Tuesday, October 9, 2012

WATAKIWA KUACHA KAZI KAMA WANAONA MISHAHARA HAITOSHI

Na Lucas Raphael,Tabora

NAIBU Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Goodulack Ole Medeye amewataka watumishi wa wizara hiyo ambao wanaona mshahara wanaolipwa na serikali hautoshi waandike baarua ya kuacha kazi ,badala ya kuendelea kuomba na kuwashawishi wananchi kwa Rushwa kwa watu masikini.

Kauli hiyo wa wziri inafuatia kutolewa kwa malalamiko kutoka kwa wakazi wa mkoam wa tabora na wilaya zake juu ya watumishi wa Idara hiyo kukithiri kwa kuomba na kupokea Rushwa .

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Mandeleo ya makazi, alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Sekondari ya Uyui mjini Tabora, ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa ni kusikiliza kero mbalimbali za wananchi zinazohusiana na masuala ya ardhi na makazi.

Medeye aliwaambia wafanyakazi idara ya ardhi katika Manispaa ya Tabora kwamba kama kunamtumishi wa idara hiyo ambaye anaona mshahara anaolipwa hautoshi hana budi kuandika barua ya kuomba kuacha kazi badala ya kuwa wanaomba rushwa kwa wananchi wanaohitaji huduma ya kupatiwa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi.

“Mimi naona kama unaona mshahara wako unaolipwa na serikali haukutoshi, andika barua kwa mkuu wako ya kuacha kazi nasio kuwadhurumu wananchi masikini” alisema Medeye.

Alisema kuwa kwa muda mrefu sasa amekuwa akisikia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi dhidi ya watumishi wa idara ya ardhi katika Manispaa ya Tabora hivyo akamwagiza mkuu wa wilaya ya Tabora ,Suleiman Kumchaya, kuwachukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwafirisi mali zao, watumishi wa idara hiyo watakaobainika kupora maeneo ya wananchi na kuwauzia matajili.

Kwa upande wake Naibu Waziri huyo alielezea jinsi ambavyo alitaka kupewa rushwa ya dola laki 8 ili atoe upendeleo wa kugawa eneo fulani na kampuni moja ambayo hata hivyo hakuitaja, lakini alikataa kuchukua.

“Mimi nilikataa rushwa ya dola laki 8 sasa ninyi hapa Tabora nawashangaa mnaendekeza vijirushwa hivi vidogo vitawasaidia nini, kwanza angalia huyu mtu unayechukua rushwa kwake anahali gani” alihoji Medeye.

Katika mkuatano huo mmoja wa wananchi ,Juma Rashid Nasssro alimtaka Naibu Waziri Medeye, kuondoka na Mwenyekiti wa baraza la ardhi wilaya ya Tabora, kwamadai kwamba amekuwa akitoa maamuzi katika kesi za ardhi kwa kuwapendelea watu wenye kipato cha juu nasio masikini.

Aliendelea kumshambulia Mwenyekiti huyo wa baraza la ardhi mbele ya Naibu waziri kwamba, amekuwa akiwapendelea matajili na kwanyanyasa wanyonge katika kesi za ardhi, na kusisitiza kwamba ahamishwe Tabora.

“Mheshimiwa Waziri tukuomba unapoondoka uondoke na huyu Mwenyekiti wa baraza la ardhi Tabora, huyu anatunyanyasa sana

Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la ardhi wilaya ya Tabora Emmanuel Sululu, alipotakiwa kuthibitisha madai hayo alisema kuwa madai hayo hayana ukweli wowote.

“Unajua mtu anapokwenda mahakamani huwa anatarajia kuwa atashinda, hakuna anayeenda mahakamani kwa matarajio ya kushindwa, sasa mimi ninapotoa maamuzi ya haki kwa mtu ambaye sio mwelewa ataona napendelea, kumbe hapana” alisema Sululu.

Mwisho 

No comments:

Post a Comment