Friday, December 7, 2012

KANISA LA MOROVIAN NYAKATO JIJINI MWANZA LAKATAA MISAADA KWA SHARTI WALILOPEWA LA KURUHUSU USHOGA NA NDOA ZA JINSIA MOJA


Ni majengo ya kituo hicho cha kanisa Morovian nyakato jijini Mwanza kilichojengwa na wananchi waumini wenyewe.





Pembeni nyumba ya ibada pembeni kituo kwa cha kulelea watoto wa mitaani, watoto yatima na waishio katika mazingira magumu, tazama eneo hili na mazingira ni kama hayo.


Kanisa la Morovian Nyakato jijini Mwanza limesema katu halitofungua milango kwa wahisani na wafadhili wanao shinikiza kanisa hilo kuruhusu ndoa za jinsia moja na suala la ushoga kama moja ya masharti ya kupata misaada.

Hilo limebainishwa jana na Mchungaji wa kanisa la Morovian lililoko Nyakato jijini Mwanza Mch. Ezekiel Yona, wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari akisema kuwa ni moja kati ya changamoto kwa kanisa lake lilizokumbana nazo wakati wa kufanikisha mradi wa ujenzi wa kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum ili kuiweka jamii pamoja na kutambua kukua kwa lindi la watoto wa mitaani, watoto yatima na waishio katika mazingira magumu linalohitaji kiasi cha shilingi milioni 43,050,000/= kukamilika.


Mch. Ezekiel amesema kuwa jengo wanalolimiliki sasa limejengwa kwa michango ya waumini wazalendo waliojitolea baada ya kukataa misaada ya mashirika ya nchi fulani (majina ameyahifadhi) ambayo yalitoa masharti kwa kanisa hilo kukubali kuwa na ndoa ya jinsia moja  ambayo ni nje ya maadili ya jamii ya watanzania na kanisa la Mungu, hivyo wameamua kuuthibitishia ulimwengu kuwa kanisa la Mungu litajengwa na washirika wenyewe.

Bofya play..



Mnamo jumapili ya tarehe 9 mwezi huu disemba 2012 Kanisa la Morovian Nyakato litaendesha harambee kuchangia kumalizia ujenzi walioanza hivyo kamati ya ujenzi wa kituo hicho wamewaomba wanajamii kushiriki katika jambo hilo ambapo viongozi mbalimbali wa kiserikali na taasisi mbalimbali wameahidi kuhudhuria.








Kuhusu suala la baadhi ya vituo kuanzishwa kwa maslahi ya wamiliki wa vituo hivyo binafsi mjumbe wa kamati ya ujenzi wa kituo hicho cha kanisa Morovian Nyakato ametoa wito kwa serikali kuunda chombo kitakacho kupitia mfumo wa uendeshaji wa asasi hizo hivyo kulea watoto kubaini mapungufu ikiwa ni pamoja na kuvifungia na kuvifuta vituo vyenye sifa zisizo stahili. Kumsikiliza Bofya play..

No comments:

Post a Comment