Na Lucas Raphael,Tabora
NAIBU Waziri wa
Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Goodulack Ole Medeye amewataka watumishi wa
wizara hiyo ambao wanaona mshahara wanaolipwa na serikali hautoshi waandike
baarua ya kuacha kazi ,badala ya kuendelea kuomba na kuwashawishi wananchi kwa
Rushwa kwa watu masikini.
Kauli hiyo wa wziri inafuatia kutolewa kwa malalamiko
kutoka kwa wakazi wa mkoam wa tabora na wilaya zake juu ya watumishi wa Idara
hiyo kukithiri kwa kuomba na kupokea Rushwa .
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Mandeleo ya makazi, alitoa
kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Sekondari
ya Uyui mjini Tabora, ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa ni kusikiliza kero
mbalimbali za wananchi zinazohusiana na masuala ya ardhi na makazi.
Medeye aliwaambia wafanyakazi idara ya ardhi katika
Manispaa ya Tabora kwamba kama kunamtumishi wa
idara hiyo ambaye anaona mshahara anaolipwa hautoshi hana budi kuandika barua
ya kuomba kuacha kazi badala ya kuwa wanaomba rushwa kwa wananchi wanaohitaji
huduma ya kupatiwa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi.
“Mimi naona kama
unaona mshahara wako unaolipwa na serikali haukutoshi, andika barua kwa mkuu
wako ya kuacha kazi nasio kuwadhurumu wananchi masikini” alisema Medeye.
Alisema kuwa kwa muda mrefu sasa amekuwa akisikia
malalamiko mengi kutoka kwa wananchi dhidi ya watumishi wa idara ya ardhi
katika Manispaa ya Tabora hivyo akamwagiza mkuu wa wilaya ya Tabora ,Suleiman
Kumchaya, kuwachukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwafirisi mali zao,
watumishi wa idara hiyo watakaobainika kupora maeneo ya wananchi na kuwauzia
matajili.
Kwa upande wake Naibu Waziri huyo alielezea jinsi
ambavyo alitaka kupewa rushwa ya dola laki 8 ili atoe upendeleo wa kugawa eneo
fulani na kampuni moja ambayo hata hivyo hakuitaja, lakini alikataa kuchukua.
“Mimi nilikataa rushwa ya dola laki 8 sasa ninyi hapa
Tabora nawashangaa mnaendekeza vijirushwa hivi vidogo vitawasaidia nini, kwanza
angalia huyu mtu unayechukua rushwa kwake anahali gani” alihoji Medeye.
Katika mkuatano huo mmoja wa wananchi ,Juma Rashid
Nasssro alimtaka Naibu Waziri Medeye, kuondoka na Mwenyekiti wa baraza la ardhi
wilaya ya Tabora, kwamadai kwamba amekuwa akitoa maamuzi katika kesi za ardhi
kwa kuwapendelea watu wenye kipato cha juu nasio masikini.
Aliendelea kumshambulia Mwenyekiti huyo wa baraza la
ardhi mbele ya Naibu waziri kwamba, amekuwa akiwapendelea matajili na
kwanyanyasa wanyonge katika kesi za ardhi, na kusisitiza kwamba ahamishwe
Tabora.
“Mheshimiwa Waziri tukuomba unapoondoka uondoke na
huyu Mwenyekiti wa baraza la ardhi Tabora, huyu anatunyanyasa sana
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la ardhi wilaya
ya Tabora Emmanuel Sululu, alipotakiwa kuthibitisha madai hayo alisema kuwa
madai hayo hayana ukweli wowote.
“Unajua mtu anapokwenda mahakamani huwa anatarajia
kuwa atashinda, hakuna anayeenda mahakamani kwa matarajio ya kushindwa, sasa
mimi ninapotoa maamuzi ya haki kwa mtu ambaye sio mwelewa ataona napendelea,
kumbe hapana” alisema Sululu.
Mwisho