Friday, January 25, 2013

HII KALI SASA NDIZI ZACHUMBIWA TANGIA SHAMBANI KWA SHILINGI 1000 WILAYANI RUNGWE MBEYA

HII NI MIGOMBA AMBAYO NDIZI ZAKE ZIMECHUMBIWA NA WALANGUZI KWA SHILINGI 1000/ WILAYANI RUNGWE KWAKWELI MKULIMA ANAIBIWA
AKINA MAMA WA KIWIRA WILAYANI RUNGWE WAKIUZA MIKUNGU YA NDIZI KATI YA SHILINGI 1000 MPAKA 1500 KWA MKUNGU MMOJA NA WALANGUZI WANANUNUA HAPO NA KUSAFIRISHA KUPELEA DSM 
BIBI HUYU ANAUZA HUO MKUNGU WA NDIZI KWA SHILINGI 800 ILI APATE HELA YA SABUNI NA CHUMVI
HII MIKUNGU YA NDIZI TAYARI IMENUNULIWA NA WALANGUZI KWA KILA MKUNGU KWA SHILINGI 1000 MPAKA 1500 HAPO ZINASUBIRI KUSAFIRISHWA KWENDA DSM
HUYU BWANA YEYE NDIYE MWENYE BEI KUBWA KWANI MKUNGU WA NDIZI ANAUZA SHILINGI, 2500 HAKIKA SERIKALI INATAKIWA KUWASAIDIA WAKULIMA HAWA
HAPA NI KIWIRA KWENYE GULIO LA IJUMAA NDIPO WAKULIMA WANAPOLETA MAZAO YAO HAPA NA KUNUNULIWA NA WALANGUZI TOKA DSM
MZIGO WA NDIZI UNAENDELEA KUPANDISHWA KATIKA MAROLI TAYARI KWA KWENDA DSM KWA UJUMLA MKUNGU MMOJA WA NDIZI HUSAFIRISHWA KWA KATI YA SHILINGI 1OOO MPAKA 1500 KWA KWENDA DSM NA UKIFIKA HUKO HUO MKUNGU WA DIZI HUUZWA KWA SHILINGI 1,5000 MPAKA 25,000 KWAKWELI MKULIMA HAKUNA ANACHOAMBULIA ILA MLANGUZI NDIYE ANAEFAIDI MAZAO HAYO
NDIZI HIZOOOO MKUNGU MMOJA KWA SHILINGI 1000 NA UNAENDA KUUZWA DSM KWA SHILINGI 15,000 DU HII KALI
HAKIKA KWELI CHOMBO CHA MWALIMU FAIDA TUPU MUKULIMA ANAAMBULIA PATUPU
HAPA MPAKA SHILINGI 500 UNAPATA MKUNGU WA NDIZI
HAPA MWANDISH WETU JOSEPH MWAISANGO AKIBEMBELEZWA ANUNUE MKUNGU WA NDIZI KWA SHILINGI 1000/ NA WANAZIDI KUSHUSHA MAPAKA SHILINGI 700/ SIJUI ATANUNUA MKUNGU WA NANI HAPA MAANA KILAMMOJA ANAMSHAWISHI KWA BEI YAKE

PICHA NA MBEYA YETU

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA NA BIASHARA YATEMBELEA VIWANDA VYA KONYAGI NA TBL D


 Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda  na Biashara, Deo Sanga (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa,kuhusu utengenezaji wa konyagi kubwa wakati wa ziara ya kamati hiyo, kwenye kiwanda hicho, Dar es Salaam juzi.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, wakiangalia uzalishaji walipotembelea kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, Mahamoud Mgimwa (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa wakati wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea kiwanda hicho Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, wakiangalia uzalishaji walipotembelea kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Dar Es Salaam
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara wakitembelea sehemu ya mitambo ya kujaza bia kwenye chupa katika kiwanda cha TBL, Dar es Salaam
 Meneja wa Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania, Martine Calvin (kulia), akiwapatia maelezo kuhusu historia ya kiwanda hicho, wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, walipotembelea kiwanda hicho.

 Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu (kulia) akiwakaribisha wajumbe wa kamati hiyo kwenye chumba cha mikutano tayari kupata taarifa ya utendaji wa kampuni hiyo.
 Mkurugenzi wa Miradi Maalumu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Phocas Lasway akitoa maelezo jinsi ongezeko la kodi ya asilimia 25 lililovyoathiri uzalishaji wa kampuni hiyo.
 Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mgimwa akielezea jinsi watakavyoshirikiana na TBL kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazikabili kampuni hiyo.Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo (kushoto), ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), akizungumza wakati wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara walipotembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), juzi katika Makao Makuu kampuni hiyo, Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo,  Ahmed Salum na Mahamoud Mgimwa ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Wanachama na Mawasiliano wa CTI, Neema Mhondo akielezea jinsi Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kilivyopandisha kiholela ada kwa kampuni mbalimbali kutoka sh. 400,000 hadi milioni 7 kwa mwaka.
Wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza ziara kiwandani hapo.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO

BALOZI ZETU ZINAHITAJI KUJITEGEMEA:SPIKA MAKINDA



1Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasili kwenye Ubalozi wa Tanzania DRC na kusalimiana na watendaji wa ubalozi huo baada ya kupokelewa na Kaimu Balozi Mhe. Hemed Mgaza (kushoto) Spika Makinda ameandamana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulizni na Usalama, Mhe. Mussa Azzan Zungu. Spika Makinda ameshauri kuwa wakati umefika kwa balozi zetu kuwezeshwa ili zijitegemee.
2Spika Anne Makinda akisalimiana na wafanyakazi wa Ubalozi
3Spika akisaini Kitabu cha wageni
4Makamu Mwenyekiti  Mhe. Zungu akisaini kitabu cha wageni
5Picha ya Pamoja na wafanyakazi
6Jengo la Ubalozi. Jengo hili lipo kando ya barabara kuu Kinshasa, eneo maarufu kwa biashara.
7
Wajumbe kaamati maalum wakiendelea na mkutano wa FP/ICGLR

Wednesday, January 23, 2013

POLISI TABORA WAPATA PIKIPIKI 13 KWA AJILI YA KUKABILIANA NA UHARIFU


 Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Acp Anthony Rutha akimkabidhi Pikipiki mkaguzi msaidizi wa Polisi Joseph Matui katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi ya Jeshi la Polisi mkoani Tabora.


Na Beatrice Masaki - Tabora

Jeshi la polisi mkoani Tabora limepokea pikipiki  13 kutoka kwa Inspekta Jenerali  Said Mwema zitakazosaidia harakati za kukabiliana na vitendo vya uhalifu   katika mkoa huo.

Akikabidhi pikipiki hizo kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, ACP Anthon Rutha amesema kuwa,pikipiki hizo zitagawiwa kwa wakaguzi wa kila tarafa wa wilaya za Igunga ,Uyui,Urambo ,Sikonge,Nzega na Tabora mjini  kwa lengo la kusaidia ulinzi  na usalama wa wananchi.

 Kamanda huyo wa polisi wa mkoa wa Tabora ametoa  wito kwa wakaguzi wa kila tarafa kuzitumia pikipiki hizo  kwa malengo yaliyokusudiwa na si kuzitumia kwa matumizi binafsi na kuwataka wazitunze  vizuri kwani kwa kufanya hivyo , kunaweza kusaidia kudhibit uhalifu kwa wakati na kuimarsha amani mkoani hapa.

Akipokea pikipiki hizo kwa niaba ya  wakaguzi wa tarafa mkoani hapa mkaguzi wa polisi Joseph Matui wa tarafa ya Tabora kaskazini amesema kuwa, pikipiki hizo zitawasaidia kufika maeneo ambayo wananchi wanahitaji kujua mambo  mbalimbali ikiwa ni pamoja na  juu ya ulinzi na usalama wa mali zao.

 Matui  amewataka wananchi kuonesha ushirikiano kwa askari  jeshi la polisi  pindi wanapofika katika maeneo yao  na pika wawe tayari  kuwafichua wahalifu.

MAAFA STENDI YA UBUNGO JIJINI DAR-ES-SALAAM


ubungo1 6ac3f
ubungo2 cc0a5
SEHEMU ya ukuta wa kituo cha mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo, jijini Dar es Salaam, leo alfajiri umeanguka na kuyaharibu vibaya magari zaidi ya ishirini yaliyokuwa yameegeshwa nje ya eneo hilo. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela alisema kuwa idadi ya magari yaliyopatwa na ajali hiyo yanakadiriwa kufikia 24 ambapo watu watatu wanasemekana wamejeruhiwa.
ubungo3 3104f
ubungo4 27999
ubungo5 bb613
ubungo c5ed1

Monday, January 21, 2013

JK AWASILI UFARANSA KWA ZIARA YA SIKU TATU



1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na mke wa Rais wa Mali Mama Touré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu.
1c37
Mama Salma Kikwete akiongea na mke wa Rais wa Mali Mama Touré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu.
2Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mke wa Rais wa Mali Mama Touré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu.

Wanawake waendelea kufariki kwa matatizo ya uzazi Mbeya


 MRATIBU WA HUDUMA ZA AFYA NA MTOTO HOSPITALI YA MKOA WA MBEYA, PRISCA BUTUYUYU.

LICHA ya Serikali kutambua na kusema kuwa Lengo la Milenia ni kufikia vifo 54 kwa kila vizazi hai 1,000 ifikapo mwaka 2015, wanawake 906 wamefariki dunia kwa matatizo ya uzazi mkoani Mbeya.

Akizungumza katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi ofisni kwake mwishoni mwa mwaka 2012, Mratibu wa huduma za Afya na mtoto katika Hospitali ya mkoa wa Mbeya Prisca Butuyuyu alisema kuwa kati ya vifo hivyo wilaya ya Mbeya Jiji ndiyo inayoongoza kwa vifo vilivyotokana na uzazi na kufuatiwa na wilaya ya Mbarali.

‘’Wilaya ya Mbeya City inaongoza kuwa na vifo vingi ambapo kwa kipindi cha mwaka 2011 vifo vimetokea 363 sawa na asilimia109, Mbarali vifo 172 sawa na asilimia 58, Chunya 150 sawa na asilimia 63, wilaya ya Ileje vifo 145 sawa na asilimia 33 na wilaya ya Rungwe vifo 133 sawa na asilimia 55’’

‘’Wilaya zingine ni wilaya ya Mbeya Vijijini vifo 113 sawa na asilimia 38, Wilaya ya Mbozi vifo 105 sawa na asilimia 45 a wilaya ya Kyela vifo 88 sawa na asilimia 67 na katika takwimu hizi wilaya ya Kyela kuna uhalisia tofauti  na wilaya zingine’’ alisema Butuyuyu.

Anazitaja baadhi ya sababu ambazo zinasababisha vifo vitokanavyo na uzazi kuwa ni pamoja na ugonjwa wa Maralia, damu kupungua kwa mama mjamzito, kutokwa kwa damu nyingi wakati wa kujifungua, uambukizi wa homa kali, huduma hafifu, VVU na kifafa cha Mimba.

Anakiri kuwa vifo hivyo na takwimu walizonazo kama Hospitali ya mkoa inadhihilisha kuwa hawajafikia kiwango cha kuridhisha cha jamii kupata uelewa madhubuti wa kujifungulia katika vituo vya Afya na Hospitali kwani asilimia 40 wanajifungulia nje ya vituo vya huduma ikiwemo nyumbani ama kwa Wakunga wa jadi na ndiyo maana jedwali (Grafu) la vifo linapanda na kushuka.

Alitoa wito kwa viongozi wa kata na vijiji kusaidiana na Wizara ya afya na ustawi wa jamii  kwa kutoa elimu  kupitia mikutano ya adhara kwa jamii hususan wakinamama wajawazito  kuondokana na dhana ya kujifungulia majumbani au kwa wakunga wa jadi ili kuondokana  na changamoto hiyo inayochangiwa na uelewa mdogo wa kushiriki katika vituo vya afya na zahanati hususan vijijini.

Alisema katika kukabiliana na hilo  wizara ya afya inamikakati kabambe  ya kuhakikisha  kuwa elimu hiyo inatolewa vijijini ambapo ndio kuna changamoto kubwa ya mwamko duni ya wakinamama wajawazito  kujifungulia katika vituo vya afya na zahanati.

Alisema kuwa utafiti uliofanywa umegundua  changamoto hiyo   inachangiwa na kuwepo kwa uhaba wa vyombo vya usafiri  ubovu wa miundombinu  na umbali  wa vituo vya afya na kwamba  serikali kupitia wizara ya afya inatakiwa kufanya jitihada za haraka kusogeza  huduma za afya vijijini ili kunusuru vifo vya wakinamama wajawazito wakati wa kujifungua na watoto.

":Hii ni changamoto kubwa kwa serikali na kwamba mikakati inatakiwa kuwepo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kutosha kwa jamii kutambua umuhimu wa kujifungulia katika vituo vya afya na zahanati ili kuondokana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza wakati wa kujifungua ikiwa ni pamoja na kupatiwa kinga za kuzuia maradhi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto"Alisema Butuyuyu.

Aidha alisema  takwimu za mkoa wa Mbeya katika kipindi cha mwaka 2011 kwa wilaya ya Ileje ndio inayoongoza kwa tatizo hilo kutokana na kuwa na idadi ndogo ya akina mama wanaojifungulia kwenye vituo vya afya.

 Alisema katika wilaya ya Ileje ni asilimia 33 tu ya akina mama wajawazito walijifungulia kwenye vituo ambapo asilimia 57 walijifungulia majumbani huku wilaya ya mbeya mjini ndio ambayo ina idadi kubwa ya akina mama wanaojifungulia kwenye vituo ambapo asilimia 109 ya akina mama wajawazito walijifungua kwenye vituo vya afya .

Kwahisani ya Gordon Kalulunga, Mbeya