Saturday, January 12, 2013

DIWANI WA CCM AKAMATWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KUKATA WANAWAKE VICHWA



 

NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
 
MWENYEKITI wa chama cha mapinduzi,(CCM),Hassan Wakasuvi,amesema kilimo cha tumbaku mkoani Tabora,wakulima wake wataendelea kuumia kufuatia baadhi ya watumishi wa serikali, na askari polisi kujiingiza katika ulanguzi wa zao hilo katika kipindi cha masoko.
 
Wakasuvi alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibuni baada ya mkutano mkuu wa chama kikuu cha wakulima wa tumbaku kanda ya magharibi,(WETCU),mkoani humo.
 
Alisema hali ikiendelea itafikia mahali zao la kumnufaisha mkulima itakuwa ndoto hivyo ni vyema serikali ya mkoa ikafuatilia hilo na kulifanyika kazi ili haki za wakulima zionekane na siyo ilivyo sasa.
 
“Katika mkutano mkuu wa WETCU ambao uliambatana na uchaguzi,mkuu wa uongozi wake, wapo wakulima waliotoa kero ya baadhi ya watumishi wa serikali na askari polisi wanajihusisha na ulanguzi wa zao la tumbaku.” Alisema.
 
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kufuatia wakulima hao kulalamika hayo,hata yeye ameshafanyika kazi lalamiko hilo na kuona ipo haja ya kuweka wazi tatizo hilo ili kuondoa dhuluma iliyopo ikiwezekana kuwataja kwa majina endapo wataendelea na biashara hiyo.
 
Alisema amewasilisha kilio hicho kwa mkuu wa mkoa wa Tabora,Fatma Mwassa ili aweze chukua hatua stahiki dhidi ya watumishi wa serikali na serikali wanaojihusha na ulanguzi wa tumbaku ambapo mkuu huyo wa mkoa amesema atafuatilia kwa ukaribu na kuchukua hatua.
 
Wakasuvi aliongeza kuwa yupo tayari kumtetea mkulima yoyote kati ya wale waliotoa malalamiko yao mbele ya mwenyekiti wa WETCU Alcard Iragila kuwa kuna watumishi wa serikali na askari polisi wanalangua tumbaku kipindi cha mauzo na masoko.
 
“Tuhuma hizi ni za kweli wala hakuna haja ya kusingizia mtumishi wa serikali ama askari polisi……siyo majungu ni tuhuma za ukweli na tutapigania hili hadi mwisho na tabia hii ya dhuluma kukomeshwa kabisa.”alisema 
 
Alisema kuwa anajua kuwa wakulima waliothubutu kutamka kuwa askari polisi na baadhi ya vigogo wa serikali wanalangua tumbaku kipindi cha masoko ya zao hilo watasumbuliwa, lakini anaamini kuwa anawatetea kwa nguvu zote hadi pale haki inapatikana.

RAIS JK - "KUNA HAJA YA KUUNDWA HALMASHAURI MBILI WILAYA YA UYUI"

 Rais Kikwete akifungua jiwe la msingi ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Tabora hadi Nyahua.
 Mkuu wa wilaya ya Uyui Bi.Lucy Mayenga akiwa jukwaani kwa lengo la kuwasalimia wananchi na kumkaribisha Rais Kikwete katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara.
 Baadhi ya Waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Uyui nao walitoa mpya baada ya kukosa viti vya kukalia katika mkutano wa hadhara wakaamua kukaa chini wakiwa na shauku ya kumsikiliza Rais Kikwete kwenye viwanja vya Chipukizi Tabora mjini.


Na Lucas Raphael,Tabora.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika  ziara yake ya kikazi mkoani Tabora amesema kuwa kuna haja ya kuundwa Halmashauri mbili katika wilaya ya Uyui ili kusogeza karibu huduma za maendeleo kwa wananchi.

Akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Uyui katika kata ya Ilolangulu alisema serikali yake itatekeleza ombi lao la kuwa na halmashauri mbili katika wilaya moja, huku akiahidi kuiagiza wizara ya ardhi na maendele ya makazi kupima ardhi ya vijiji hivyo ili waweze kupata hati ya kumiliki ardhi ili waweze kukopesheka katika taasisi za fedha.

Alisema hipo haja ya kuwa na halmashauri hizo mbili ilikuwaze kusongeza mahitaji muhimu kwa wananchi hasa ukizigatia hoja yaumbali mrefu kutioa ilolagulu hadi Isikizya .

Dkt kikwete alisema kwamba licha ya umbali huo lakini hipo haja kwa wananchi kuwa karibu na utawala wao ili kusuma maendeleo kwa wananchi na wapiga kura wa wilaya ya uyui na jimbo la Tabora Kaskazini.

Akizungumzi swala la ardhi Rais kikwete alisema kwamba hatamwangiza wazri husika kufika katika kijiji hicho ili kiweze kupimwa na hatimaye wananchi wa kata hiyo waweze kupata hati na kupata mikopo katika taasisi za fedha .


Awali Rais Kikwete alimtaka mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Ilolangulu wilayani Uyui kueleza kero zinazowakabili wananchi wake ambapo mwenyekiti wa serikali ya kijiji, Ali Magowa, alimweleza kuwa wananchi wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusafiri umbali mrefu kufwata huduma za kiutawala, kuwa na ardhi ambayo haija piwa na kukosekana kwa maji safi na salama.

Hata hivyo alisema kwamba mradi wa milenia mbola bado unahitaji kuendelezwa na serikali ili kuwasaidia wananchi wa vijiji 16 mabvyo vipo chini ya maradi huo.

Alisema mradi wa viojiji vya milenia ni muhimu sana kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania kwani umesaidia kupunguza umaskini kwa idadi kubwa ya wajkazi wa vijiji hivyo .

Alisema kwamba haba baada ya mradi huo kulimza muda wake serikali itaendelea kuendeleza ili kuwa wasaidia wananchi kuendelea kupata mafanikio ya tanfa lao.

Akizungumzia huduma duni za maji waziri wa maji nchini Prof, Jumanne Maghembe, amesema vijiji hivyo vitapatiwa huduma ya maji safi na salama katika kipindi kifupi kijacho.

Alisema utafiti wa upatikanaji wa maji katika vijiji hivyo ulifanywa na jaica ulisitishwa baada ya nchi ya Japan kukumbwa na tetemeko la tsunami ambapo kwa sasa serikali ya Japan ipo teari kuendelea na utekelezaji wa mradi huo.

Wilaya hii ya  uyui mkoani Tabora ambayo wananchi wake wanahitaji kusogezewa huduma za kijamii, kiutawala inatarafa 3, ambazo ni Ilolangulu, Igalula na Uyui, ina kata 24 na vijiji 120  ikikadiriwa kuwa na watu wapatao 372,761 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 .

Friday, January 11, 2013

HAKUNA MTANZANIA ATAYEKUFA KWA NJAA -JK

 
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya watoto wanaoishi katika kijiji cha Igombe manispaa ya Tabora wakati wa ziara yake hapa mkoani Tabora.

 
 
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya watoto wanaoishi katika kijiji cha Igombe manispaa ya Tabora wakati wa ziara yake hapa mkoani Tabora.
 
 
Na Lucas Raphael,Tabora

RAIS wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete amewatoa hofu watanzania na kusema kwamba hakuna mtanzania yoyote atakaekufa kwa njaa japo maeneo mengi ya nchi yamekuwa yakilalamikia tatizo la kuwepo kwa njaa kwa baadhi ya mikoa na wilaya.
 
Kauli hiyo aliitoa juzi wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya chipukizi mjini Tabora wakati wa ziara yake mkoani hapa.
 
Alisema kwamba kutokana na tatizo la njaa kwa baadhi ya mikoa serikali ipo tayari kuhakikisha hakuna mwananchi ama mtanzania atakaye kufa kutokana na janga hilo.
 
Alisema kwamba tayari srikali imejipanga kuhakikisha kila mtu anapata chakula cha msaada kupitia kamati za mahafa za wilaya kata na mkoa kwa ajili ya kupatiwa chakula hicho .
 
Dkt Kikwete alisisitiza kwamba hifadhi za chakula zilizopo katika mikoa ya shinyanga kwa ukanda huu inachakula cha kutosha kwa ajili ya wananchi wa mikao ya ukanda huu.
 
Hata hivyo alisema kwamba kama chakula kitakwisha kwenye magahala yan hifadhi za taifa serikali ipo tayari kuangiza chakula hicho hata nje ya nchi ili kuakikisha kuna mtu anayejkufa kwa kukosa chakula .
 
Alisema kwamba licha ya ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa tayari kimefanya  tathimini ya mahitaji ya chakula kwa baadhi ya mikoa na wilaya hapa nchini na katika maghala ya hifadhi ya chakula na kuonyesha kuwa  bado kipo na chakutosha kwa mikoa ambayo imeomba chakula kwa ajili ya wananchi wake .
 
Rais kiwete akizungumzia swala la ukimwi alisema bado maambukizi ya ukimwi yanatishia maisha ya watanzania wengi na kuwataka wanatanzia watumia kinga kwa ajili ya kufanya tendo hilo.
 
Alisema kwamba kitendo cha wananchi wengi nchini kupata maambukizi ya ukimwi na ukimwi imekuwa si cha dharula bali ni chakujitakia na cha makusudi kwani kabla ya kwenda kwenye haadi lazima kupanga wapi mkutane na kufanya kitendo hicho.
 
Alisema kwamba sasa kabla ya kufanya inabidi kila mtu hatafute kinga na nani haje nayo ili kuwaza kujikinga na mambakizi hayo ya ukimwi .
 
“jamani hali ya maambukizi ya ukimwi nchini yanatisha lakini basi tumieni kinga ili maambukizi hayo yasiongezeke kwani kitendo hicho kipangwa muda na saa sasa nini kinashindikana kununua kinga ili kuwaze kujikinga wote na maambukizo hayo”.alihoji rais kikwete.
 
Alisema kwamba katika kipindi cha januari hadi septemba mwaka jana mkoa wa tabora jumla ya watu 41,032 walipimwa ,kati hao wanaume 19 ,531 na wanawake 21,591.
 
Alisema kuwa watu 3,136 walikutwa na maambukizi ya ukimwi kati yao ni wanaume 1,324,na wananwake 1820sawa na asilimia 7.6 kwa wale waliopima hali hii inaonesha bado maambukizi yapo juu.
 
Dkt kikwete aliendelea kusema kwamba watu 39,659 wanahudhuria klinik na kati ya hao watu 20,486 wanatumia dawa na ARVs ambao ni sawa na asilimia 51.6 .
 
Alisema kwamba kwa hali  hiyo ni mbaya sana hivyo kila mmoja wetu anawajibu mkubwa wakujilinda afya yake .
 
Hata hivyo Rais Jakaya Kikwete  amewahakikishia wananchi wa tarafa ya iloloagulu katika wilaya ya Uyui kuwa swala la wilaya hiyom kuwa na halmashauri mbalin linawezekana ili kupunguza kero kwa wananchi hao.
 
Awali mwenyekiti wa srikali ya kijiji cha ilolagulu ,Ally Magowa alimwambia Rais kwamba wananchi wa kijiji hicho wamekuwa wakitembea umabli mrefu kw ajili ya kupata huduma za kiserikali kutoka hapo hadi Isikizya .
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
  

JK AZINDUA UJENZI WA MRADI MKUBWA WA MAJI TABORA


 Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo ya ramani ya miundombinu ya maji mjini Tabora kutoka kwa mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Tabora Tuwasa,wakati wa uzinduzi wa ujenzi mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 7.5.
 Waziri wa maji Prof.Jumanne Maghembe akitoa maelezo kwa Rais JK wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa maji katika mitambo ya bwawa la Igombe mkoani Tabora.

 Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na majitaka mjini Tabora Tuwasa Injinia Mkama Bwire akitiliana saini ya mkataba wa ujenzi mkubwa maji mbele ya Rais Kikwete wakisimamiwa na Waziri wa maji Prof.Maghembe.

SERIKALI KUFUFUA SHIRIKA LA RELI TANZANIA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete (yumo garini kushoto) akikagua sehemu ya kutua na kupaa ndege ya uwanja wa Tabora leo Januari 10, 2013 mara baada ya kuzindua rasmi ujenzi wake
Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli (kulia)  na Waziri wa  Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe wakiongea wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Tabora leo Januari 10, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe Radhia Msuya mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataikfa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea mkoani Tabora alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku tano kukagua shughuli za maendeleo na kuzindua miradi mbalimbali.(PICHA NA IKULU)
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 
 
SERIKALI imetangaza hatua kubwa na kabambe za kufufua usafiri wa abiria na mizigo,  ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mabehewa na injini za treni, katika hatua kubwa za aina yake kuchukuliwa na Serikali kwa muda mrefu katika kurekebisha usafiri wa treni nchini.
Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Harrison George Mwakyembe ametangaza hatua hizo leo, Alhamisi, Januari 10, 2013, wakati alipokuwa anamkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuweka jiwe la msingi kwenye ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Ndege wa Tabora ikiwa ni tukio la mwisho la ziara yenye mafanikio makubwa ya siku tano ya Rais Kikwete katika Mkoa wa Tabora.

Mheshimiwa Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete na mamia kwa mamia ya wananchi waliohudhuria sherehe ya uwekaji jiwe hilo la msingi kwenye Uwanja huo kuwa Wizara yake imeanza kubadilisha reli nyepesi, iliyochakaa na yenye uzito mdogo kwa Reli ya Kati.
Amesema kuwa kwa kupitia mashirika yake ya RAHCO na Shirika la Reli Tanzania (TRL) Serikali itafanya marekebisho hayo makubwa njia mzima ya Reli ya kati na kuwa mafundi wa mashirika hayo tayari wamefika Mkoa wa Morogoro.

Waziri Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete kuwa Serikali kupitia Wizara yake na mashirika yake hayo, imeagiza mabehewa mapya ya mizigo 274, imeagiza mabehewa mapya ya abiria 22, imeagiza mabehewa mapya ya kubebea kokoto 25 na pia imeagiza mabehewa ya breki (brake vans) 34 na tayari malipo ya awali yamefanyika.

Katika namna inayothibitisha dhamira ya Serikali kurekebisha hali ya usafiri wa reli nchini, Mheshimiwa Mwakyembe pia amewaambia wananchi kuwa Wizara yake pia imeagiza crane mpya na kubwa ya kubebea mizigo yenye uzito unaofikia kilo 100.

Kuhusu injini za treni, Waziri Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete kuwa zabuni kwa ajili ya kutengeneza upya (re-manufacturing) injini nane za treni imetolewa ili utengenezaji huo ufanyike, iwe ni ndani ama nje ya nchi.
 
Pia Waziri amesema kuwa oda imetolewa kwa ajili ya utengenezaji wa injini mpya 13 za treni ambazo malipo yake yatafanyika katika mwaka ujao wa fedha hata kama utengenezaji wa injini hizo utaanza.

Aidha, Waziri amesema kuwa Wizara kupitia mashirika yake hayo mawili imeagiza spea za kutosha kuweza kufanya ukarabati mkubwa wa injini tano kwenye karakana zilizoko hapa nchini.

“Mheshimiwa Rais, kwa hesabu nyepesi tu ni kwamba katika kipindi kifupi tutaweza kuwa na injini kiasi cha 26 ambazo zitarudisha uhai wa usafiri wetu wa reli kwa kiasi kikubwa sana,” Waziri Mwakyembe amemwambia Rais Kikwete.

 Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
 10 Januari, 2013

WAHARIRI NA BARAZA LA HABARI WATEMBELEA VITENGO VYA TUME YA KATIBA



 Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Assaa Rashid (wa pili kulia), akitoa ufafanuzi uhifadhi wa maoni ya maandishi yanawasilishwa na wananchi katika Tume kwa wadau wa Taasisi za Habari nchini waliotembelea ofisi za Tume leo (Januari 10, 2013). Taasisi zilizotembelea Tume ni Baraza la Habari Tanzania (MCT), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na Jukwaa la Wahariri (TEF).
 Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Mohammed Khamis Hamad akitoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa uchambuzi wa maoni ya wananchi kwa Ujumbe wa Taasisi za Habari nchini uliotembelea ofisi za Tume leo (Januari 14, 2013). Taasisi zilizotembelea Tume ni Baraza la Habari Tanzania (MCT), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na Jukwaa la Wahariri (TEF).
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Hanifa Masaninga akitoa ufafanuzi kuhusu uandaaji wa maoni ya wananchi na kuwa Kitengo cha Taarifa Rasmi (Hansard) kwa ujumbe wa Taasisi za Habari nchini waliotembelea ofisi za Tume leo (januari 10, 2013). Taasisi zilizotembelea Tume ni Baraza la Habari Tanzania (MCT), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) na Jukwaa la Wahariri (TEF).
Picha na Tume ya Katiba.

POLISI TABORA WAKOSANYA ZAIDI YA MILIONI 400

Na Lucas Raphael,Tabora

Jeshi la Polisi mkoani Tabora, limesema kuwa  limekusanya kiasi cha shilingi milioni 445.9 kwa kipindi cha mwaka jana, ikiwa ni fedha zilizotokana na tozo za  adhabu za makosa ya usalama barabarani.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tabora, ACP Antony Ruta, amesema kuwa kiasi hicho cha fedha zilizokusanywa na jeshi hilo kimetokana na makosa  14,604 yaliyofanyika katika kipindi cha mwaka jana katika wilaya zote saba za mkoa huo.

Alisema kwa mujibu wa takwimu hizo idadi ya makosa ya usalama barabarani yaliyofanywa na madereva katika mkoa huo imeoongezeka kwa aslimia 100 ikilinganishwa na makosa ya usalama barabarani yaliyofanywa  mwaka juzi ambayo ni 7,589 na kuingiza shilingi milioni 196.5 kutokana na tozo za makosa hayo.

Akizungumzia takwimu za makosa ya jinai yaliyofanyika katika mkoa huo kwa kipindi cha mwaka jana, Kamanda Ruta, alisema kuwa jumla ya makosa 18,586 yamefanyika katika mkoa huo na kulipotiwa katika vituo mbali mbali vya polisi ikilinganishwa na makosa 19,172 yaliyofanyika kwa kipindi cha mwaka juzi. Kukiwa na upungufu wa makosa 586.

Akizungumzia takwimu zilizotokana na vifo vilivyosababishwa na ajali za barabarani,  kamanda alisema kuwa jumla ya watu 152 walipoteza maisha katika matukio  118 ya ajali yaliyotokea mkoani Tabora kwa kipindi cha mwaka jana huku watu 765 wakijeruhiwa na baadhi yao wakipata ulemavu wa kudumu.

Kamanda alitoa wito kwa madereva kuendesha magari kwa tahadhari kubwa, kuepukana na mwendo kasi usiokuwa wa lazima na kufuata sheria na taratibu ili kuokoa maisha ya abiria wasiokuwa na hatia.


Mwisho.

Thursday, January 10, 2013

DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AMEFANYA IBADA YA SHUKRANI NA KUTOA MSAADA WA BAISKELI 10 KWA WALEMAVU WA MIGUU

Mimi ni nani mbelezako bwana mpaka ukanijalia kuwa hai hadi hii leo nakushukuru mungu kuniokoa katika majanga mbalimbali ya mwaka uliyopita hasa kwenye ile ajali iliyonitokea Mbalizi kwani zaidi ya watu 12 walifariki hayo ni baadhi ya maneno aliyokuwa akitamka Dr Mary Mwanjelwa kwenye ibada ya shukrani iliyofanyika katika kanisa la Moravian ushirika wa Ruanda jijini Mbeya
Dr Mary Mwanjelwa akiwa na naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo wakiimba kwa pamoja katika ibada hiyo ya shukrani

Ndugu jamaa na marafiki toka sehemu mbali mbali walihudhuria ibada hii ya shukrani
Tizo kijana aliyemwokoa mweshimiwa Dr Mary Mwanjelwa kwenye ajali mbaya iliyotokea mwaka jana maeneo ya mbalizi Mbeya hapa akielezea jinsi aliyomwokoa anasema ni mungu tu ndiye aliyetenda hayo maajabu kwani hakujua kabisa kama huyo dada ni mbunge wengi waliogopa kwenda kwenye gari alimokuwamo mbunge kwani moto mkubwa ulikua umeanza kuwaka akajikuta tu kaamua kwenda kwenye gari hiyo baada ya kuona mkono wa kuomba msaada na alipofika ilibidi avunje kioo cha gari hiyo na kumtoa Dr Mary Mwanjelwa kwenye gari hiyo huku moto ukiendelea kuwaka 
Kijana Tizo akilia akisema huwenda mungu alikuwa na makusudi yake kunifanya mimi niwe daraja la kumuokoa dada Mary 
Mchungaji Nyambo  naibu waziri Mulugo na mkewe wakiwa makini kumsikiliza Tizo jinsi alivyomwokoa Dr Mary Mwanjelwa
Ndugu jamaa na marafiki wakimsikiliza Tizo

Hili ndilo gari alimokuwemo mweshimiwa mbunge Dr Mary Mwanjelwa katibu wake aliteketea kabisa kwenye gari hilo
dreva wagari ya mbunge kwa sasa anaendelea vizuri bado yupo kwenye matibabu DSM
Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini Magharibi Alinikisa Cheyo Ndiyo aliongoza ibada hiyo ya shukrani
Add caption
Naibu waziri wa elimu Philipo Mulugo na Dr Mary Mwanjelwa wakicheza pamoja na kwaya ya Debora Mwaisabila kanisani hapo
Debora Mwaisabila akiwa na waheshimiwa wabunge wakimtukuza mungu kwa wimbo
Kwaya ya Paradise ikiimba kanisani hapo
Mweshimiwa mbunge Dr Mary Mwanjelwa ametoa msaada wa baiskeli 10 za walemavu wa miguu  zenye dhamani ya shilingi milioni 2.5  hapa akiwa pamoja na walemavu hao baada ya kuwakabidhi baiskeli zao

ASKARI POLISI 7 WANATUHUMIWA KWA KUMPIGA NA KUMJERUHI RAIA MBOZI MBEYA


Kamanda Diwani

Na mwandishi wetu.
 Askari polisi saba wa kituo cha polisi Mbozi wanatuhumiwa kwa kumpiga, kumjeruhi na kumsababishia maumivu makali Laiton Mwakalinga mwenye umri wa miaka 33 mkazi wa Kijiji cha Haterere.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Laiton Mwakalinga alipigwa na askari wakati akipeleleka malalamiko dhidi ya shemeji yake aliyemtishia kumuua ambapo askari hao walimtaka atoe kiasi cha shilingi elfu arobaini na alipogoma ndipo walipoanza kumpiga hadi kumvunja mkono.
 Kutokana na kitendo hicho Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwani Athumani ameahidi kulifuatilia tukio na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa haraka na zenye ukweli ili tatizo kutafutiwa ufumbuzi ili kupatikana kwa haki sawa kwa raia na vyombo vya usalama.
Aidha amesema kitendo cha askari kumpiga raia ni kosa na halitakwi kufumbiwa macho na kwamba askari kuwakamata raia na  kuwapiga sio utaratibu na haipo katika utaratibu wa upelelezi wa jeshi hilo nani kosa la jinai na lisichukuliwe kama ni utaratibu wa Polisi bali ni wa mtu binafsi askari mmoja mmoja kujichukulia umamuzi.

JINAMIZI LA MOTO LAANZA TENA MWAKA HUU LACHOMA MADUKA MAWILI USIKU WA KUAMKIA LEO MWANJELWA MBEYA

Moja ya duka ambalo lilianza kuwaka moto mida ya saa tatu usiku kutokana na hitirafu ya umeme likiwa na baadhi ya nguo zilizoungua kwa moto huo maduka hayo yapo jirani na kituo cha afya cha Ruanda jijini Mbeya
Mbeya yetu haikuweza kuwahi kwenye tukio ilikuta tayari kikosi cha zimamoto mbeya kwa kushilikiana na jeshi la polisi walikwisha zima moto huo kwa ujumla wakazi waeneo hilo la mwanjelwa wamewashukurusana kikosi cha zimamoto na polisi kwa kuwahi kwenye tukio na kuuzima moto huo
Baadhi ya wamilikiwa maduka hayo wakilia kwa uchungu baada ya kuona baadhi ya mali zao zilivyoteketea kwa moto
Baadhi ya wafanyabiashara wa eneo hilo la mwanjelwa wakimfariji mwenzao ambae duka lake limeungua
Hili ndilo eneo la maduka ya wafanya biashara wa nguo mwanjelwa yalionusurika kuwaka moto jana usiku


Picha na Mbeya yetu