Mnamo tarehe 17.01.2013 majira ya saa
23:00hrs huko katika eneo la kiwira kata ya Kiwira wilaya ya Rungwe mkoa wa
mbeya. Joseph s/o Mwaenga, miaka 32, Kyusa, mwendesha pikipiki @ bodaboda na
mkazi wa kiwira. Alijimwagia mwilini mafuta aina ya petroli na kisha kumwagia
mafuta mengine kituo kidogo cha polisi kiwira na kutoa kiberiti kwa nia ya
kutaka kujilipua. Mtuhumiwa alidhibitiwa na askari waliokuwa zamu kwa kumkamata
na kumuweka chini ya ulinzi. Hakuna madhara ya kibinadamu wala mali
yaliyotokea. Chanzo cha tukio hili ni mtuhumiwa kufanya fujo katika
kijiwe/kituo chake cha bodaboda akiwa amelewa na alipotaka kukamatwa na
wananchi alikimbia hivyo wananchi kuichukua pikipiki yake na kuisalimisha kituo
cha polisi Kiwira ndipo mtuhumiwa alikwenda kituo cha polisi akiwa bado amelewa
huku akiwa na dumu la mafuta ya petroli. Taratibu za kisheria zinafanywa ili
mtuhumiwa afikishwe mahakamani. Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishna
msaidizi wa polisi Diwani athumani anatoa wito kwa jamii kutokutumia vilevi kupita
kiasi kwani inaweza kusababisha madhara makubwa pasipo kutarajia.
Signed
By,
[DIWANI
ATHUMANI – ACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment