MRATIBU WA HUDUMA ZA AFYA
NA MTOTO HOSPITALI YA MKOA WA MBEYA, PRISCA BUTUYUYU.
LICHA ya Serikali kutambua na kusema kuwa Lengo la Milenia ni
kufikia vifo 54 kwa kila vizazi hai 1,000 ifikapo mwaka 2015, wanawake 906
wamefariki dunia kwa matatizo ya uzazi mkoani Mbeya.
Akizungumza katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi
ofisni kwake mwishoni mwa mwaka 2012, Mratibu wa huduma za Afya na mtoto katika
Hospitali ya mkoa wa Mbeya Prisca Butuyuyu alisema kuwa kati ya vifo hivyo
wilaya ya Mbeya Jiji ndiyo inayoongoza kwa vifo vilivyotokana na uzazi na
kufuatiwa na wilaya ya Mbarali.
‘’Wilaya ya Mbeya City inaongoza kuwa na vifo vingi ambapo kwa
kipindi cha mwaka 2011 vifo vimetokea 363 sawa na asilimia109, Mbarali vifo 172
sawa na asilimia 58, Chunya 150 sawa na asilimia 63, wilaya ya Ileje vifo 145 sawa
na asilimia 33 na wilaya ya Rungwe vifo 133 sawa na asilimia 55’’
‘’Wilaya zingine ni wilaya ya Mbeya Vijijini vifo 113 sawa na
asilimia 38, Wilaya ya Mbozi vifo 105 sawa na asilimia 45 a wilaya ya Kyela
vifo 88 sawa na asilimia 67 na katika takwimu hizi wilaya ya Kyela kuna
uhalisia tofauti na wilaya zingine’’ alisema Butuyuyu.
Anazitaja baadhi ya sababu ambazo zinasababisha vifo vitokanavyo
na uzazi kuwa ni pamoja na ugonjwa wa Maralia, damu kupungua kwa mama mjamzito,
kutokwa kwa damu nyingi wakati wa kujifungua, uambukizi wa homa kali, huduma
hafifu, VVU na kifafa cha Mimba.
Anakiri kuwa vifo hivyo na takwimu walizonazo kama Hospitali ya
mkoa inadhihilisha kuwa hawajafikia kiwango cha kuridhisha cha jamii kupata
uelewa madhubuti wa kujifungulia katika vituo vya Afya na Hospitali kwani
asilimia 40 wanajifungulia nje ya vituo vya huduma ikiwemo nyumbani ama kwa
Wakunga wa jadi na ndiyo maana jedwali (Grafu) la vifo linapanda na kushuka.
Alitoa wito kwa viongozi wa kata na vijiji kusaidiana na Wizara
ya afya na ustawi wa jamii kwa kutoa elimu kupitia mikutano ya
adhara kwa jamii hususan wakinamama wajawazito kuondokana na dhana ya
kujifungulia majumbani au kwa wakunga wa jadi ili kuondokana na
changamoto hiyo inayochangiwa na uelewa mdogo wa kushiriki katika vituo vya
afya na zahanati hususan vijijini.
Alisema katika kukabiliana na hilo wizara ya afya
inamikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa elimu hiyo inatolewa
vijijini ambapo ndio kuna changamoto kubwa ya mwamko duni ya wakinamama
wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya na zahanati.
Alisema kuwa utafiti uliofanywa umegundua changamoto
hiyo inachangiwa na kuwepo kwa uhaba wa vyombo vya usafiri
ubovu wa miundombinu na umbali wa vituo vya afya na kwamba
serikali kupitia wizara ya afya inatakiwa kufanya jitihada za haraka
kusogeza huduma za afya vijijini ili kunusuru vifo vya wakinamama
wajawazito wakati wa kujifungua na watoto.
":Hii ni changamoto kubwa kwa serikali na kwamba mikakati
inatakiwa kuwepo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kutosha kwa jamii kutambua
umuhimu wa kujifungulia katika vituo vya afya na zahanati ili kuondokana na
changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza wakati wa kujifungua ikiwa ni
pamoja na kupatiwa kinga za kuzuia maradhi kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto"Alisema Butuyuyu.
Aidha alisema takwimu za mkoa wa Mbeya katika kipindi cha
mwaka 2011 kwa wilaya ya Ileje ndio inayoongoza kwa tatizo hilo kutokana na
kuwa na idadi ndogo ya akina mama wanaojifungulia kwenye vituo vya afya.
Alisema katika wilaya ya
Ileje ni asilimia 33 tu ya akina mama wajawazito walijifungulia kwenye vituo
ambapo asilimia 57 walijifungulia majumbani huku wilaya ya mbeya mjini ndio
ambayo ina idadi kubwa ya akina mama wanaojifungulia kwenye vituo ambapo
asilimia 109 ya akina mama wajawazito walijifungua kwenye vituo vya afya .
Kwahisani ya Gordon Kalulunga, Mbeya
No comments:
Post a Comment