Saturday, December 8, 2012

MSANII MAUA ANAKARIBIA KUTOA ALBUM MPYA YA VIDEO JIANDAE KUPATA VITU VIPYA







DK.SHEIN AKUTANA NA VIONGOZI WIZARA YA BIASHARA ,VIWANDA NA MASOKO

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya

Biashara Viwanda na Masoko, katika utekelezaji wa Mpango wa kazi za

Wizara hiyo katika  Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar leo. [

Picha  na Ramadhan   Othman,IKULU.]
 
Watendaji wa Wizara ya  Biashara Viwanda na Masoko, wa
Idara mbali mbali  wakiwa katika  Mkutano na  Rais wa Zanzibar na

Mwenyekiti   wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,  katika

utekelezaji wa  Mpango wa kazi za Wizara hiyo,wakiwa katika Ukumbi wa

Mikutano Ikulu Mjini  Zanzibar. [ Picha  na Ramadhan Othman,IKULU.]
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya  Biashara

Viwanda na Masoko, katika utekelezaji wa Mpango wa kazi za Wizara hiyo

katika  Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar leo,(kushoto) Makamo

wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif, [ Picha  na Ramadhan

  Othman,IKULU.]

Friday, December 7, 2012

KANISA LA MOROVIAN NYAKATO JIJINI MWANZA LAKATAA MISAADA KWA SHARTI WALILOPEWA LA KURUHUSU USHOGA NA NDOA ZA JINSIA MOJA


Ni majengo ya kituo hicho cha kanisa Morovian nyakato jijini Mwanza kilichojengwa na wananchi waumini wenyewe.





Pembeni nyumba ya ibada pembeni kituo kwa cha kulelea watoto wa mitaani, watoto yatima na waishio katika mazingira magumu, tazama eneo hili na mazingira ni kama hayo.


Kanisa la Morovian Nyakato jijini Mwanza limesema katu halitofungua milango kwa wahisani na wafadhili wanao shinikiza kanisa hilo kuruhusu ndoa za jinsia moja na suala la ushoga kama moja ya masharti ya kupata misaada.

Hilo limebainishwa jana na Mchungaji wa kanisa la Morovian lililoko Nyakato jijini Mwanza Mch. Ezekiel Yona, wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari akisema kuwa ni moja kati ya changamoto kwa kanisa lake lilizokumbana nazo wakati wa kufanikisha mradi wa ujenzi wa kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum ili kuiweka jamii pamoja na kutambua kukua kwa lindi la watoto wa mitaani, watoto yatima na waishio katika mazingira magumu linalohitaji kiasi cha shilingi milioni 43,050,000/= kukamilika.


Mch. Ezekiel amesema kuwa jengo wanalolimiliki sasa limejengwa kwa michango ya waumini wazalendo waliojitolea baada ya kukataa misaada ya mashirika ya nchi fulani (majina ameyahifadhi) ambayo yalitoa masharti kwa kanisa hilo kukubali kuwa na ndoa ya jinsia moja  ambayo ni nje ya maadili ya jamii ya watanzania na kanisa la Mungu, hivyo wameamua kuuthibitishia ulimwengu kuwa kanisa la Mungu litajengwa na washirika wenyewe.

Bofya play..



Mnamo jumapili ya tarehe 9 mwezi huu disemba 2012 Kanisa la Morovian Nyakato litaendesha harambee kuchangia kumalizia ujenzi walioanza hivyo kamati ya ujenzi wa kituo hicho wamewaomba wanajamii kushiriki katika jambo hilo ambapo viongozi mbalimbali wa kiserikali na taasisi mbalimbali wameahidi kuhudhuria.








Kuhusu suala la baadhi ya vituo kuanzishwa kwa maslahi ya wamiliki wa vituo hivyo binafsi mjumbe wa kamati ya ujenzi wa kituo hicho cha kanisa Morovian Nyakato ametoa wito kwa serikali kuunda chombo kitakacho kupitia mfumo wa uendeshaji wa asasi hizo hivyo kulea watoto kubaini mapungufu ikiwa ni pamoja na kuvifungia na kuvifuta vituo vyenye sifa zisizo stahili. Kumsikiliza Bofya play..

NAMNA MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA TANZANIA DAIMA AJERUHIWA KWA RISASI

 Shabaan Matutu akionesha sehemu ya mkono wake wa kulia ambao ulipata majeraha wakati polisi walipotumia nguvu kuingia chumbani kwake na kumtwanga risasi iliyompiga upange wa kushoto wa kifua chake.
 Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Free Media inayochapisha magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Shaaban Matutu akionesha jeraha lililotokana na kupigwa risasi na Polisi katika tukio lililotokea usiku wa kuamkia leo - baada ya polisi kuvamia nyumbani kwake Tegeta jijini Dar es Salaam kwa madai ya kumtafuta mtuhumiwa waliyekuwa wakimsaka. Matutu kwa sasa amelazwa Hospitali ya Muhimbili katika Kitengo cha Mifupa (MOI) kwa ajili ya matibabu zaidi.
 Shabaan Matutu akionesha sehemu ya mkono wake wa kulia ambao ulipata majeraha wakati polisi walipotumia nguvu kuingia chumbani kwake na kumtwanga risasi iliyompiga upange wa kushoto wa kifua chake.
 Daktari aliyekuwa zamu katika Hospitali ya Mwananyamala akiangali picha ya X-Ray ya Matutu mara baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo na kufanyiwa kipimo hicho, kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Wafanyakazi wa Free Media, Khadija Kalili kushoto na Maria Kayala (kulia) ambao walifika Hospitali ya Mwananyamala baada ya kupata taarifa za tukio hilo.Picha Zote na Habari na Dande Francis

MWANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAMU AUAWA MKOANI MARA TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KIFO

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KIFO CHA MTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU
 
Mitandao ya Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania na ule wa Watetezi Mashariki na Pembe ya
Afrika (EHAHRDN) imepokea kwa mshituko mkubwa kifo cha mtetezi wa haki za binadamu
Eustace Nyarugenda.
 
Mshituko huo unatolewa katika tamko la pamoja lililoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za
Bindamu Tanzania (THRD), Shirika la Kivulini lenye makao yake jijini Mwanza, na shirika
alilokwa akilifanyia kazi marehemu la ABC-Foudation. Mashirika mengine wanachama kutoka
Kanda ya Ziwa na nchi nzima pamoja na watu binafsi pia wameonyesha kuguswa na msiba huo ni
kusema ni pigo kubwa kwa watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania na katika ukanda wote
huo wa Ziwa.
 
Tayari Jeshi la Polisi kupitia kwa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mara Japhet Lusingu – SSP
aliyesema katika taarifa yake kwa wanahabari kwamba marehemu alifariki dunia kabla ya kupatiwa
matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Bunda alipofikishwa kwa ajili ya kujaribu kuokoa maisha
yake.

Tarifa hiyo ya polisi ilisema kwamba marehemu alikutwa katika nyumba ya kulala wageni
iitwayo Savana Bar and Guest House katika chumba namba 4 akiwa anakoroma baada ya kuvunja
mlango wa chumba hicho alichokuwa amepanga siku hiyo ya tukio majira ya saa 12.30 jioni.
 
Marehemu alikutwa akitokwa na mapovu mdomoni huku mezani kukiwa na chupa ya bia aina ya
Castle Milk iliyotumika ikiwa na pombe kidogo na chupa ya dawa ya kuulia wadudu aina ya Nivan.
Nyarugenda ambaye pia alikuwa mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na
Watoto la Action Based Community Foundation ambalo ni mwanachama, alipotea siku ya Jumatatu
tarehe 03 ya mwezi huu majira ya saa 12:00 asubuhi. Aliondoka nyumbani kwake akiwa amevaa
kaptula ya jeans rangi ya blue, tisheti na kandambili na mkononi akiwa amebeba kitabu cha kumbu
kumbu.
 
Kwa mujibu wa msaidizi wake Bw. Andreas Migiro, aliyepo katika semina ya watetezi wa haki za
binadamu jijini Dar es Salaam na binti wa marehemu anayeitwa Wema, hii ni mara ya pili kwa
marehemu huyo kupotea katika mazingira yenye utata. Tukio la kwanza lilitokea mwezi Agosti
mwaka jana na marehemu alipatikana baada ya siku nne akiwa katika hali dhaifu. Tukio la pili
limekuja baada ya mtetezi huyo kumuaga binti yake kwamba atakuwepo mjini Musoma kwa muda
na kisha ataelekea mjini Tarime.

Kwa mujibu wa Migiro katika tukio la awali wadau mbali mbali likiwamo shirika la Kivulini lilipo
jijini Mwanza walitoa ushirikiano mkubwa hadi kupatikana kwa mtetezi huyo mjini Bariadi.
Uchunguzi wa kitabibu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando ya jijini Mwanza, ulionyesha
kwamba hapakuwapo na ushahidi wa kuwekewa sumu au kitu chenye madhara kwa mtetezi huyo
mara alivyopotea mara ya kwanza. 

Hata hivyo baada ya kurejea ofisini alionyesha kuwa mwenye
dalili za kuathirika kisaikolojia lakini baadaye hali hiyo ilipotea na akaendelea na kazi kama
kawaida hadi lilipotokea tukio hili la kifo.
 
Mara ya mwisho mtetezi huyo alikuwa anaendesha zoezi la kongamano la siku 16 za kupinga
unyanyasaji wa kijinsia lililofadhiliwa na shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la
WILDAF. 

Kupotea kwake na hatimaye kifo chake huenda kukahusishwa na shughuli zake za
kupinga vitendo viovu dhidi ya wanawake na watoto lakini kwa sasa mtandao wa THRD-Coalition
unasubiri uchunguzi zaidi wa Jeshi la Polisi kwa ajili ya kutoa tamko rasmi.
Ombi letu kwa Jeshi la Polisi
 
Mtandao unalisihi Jeshi la polisi kuongeza nguvu katika uchunguzi wa mazingira na hatimaye kifo
hicho na kutoa taarifa kwa umma kuhusu kifo hichi cha mtetezi wa haki za binadamu.
Onesmo Olengurumwa,
Mratibu Wa Kitaifa
 
NI HERI KWA MTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KUBAKIA HAI KULIKO KUFA