Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea,
namkariri Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye
barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani
au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea
Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga
wilayani Muheza
hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo
chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya
Muheza”
Kamanda amesema hakuna kona kali sana
wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati
ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu
haitembei.
Kwenye gari alikua mwenyewe