HATIMA
YA KUFUMU LEO
HATIMAYE HUKUMU ya Kesi ya kupinga matokeo yaliyo mpatia ushindi katika
uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana Mbunge wa Jimbo la Igunga
Dkt,Peter Dalali Kafumu kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM) katika Mahakama
kuu ya kanda ya Tabora inatarajiwa kutolewa kesho mapema Agust 21 mwaka huu saa
Tatu asubuhi.
Shauri hilo lilifunguli na mlalamikaji Joseph
kashindye aliyekuwa mgombea mbunge kupitia chama cha Demokrasia na
maendeleo(CHADEMA) dhidi ya Dkt,Peter Dalali kafumu,Mwanasheria mkuu wa
serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo hilo Protace Mgayane.
Shauri hilo lilianza kusikilizwa rasmi march 26 mwaka
huu na Jaji Mery Nsimbo shangali.
Akizungumza na Habari leo kwa njia ya simu yake ya
mkononi Hakimu Mkazi mfawidhi wilaya silvester Kainda alisema Mahakama kuu
kanda ya Tabora ilipanga hukumu hiyo isomwe Agust 20 mwaka huu kutokana na siku
hiyo kuwa iddi pili hivyo Hukumu inasomwa leo.
Wakili wa mlalamikaji Prf,Abdallah safari kwa njia ya
simu yake ya mkononi alisema kuwa zaidi ya malalamiko 13 waliyawasilisha
katika mahakama hiyi kuu ya kanda ya Tabora.Wakili safari alisema kuwa
kulingana na malalamiko hayo wanaiachia mahakama itatoa maamuzi yake’’tuaiachia
mahakama itatoa hukumu kwani kwa kila kitu tumekiwasilisha na mashitaka hayo
yote yalisikilizwa’’alisema safari.
Kwa upande wa mjibu madai wa kwanza Dkt,Peter Kafumu
akiwakilishwa na mawakili wawili Antony Kanyama pamoja na Kayaga kamaliza.
Mmoja ya malalamiko yanayo lalamikiwa katika kesi hiyo
ni pamoja na Vitishi katika uchagu huo mdogo,Kutoa ahadi ya ujenzi wa Daraja la
Mbuntu pamoja na ahadi za kugawa mahindi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment