana budi kuyaheshimu maamuzi hayo kwani mahakama imefanya kazi yake inavyotakikana.

“Kama kunamtu anaona hukumu hiyo haikutenda haki anaweza kwenda mahakamani kukata rufaa, lakini mimi nashauri nivyema tujipange upya tuingie ulingoni” alisema Sitta.

“Hapa mimi sina maoni juu ya jambo hilo bali chamsingi ni vyema tukakaa kutafakali yaliyotokea huko Igunga, ili basi tukiona inafaa kukata rufaa sawa, nakama tuingie ulingoni yote ni sawa” alisisitiza Bw. Sitta.

Kuhusu ufisadi ,Sitta ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alisema yeye kama kiongozi wa serikali ni vema akafuata maadili ili hata anaahidi kutoa mchango wake kwa watu hawezi kutoa kwa harakaharaka, kwani maadili yanaweza kumbana.

“Unajua sisi viongozi wa Serikali pesa zetu ni lazima uzitoe polepole ukifanya haraka utaitwa fisadi”alisema waziri Sitta.

Kwa upande wake mkuu wa itifaki wa VIWAWA jimbo kuu la kanisa katoliki ,John Pinini alisema kwamba Ni kiongozi wa kuigwa, na kuwaomba viongozi wengine wa serikalini kuwa na moyo kama huo kwa kumtolea Mungu.

Sitta ametoa kauli hiyo siku mbili baada ya  Mahakama Kuu ya kanda ya Tabora kutengua ushindi wa mbunge wa  jimbo la Igunga Dkt,Peter Dalali Kafumu, kufuatia mahakama hiyo kukubaliana na hoja za upande wa mlalamikaji dhidi ya CCM Joseph Kashindye kwamba uchaguzi huo uligubikwa na vitendo vya rushwa.

Ilielezwa kwamba Katika moja ya mikutano ya kampeni ya uchaguzi huo mdogo wa jimbo la Igunga uliofanyika mwaka jana, Rage alipita mitaani huku akiwatangazia wananchi kuwa mgombea ubunge wa Chadema amejitoa hivyo wasijisumbue kumpigia kura na badala yake wamchague mgombea wa CCM.

Mwisho



MAHAKAMA KUU NZEGA




M
ahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora, imetengua matokeo ya uchaguzi mdogo katika jimbo la Igunga mkoani Tabora, baada ya kubainika kuwa uchaguzi huo ulitawaliwa na vitendo vya rushwa, kampeni chafu na vitisho dhidi ya wapiga kura.
Jaji Mary Nsimbo Shangali wa mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora, alitangaza kutengua matokeo hayo baada ya mahakama hiyo kuridhika na hoja saba  zilizowasilishwa na upande wa mlalamikaji  kati ya hoja  17 zilizowasilishwa katika mahakama hiyo.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Mlalamikaji aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  Joseph kashindye, ambaye aliwakilishwa na wakili Maarufu nchini Profesa Abdallah Safari  ambapo alipinga mtokeo ya uchaguzi huo akilalamikia kukiukwa kwa sheria ya uchaguzi mkuu.
Upande wa Utetezi  uliwakilishwa na  mawakili Mohamed Salum Malik na Gabriel Malata kutoka ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali, Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Igunga,  na mawakili Antony Kanyama na Kamaliza Kayaga waliokuwa wakimtetea mbunge wa Igunga Peter Dalali Kafumu.
Akisoma hukumu hiyo iliyochukua saa nne, Jaji Shangali alisema kuwa mahakama imeridhika na upande wa mlalamikaji katika malalamiko yake saba, ambayo alisema yanathibitika na kuonyesha kuwa uchaguzi huo mdogo wa jimbo la Igunga haukuwa huru na haki.
Alivitaja baadhi ya kasoro zilizopelekea kutengeliwa kwa uchaguzi huo ni pamoja na  Ahadi  iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi  Dk. John Pombe Magufuli, kuhusu  ujenzi wa daraja la Mbutu ambalo alidai kwamba  kama wananchi hawataichagua CCM daraja hilo halitajengwa, wakati ambapo katika kipindi hicho kulikuwa na shida kubwa ya usafiri katika eneo hilo.
Alisema Pia Waziri huyo alitumia nguvu  na kuwatisha wapiga kura kwamba kama hawatamchagua mgombe wa chama cha mapinduzi katika Uchaguzi huo watawekwa ndani kitu ambacho alisema kinatishia uchaguzi huo kuwa huru na wa haki.
Alisema Kitendo pia kilichofanywa na mbunge wa Tabora mjini Ismail Aden Rage, hakikuwa cha uungwana kwani alitumia lugha ya uongo kwa lengo la kupotosha wapiga kura ambapo alidai mgombea wa chama cha Demokrasia na Maendeleo  ( Chadema) amejitoa katika uchaguzi huo.
Alisema pia mbunge huyo alihusika katika vitendo vya kujenga hofu kwa wapiga kura baada ya kupanda jukwaani na Bastola, hali ambayo iliwafanya wapiga kura kuhofia na hivyo kuleta dosari katika uchaguzi huo hoja ambayo alisema imezingatiwa na mahakama.
Jaji huyo wa Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Tabora,  alioonyesha kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na imamu wa Msikiti wa Ijumaa wa Igunga, Sheikh Swaleh Mohamed, kutangaza msikitini kwa waumini wa dini ya kiislamu wasikichague chama cha Chadema kwa sababu viongozi wake wamehusika kumdhalilisha aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Igunga, Fatma Kimario.
Jaji Mary pia aliithibitisha kauli iliyotolewa na katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Wilson Mkama,  kuwa chama cha Chadema kimeingiza makomandoo katika wilaya ya Igunga kwa lengo la kuvuruga uchaguzi huo mdogo ilikuwa na madhumuni ya kupeleka vitisho kwa wananchi.
Jaji Mary pia alisema kitendo cha serikali kugawa mahindi ya msaada kwa wakazi wa Igunga katika kipindi cha kampeni kitu ambacho kimeleta fadhaa kubwa kwa wapiga kura, huku akihoji je ni nani aliyekufa njaa katika kipindi hicho na kwamba kulikuwa na umuhimu gani wa kugawa mahindi katika kipindi cha kampeni.
Kuhusu hoja iliyotolewa na upande wa utetezi  ya kumtaka mlalamikaji kuwasilisha malalamiko yake kwa tume ya Taifa ya Uchaguzi badala ya kuyafikisha mahakamani, alisema kuwa hoja hiyo haina mashiko na kwamba mlalamikaji anahaki ya kupeleka malalamiko hayo katika mahakama kuu.
Kutokana na kasoro hizo, Jaji Mary alitangaza rasmi kutengua matokeo ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga na kuigaza tume ya Taifa ya uchaguzi kufuata taratibu za kufanya mchakato mwingine wa uchaguzi katika jimbo hilo.
Aliuagiza upande wa walalamikiwa ambao ni msimamizi wa Uchaguzi, Mwanasheria mkuu wa serikali na aliyekuwa mbunge wa Igunga, Peter Dalali Kafumu kulipa gharama zote za kesi hiyo.
Mamia ya watu walijitokeza kusikiliza hukumu huyo na mara baada ya kutolewa mamia ya wafuasi wa Chadema walikuwa wakishangia kwa nguvu, shamrashamra, vifijo na kisha kufanya maandamano yasiyokuwa rasmi kwa dakika kadhaa huku mashabiki, wanachama na wapenzi wa chama cha mapinduzi wakionekana kuduwaa na kutoamini kilichotokea katika mahakama.
Mahakama kuu ya Tanzania ilianza kusikiliza kesi hiyo Machi 26 mwaka huu, baada ya mgombea huyo wa Chadema kufungua malalamiko yake novemba mwaka jana, baada ya uchaguzi huo mdogo kufanyika oktoba 2 mwaka jana, kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo kwa miaka 14 Rostam Aziz.

Mwisho.

HATIMA YA KAFUMU



HATIMA  YA  KUFUMU  LEO

HATIMAYE HUKUMU ya Kesi ya kupinga matokeo yaliyo mpatia ushindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana Mbunge wa Jimbo la Igunga Dkt,Peter Dalali Kafumu kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM) katika Mahakama kuu ya kanda ya Tabora inatarajiwa kutolewa kesho mapema Agust 21 mwaka huu saa Tatu asubuhi.

Shauri hilo lilifunguli na mlalamikaji Joseph kashindye aliyekuwa mgombea mbunge kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) dhidi ya Dkt,Peter Dalali kafumu,Mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo hilo Protace Mgayane.

Shauri hilo lilianza kusikilizwa rasmi march 26 mwaka huu na Jaji Mery Nsimbo shangali.

Akizungumza na Habari leo kwa njia ya simu yake ya mkononi Hakimu Mkazi mfawidhi wilaya silvester Kainda alisema Mahakama kuu kanda ya Tabora ilipanga hukumu hiyo isomwe Agust 20 mwaka huu kutokana na siku hiyo kuwa iddi pili hivyo Hukumu inasomwa leo.

Wakili wa mlalamikaji Prf,Abdallah safari kwa njia ya simu yake ya mkononi alisema kuwa  zaidi ya malalamiko 13 waliyawasilisha katika mahakama hiyi kuu ya kanda ya Tabora.Wakili safari alisema kuwa kulingana na malalamiko hayo wanaiachia mahakama itatoa maamuzi yake’’tuaiachia mahakama itatoa hukumu kwani kwa kila kitu tumekiwasilisha na mashitaka hayo yote yalisikilizwa’’alisema safari.

Kwa upande wa mjibu madai wa kwanza Dkt,Peter Kafumu akiwakilishwa na mawakili wawili Antony Kanyama pamoja na Kayaga kamaliza.

Mmoja ya malalamiko yanayo lalamikiwa katika kesi hiyo ni pamoja na Vitishi katika uchagu huo mdogo,Kutoa ahadi ya ujenzi wa Daraja la Mbuntu pamoja na ahadi za kugawa mahindi.

Mwisho.