Kamanda Diwani
Na mwandishi wetu.
Askari polisi saba wa kituo
cha polisi Mbozi wanatuhumiwa kwa kumpiga, kumjeruhi na kumsababishia maumivu
makali Laiton Mwakalinga mwenye umri wa miaka 33 mkazi wa Kijiji cha Haterere.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
na Laiton Mwakalinga alipigwa na askari wakati akipeleleka malalamiko dhidi ya
shemeji yake aliyemtishia kumuua ambapo askari hao walimtaka atoe kiasi cha
shilingi elfu arobaini na alipogoma ndipo walipoanza kumpiga hadi kumvunja
mkono.
Kutokana na kitendo hicho
Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwani Athumani ameahidi kulifuatilia tukio na
kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa haraka na zenye ukweli ili
tatizo kutafutiwa ufumbuzi ili kupatikana kwa haki sawa kwa raia na vyombo vya
usalama.
Aidha amesema kitendo cha askari
kumpiga raia ni kosa na halitakwi kufumbiwa macho na kwamba askari kuwakamata
raia na kuwapiga sio utaratibu na haipo katika utaratibu wa upelelezi wa
jeshi hilo nani kosa la jinai na lisichukuliwe kama ni utaratibu wa Polisi bali
ni wa mtu binafsi askari mmoja mmoja kujichukulia umamuzi.
No comments:
Post a Comment