Wednesday, December 12, 2012

VURUGU ZAVUNJA MIKUTANO YA UKUSANYAJI MAONI YA KATIBA MPYA ZANZIBAR


Kamishna wa Tume ya mabadiliko ya Katiba, Prof Mwesiga Baregu

*Yadaiwa kujaa mamluki
  *Kisa, kupinga Muungano

 Na Mwinyi Sadallah
Mkutano wa kukusanya maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba mpya ya Muungano umevunjika kwa mara ya pili baada ya kutokea vurugu kubwa katika wilaya ya Mjini, Zanzibar huku mtu mmoja akijeruhiwa kwa kitu chenye ncha kali.

Vurugu hizo zilitokea kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Mzalendo, Jimbo Magomeni juzi na Uwanja wa Mpendae mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na kujirudia jana.

Akizungumza na NIPASHE jana, Kamishina wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Mwesiga Baregu, alithibitisha kuvunjika kwa mkutano huo kwa mara ya pili baada ya kutokea vurugu na mabishano makali baina ya wananchi kabla ya Tume kuanza kazi ya kukusanya maoni.

Alisema kwamba, juzi katika uwanja Mzalendo Magomeni watu wasiokuwa wakazi wa eneo hilo walikwenda wakiwa wamepakiwa katika magari wakitaka kutoa maoni, lakini walizuiwa na wananchi wenzao wa maeneo hayo kwa madai hawakuwa wakazi halali wa maeneo hayo.

Alieleza kwamba baada ya watu hao kufika katika uwanja huo, wananchi wakazi wa shehia ya Meya na Mpendae walipinga watu hao kutoa maoni wakati siyo wakazi wa shehia hizo.

Prof. Baregu alisema kwamba Tume baada ya kuona hali imechafuka iliamua kusitisha kazi ya kukusanya maoni kwa sababu za kiusalama hasa kwa kuzingatia kuwa haipendi kuona wananchi wakitoa maoni yao wakiwa katika ulinzi mkali wa askari wenye silaha.

Profesa Baregu alisema kwamba Tume ilikuwa na uwezo wa kuimarisha ulinzi wa polisi na kuendelea kukusanya maoni, lakini inataka wananchi watoe maoni yao wakiwa katika mazingira huru bila ya kuwapo askari wenye sare na silaha za moto.

Alisema kwamba tangu tume hiyo ilipoanza kazi ya kukusanya maoni katika wilaya ya Mjini kumejitokeza vitendo vya baadhi ya wananchi kutoa maoni kwa mvutano kati ya wanaotaka mfumo wa Muungano wa mkataba na wale wa mfumo wa Muungano wa serikali mbili, huku watu wasiokuwa wakazi wa maeneo husika wakitumika kutoa maoni.

Alisema kwamba watu hao wamekuwa wakiwahi mapema na kujipanga mwanzo kutoa maoni, kitendo ambacho huwanyima nafasi wakazi halali na kuibua vurugu katika viwanja vya kutoa maoni.

Aidha, alisema kwamba watu hao ambao siyo wakazi wa maeneo husika wamekuwa wakitaka mfumo wa Muungano wa serikali tatu ikiwamo ya Muungano wa mkataba, lakini wamekuwa wakifanya vitendo vya vurugu kama kushangilia na kuzomea kwa watu wanaotoa maoni tofauti na mtazamo wao jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu wa ukusanyaji wa maoni.

Kamishina huyo alisema hafahamu kama wananchi wanaopelekwa kwa magari kutoa maoni kama hawana nauli au katika maeneo wanayoishi hakuna huduma za kawaida za usafiri kama daladala, lakini alisema ni kosa kwa mwananchi kutoa maoni zaidi ya mara moja kwa mujibu wa sheria.

“Kwa sababu za kiusalama tukaamua kusitisha zoezi la kukusanya maoni baada ya kutokea mabishano na vurugu jambo la msingi tunaomba wananchi wazingatie sheria,’ alisema.

Prof. Baregu alisema kwamba kitendo hicho kimekuwa kikisababisha wananchi kupinga mikutano yao kuvamiwa na watu kutoa maoni wakati siyo wakazi wa meneneo hayo.

Hata hivyo, Prof. Baregu alisema kwamba Tume itaendelea na ratiba yake kama ilivyopagwa na sehemu ambayo wananchi wamekwama kutoa maoni itamua baadaye.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, Azizi Juma Mohamed, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na pia kuvunjwa kwa mikutano hiyo, lakini hakuwa na taarifa za kina kwa kuwa jana alikuwa ametingwa na shughuli za kukaguliwa kwa mkoa wake, ukaguzi unaofanywa na Kamishna wa Polisi Zanzibar. Aliahidi kutoa taarifa zaidi leo.

Hata hivyo, mashuhuda waliozungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti walisema kuwa wanahisi aliyejeruhiwa amekatwa na kisu.

NIPASHE ilifika Hospitali ya Mnazi Mmoja kutaka kujua kama wamepokea majeruhi huyo, lakini ilielezwa kwamba hakuna mtu kama huyo aliyepokewa jana hospitalini hapo.

Hata hivyo taarifa kutoka katika eneo la tukio huko Mpendae zinasema kwamba mtu mmoja alijeruhiwa kufutia vurugu hizo.

CUF WAZUNGUMZA


Akizungumza juu ya vurugu hizo kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari na Uenezi wa Chama cha Wananchi (Cuf), Salum Bimani Abdalla, alidai Kamishina wa Tume hiyo Fatma Said Ali na Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadhi ndiyo chimbuko la vurugu hizo.

“Mwakilishi Salmin Awadh Salmin, pamoja na Waziri Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Fatma Said Ali, ambaye pia ni Kamishna wa Tume wamevuruga zoezi na hatimaye wananchi kushindwa kabisa kutoa maoni yao,” alidai Bimani katika taarifa hiyo.

Alisema Cuf imeshtushwa na hali hiyo ambayo imelenga kuchafua zoezi hilo halali na pia kuinyima Tume nafasi yake ya kuendesha shughuli zake.

Alisema kwamba tokea Tume lilipoanza kazi yake mkoa wa Kusini Unguja Julai mwaka huu hadi Disemba 5 mwaka huu ilipomaliza katika wilaya ya Magharibi Unguja, haijawahi kutokea hali kama hiyo.

“CUF kinatoa wito kwa Tume kuchukua hatua zinazofaa kwa mujibu wa sheria ili kuondoa jeuri na kiburi kwa viongozi wanaotaka kuvuruga kazi ya kukusanya maoni ya wananchi” ilisema taarifa hiyo.

Bimani alisema kitendo kilichofanyika ni uvunjifu wa amani, kinyume na Sheria na pia kukiuka kifungu cha 21 (a) (i)(ii) cha Sheria ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Muungano.

CCM YAITAHADHARISHA TUME

Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimeitahadharisha Tume hiyo inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba kuwa macho na njama zinazofanywa na baadhi ya vyama vya siasa za kuandaa makundi ya vijana ambao siyo wakazi wa vituo husika vya kutoa maoni na kusababisha vurugu kutokea.

Tahadhari hiyi ilitolewa na Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi Makao Makuu ya CCM Kisiwanduwi Zanzibar, Ali Mwinyi Msuko, katika taarifa yake baada ya vurugu zilizotokea katika Jimbo la Magomeni na Mpendae wilaya ya Mjini Zanzibar.

Alisema kwamba vitendo vya kupandikiza watoa maoni mamluki vimesababisha vurugu na kuwanyima haki ya kutoa maoni wakazi halali, kitendo ambacho ni kinyume cha Sheria ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

“Vurugu hizo zimesababisha wananchi wa Shehia ya Mzalendo/Magomeni na Mpendae kushindwa kutoa maoni yao kitendo ambacho ni kuwanyima haki yao ya kikatiba,” alisema Msuko.

Alisema CCM imesikitishwa na kitendo cha watu kupakiwa katika magari na kwenda kutoa maoni katika maeneo ambayo hawaishi na kusababisha vurugu.

Aidha, alisema kwamba kitendo cha kutoa maoni zaidi ya mara moja kwa mujibu wa sheria ni kosa na wakati umefika kwa Tume kuchukua hatua kali dhidi ya watoa maoni mamluki.
CHANZO: NIPASHE

VETA KANDA YA MAGHARIBI WATAKIWA KUTOA MAFUNZO NYENYE UBORA


 
MKUU WA WILAYA YA KALIUA MKANI TABORA BW,SAVERI MAKETA AKIWASILI KATIKA VIWANJA VYA VETA AKIPOKEWA NA MURUNGEZI NA MKUU WA CHUA CHA VETA TABORA

WA KWANZA KUSHOTO NI KAIMU MKUU WA CHUA CHA ULYANKULU NA ANYEFUTA NI MKUU WA CHUA CHA VETA MKOA WA TABORA BW,MAKONGORO

MKUU WA WILAYA YA KALIUA BW,SAVERI MAKETA AKISAINI KITABU CHA WAGENI

MKURUNGEZI WA VETA KANDA YA MAGHARIBI BIBI HILDEGARDIS BITEGERA AKIWA NA MGENI RASMI SAVERI MAKETA OFISINI KWAKE

MKUU WA WILAYA YA KALIUA ALIYEMWAKILISHA MKUU WA MKOA WA TABORA AKIELEKEA KATIKA UKUMBI WA MKUTANO TAYARI KWA AJILI YA KUFUNGUA MKUTANO

WADAU WA VETA AKISIKILIZA HOTUBA YA MGENI RASMI KATIKA MKUTANO WA WADAU NA WAAJIRI ULIOWASHIRIKISHA VIONGOZI MBALIMBALI KUTOKA MIKOA YA SHINYANA,KIGOMA,SIMIYU NA TABORA


MKUU WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MKOA WA TABORA AKIWA NI MMOJAWAPO KATIKA MKUTANO HUO WA WADAU

MKUU WA WILAYA YA KALIUA ,MKURUNGEZI WA VETA WAKIWA TAYARI KUANZA KWA MKUTANO HUO





HAPA MKURUNGEZI WA VETA AKISOMA RISALA MBELE YA MGENI RASMI


MKUU WA WILA YA KALIUA AKISOMA HOTUBA KWA WADAU MBALIMBALI WALIOTOKA KATIKA MIKOA MINNE YA KANDA YA MAGHARIBI




PICHA ZOTE NA MADILI  KWA MAWASILIANO

Na Lucas Raphael,Tabora

SERIKALI imeitaka Mamlaka ya Elimu ya mafuzo na ufundi Stadi nchini kanda ya magharibi VETA kuhakikisha kuwa mafunzo wanayoyatoa yanazingatia ubora kwa kutumia mitaala iliyoandaliwa na watalaam toka viwandani.

Agizo hilo limetolewa mjini Tabora, na mkuu wa mkoa wa Tabora Bibi Fatuma Mwassa wakati akifungua mkutano kati ya VETA na waajili kutoka mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Simiyu na mwenyeji mkoa wa Tabora katika hotuba yake iliyosomwa na mkuu wa wilaya ya kaliua Saveri Maketa.

 

Katika hotuba yake mkuu huyo wa mkoa amesema kwamba VETA ni lazima ihakikishe kuwa inaajiri walimu wenye sifa na ambao wanahudhuria mafunzo ya vitendo viwandani mara kwa mara sambamba na kuwepo na karakana bora zenye vifaa vinavyokidhi mahitaji ya watalaam.

 

Aidha Bi Mwassa amesema kuwa VETA wanawajibu kuhakikisha kwamba wahusika waliopo katika sekta rasmi na isiyo rasmi, wanapata ujuzi kwa gharama nafuu wanayoweza kumudu, na kuwa ujuzi huo uwe na tija itakayokidhi mahitaji ya soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Mkuu huyo wa mkoa wa Tabora pia ameelezea umuhimu wa kusimamia ujenzi wa taifa kwa kuanzisha mafunzo ya maadili vyuoni ili vijana waweze kujitambua, kulinda afya zao, na ausalama wa maisha yao, lengo ni kuwezesha kuwa na nguvu kazi yenye afya nzuri uzalendo na maadili mazuri kwa taifa lao.

Kuhusu mafunzo kazini mkuu wa mkoa amewataka waajiri hao kutoa ushirikiano kwa VETA kwa kuwaruhusu watumishi wao na kuwapa mafunzo ya vitendo na pia kuchangia misaada mbalimbali ikiwemo mitambo kwa ajili ya kuimarisha mafunzo vyuoni kwa vitendo.

Awali mkurugenzi wa VETA kanda ya Magharibi Bibi Hildegardis Bitegera amemweleza mkuu wa mkoa kuwa VETa kanda yake, inamiliki vyuo vinne vya ufundi Stadi.

Amevitaja vyuo hivyo kuwa ni Chuo cha VETA Shinyanga chenye uwezo wa kudahili wanafunzi 400,  chuo cha VETA Tabora chenye uwezo wa kudahili wanafuzi 400,  chuo cha VETA Kigoma chenye uwezo wa kudahili wanafuzi 480 na chuo cha VETA Ulyankulu ambacho kinauwezo wa kudahili wanafunzi wapatao 280.

 

Mwisho.

SILAHA INAPOVUNJIKA KATIKA GWARIDE


 
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania akiokota moja ya silaha  iliyovunjika wakati kikosi cha Askari awa kutuliza ghasia FFU kilipotoa heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete  kwenye gwaride la miaka 51 ya uhuru lililofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Novemba 9, 2012. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

RAY C AMSHUKURU RAIS KIKWETE KWA MSAADA WA MATIBABU ,IKULU JIJINI


Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa kumsaidia matibabu,alipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C watu kushoto,Mama yake mzazi Ray C Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C.Picha na Freddy Maro
Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C leo amemtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.

Rehema aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.Kwa apande wake ,Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwaajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.

Monday, December 10, 2012

BEI YA CHAKULA TABORA YAPANDA ASILIMIA 100


BEI ya chakula katika soko kuu la mjini Tabora imepanda kwa asilimia 100, na kufanya watu wenye kipato cha chini kushindwa kumudu gharama za maisha.

Uchunguzi uliofanywa, umebaini kupanda kwa bei hiyo na hivyo kupelekea wananchi wenye kipato kidogo kushindwa kabisa kumudu manunuzi hayo.

Uchunguzi huo umebaini kwamba bei hivi sasa unga wa sembe umepanda kutoka shilingi 650, hadi kufikia kuuzwa shilingi 1500 kwa kilo moja.

Aidha bei ya mchele nayo imepanda kutoka shilingi 800, ambapo kwa sasa mchele huo unauzwa shilingi 2200, wakati maharage yamepanda kutoka shilingi 900 hadi shilingi 1900, kwa kila kilo moja.

Hata hivyo Katibu wa chama cha wafanyabiashara katika soko kuu mjini Tabora Kitwana Kaswongo amesema kuwa kupanda kwa bei hityo kunatokana na kupanda kwa gharama za usafirishaji kutoka mikoa jirani ya Rukwa na mkoa mpya wa Katavi ambako hufuatwa bidhaa hiyo.

Kasongo amesema kuwa awali gunia moja la mahindi lenye uzito wa kilo 100 lilikuwa likisafirishwa kwa shilingi 8000, lakini kwa sasa gharama hiyo imepanda hadi kufikia shilingi elfu 16,000.

Amesema kwamba wafanyabiashara wengi mkoani Tabora hufuata bidhaa hiyo kutoka mikoa hiyo lakini kutoka na kupanda kwa bei ya mafuta hapa nchini, gharama hiyo imeongezeka.

Kufuatia hali hiyo Kasongo ameiomba serikali mkoani Tabora kufanya juhudi za makusudi za kuleta mahindi ili yaweze kuuzwa kwa wananchi kwa bei nafuu kwa lengo la kuwapunguzia ukali wa maisha.

Mwisho
 Na Lucas Raphael,Tabora

HATIMAYE TANZANIA KUADHIMISHA MIAKA 51 YA UHURU.




Na. Aron Msigwa - MAELEZO.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amewaomba wakazi wa jiji la Dar es salaam kujitokeza kwa wingi kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika zitakazofanyika katika Uwanja wa Uhuru jiji Dar es salaam.

Maadhimisho hayo yameanzimishishwa mfumo wa aina yake na kuhudhuriwa na viongozi wengi wa ndani na nje ya nchi.

Akitoa ufafanuzi wa kukamilika kwa maandalizi ya sherehe hizo juzi jijini Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na mwaka huu mkoa wa Dar es salaam umepewa heshima ya kuandaa sherehe za kutimiza miaka 51 ya uhuru.

Amesema katika kipindi cha miaka 51 ya uhuru Tanzania imepata mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali za uchumi, ulinzi na usalama pamoja na uhusiano wa kimataifa.

Amefafanua kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete na kuongeza kuwa yataongozwa na kauli mbiu isemayo Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu.

Aidha amefafanua kuwa sherehe za mwaka huu zitahudhuriwa na ugeni wa marais kutoka Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na kupambwa na gwaride maalum lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania , halaiki maalum, vikundi mbalimbali vya burudani vya ngoma za asili vya hapa Tanzania hususani kutoka maeneo ya Ukerewe, Dodoma na Zanzibar.

Vikundi vingine vitakavyopamba sherehe hizo ni kundi la Taifa la sanaa kutoka nchini

MWAKYEMBE AZINDUA TRENI YA ABIRA YA MWANZA HADI DAR



Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe akipeperusha bendera kuashiria uzinduzi wa kuanza tena kwa safari za treni ya abiria kwenda Mwanza.
Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akizungumza na Uongozi wa TRL na baadhi ya Wanareli mara baada ya uzinduzi wa treni kwenda Mwanza katika stesheni ya Dar.
Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe mwenye suti akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu kabla kuzindua safari ya treni ya abiria kwenda Mwanza leo mchana katika Stesheni ya Dar es Salaam.

VIONGOZI WA SADC WATUA DAR KUHUDHURIA KIKAO CHA DHARURA


Rais Yoweri Museveni wa Uganda (kulia) akisalimiana na  Makamu wa Rais wa Tanzania Dr. Gharib Bilal  (kushoto)  alipowasili jana katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa dharura  wa Jumuiya  ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) 
 Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Msumbiji Mhe. Armando Guebuza  akipokewa na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataia Mhe. Bernard Membe
 Rais Joseph Kabila wa DRC akipokewa na Waziri wa Uvuvi Dr, David Mathayo.

 Makamu wa Rais wa Zambia Dr. Guy Scott  akifurahia jambo na Waziri wa  Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe aliyempokea
 Balozi wetu nchini Msumbiji Shamim Nyanduga (kulia) akiongea na baadhi ya maafisa wa SADC
 Kikundi cha matarumbeta cha Mount Usambara kinachoongozwa na Mzee Hoza kikitumbuiza uwanjani

 Bendera za nchi zinazojumuisha nchi za SADC zikipepea. Picha zote na Manakombo Jumaa-MAELEZO

Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika, SADC, wameanza mkutano wao wa dharura jijini Dar es salaam nchini Tanzania.  Kikao cha Asasi ya Ulinzi, Siasa na Usalama ya SADC inayojulikana kama TROIKA kilianza jana Ikulu jijini Dar es salaaam chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete.

 Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe amesema  kikao hicho cha TROIKA kimewakutanisha marais Jakaya Kikwete, Hifikepunye Phohamba wa Namibia na Jacob Zuma wa Afrika Kusini. 

Amesema mara baada ya kikao hicho cha TROIKA viongozi hao watajumuika na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye pia ni mwenyekiti wa mkutano wa kimataifa wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, pamoja na Rais Armando Guebuza wa Msumbiji ambaye ni Mwenyekiti wa sasa SADC. 


Viongozi hao kwa pamoja watajadiliana kwa kina matatizo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Madagascar na Zimbabwe ambapo watawasilisha mapendekezo yao katika mkutano mkuu wa viongozi wote 14 wa SADC utakaofanyika leo jijini Dar es salaam.

GWARIDE LA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA UHURU WA TANZANIA



Kikosi cha paredi cha Jeshi la wananchi la Tanzania (JWTZ) Kikipita mbele ya maofisa wa Vyombo vya ulinzi na Usalama wakati wa gwaride la majaribio la kuadhimisha miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania katika uwanja wa Uhuru leo asubuhi ambapo keshokutwa Desema 9 mwaka huu maadhimisho hayo yatafanyika katika uwanja huo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kikosi cha jeshi la Magereza kikipita mbele ya maofisa hao
Kikosi cha Bendera kutoka Jeshi la Wananchi la Tanzania JWTZ kikipita.
Kikosi cha Wanamaji kikitembea kwa Mwendo wa Polepole.PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM

WAMA WATOA VITANDA 80 MUHIMBILI HOSPITAL


Mwenyekiti wa Wama mama Salma Kikwete akikata utepe kama ishara ya kukabidhi vitanda 80 kwa uongozi wa Hospitali ya Muhimbili leo, kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk. Hussein Mwinyi na kushoto ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili Dk Marina Njelekela.
Mama Salma Kikwete akisoma hotuba yake mara baada ya kukabidhi vitanda 80 katika hospitali ya Muhimbili leo (kushoto) ni Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk. Hussein Mwinyi na kulia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili Dk Marina Njelekela.
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk. Hussein Mwinyi akisoma hotuba yake.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili Dk Marina Njelekela akimshukuru mama Salma Kikwete mara baada ya kupokea msaada wa vitanda hivyo leo.
Baadhi ya Mganga na wauguzi wa hospitali ya Muhimbili wakishuhudia tukio hilo.
Mama Salma Kikwete akiongozwa na Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili Dk. Marina Njelekela kushoto wakati akielekea wodini kuwatembelea wagonjwa, kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi na katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi.
Mama Salma Kikwete akimjulia hali Anna Razalo kutoka Nyegezi Mwanza mmoja wa wagonjwa wa moyo aliyelazwa hospitalini hapo.PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM