Thursday, January 17, 2013

MUSOMA UTALII YAJENGA CHUO CHAKE TABORA

Shabani Mrutu mkurugenzi wa Chuo Cha Musoma Utalii Tabora

   NA MWANDISHI WETU TABORA
UKOMBOZI wa taifa letu kwa kizazi cha sasa na kijacho,  jambo lamsimngi zaidi ni elimu bora ni suala muhimu sana ambalo litasaidia kuondokana na hali ya umasikini,maradhi na ujinga ambao umekithiri
miongozi mwa watanzania waliowengi kwa sasa.

Chuo cha musoma utalii,kilichopo mkoani Tabora, ni chuo  kilichosajiliwa na “NACTE” kinachoendesha mafunzo ya kozi mbalimbali na kimekuwa kikitoa elimu inayolingana na hali halisi ya sasa ya sayansi na teknolojia.

Aidha chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo ua juu ya kozi kama vile  uongozaji wa  watalii,hotel management,uwalimu wa chekechea, uandishi wa habari na utangazaji, secretarial na Computer hali iliyopelekea kufanikiwa  kutoa wahitimu bora waliofanikiwa kuajiriwa
na kujiairi ili kwenda sanjari na changamoto za soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Mkurugenzi wa chuo cha Musoma Utalii tawi la Tabora, Shabani  Mrutu,alisema hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake alisema chuo kimekuwa ni chuo cha  mfano wa kuigwa,na kimbilio la wengi na hadi sasa chuo hicho kimeanza ujenzi wake.

Alisema ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 80, ambapo kutakuwa na  mabweni yanayoweza kuchukua wanafunzi zaidi 200,vyumba vya madarasa 10,jengo la utawala la ghorofa na maktaba ya  kisasa,jiko la kisasa,ukumbi na sehemu za  mapumziko.

Alisema kuwa mkoa wa Tabora una vivutio vingi vya kitalii lakini  haviendelezwi ipasavyo hivyo ujenzi wa chuo mkoani hapa ni ukombozi mzuri ambao utasaidia vivutio hivyo kuonekana na hatimaye kukuza secta
ya utalii mkoani Tabora.

Mrutu alifafanua zaidi kuwa chuo hicho kilianzishwa mwaka 2004 kikiwa  na wanafunzi 42 na sasa kuna wanafunzi 280,ambapo chuo kilikua chini ya usimamizi VETA.

Aidha mkurugenzi huyo aliongeza kuwa chuo hadi sasa,kimesajiliwa na  kutambulika na NACTE kwa barua ya awali yenye kumb. Namba NACTE/BA/77/465/605/Vol 1/9 usajili ambao ulianza mwaka 2012.

Anabainisha kuwa chuo kina matawi mengi nchini ili kuwafikia vijana  wengi zaidi kwa gharama nafuu sana.

Mafanikio toka 2004 hadi sasa kampasi ya Tabora. Mrutu anabainisha kuwa mafanikio kwa tawi la Tabora,ni kuongezeka kwa  wanafunzi toka 2004 wanafunzi 42 hadi 280 mwaka 2012.

Akizungumzia mafanikio katika utoaji wa elimu katika chuo  hicho,  mkuu huyo wa chuo alisema wamejipanga vyema kutoa elimu bora na zaidi chuo kina kwa kuenmdelea kuongeza walimu ambapo hadi sasa kuna waalimu 18 wenye sifa zinazotambulika kisheria.

Alisema ili kuweza kutoa elimu bora pia wanafunzi wa chuo hicho  wamekuwa wakienda mafunzo ya vitendo kulingana na kozi wanazosoma katika mikoa mbalimbali.

Mkurugenzi huyo anaongeza kuwa wanafunzi hupelekwa katika hotel kubwa  za kitalii,kampuni za uongozaji watalii ,TANAPA na kozi za ufundishaji chekechea hupelekwa katika shule za kiingereza,wengine vituo vya radio kwa wanafunzi wanaochukua masomo ya uandishi wa habari.

Alisema maeneo mengine ya kitalii wanafunzi hao hupelekwa kwenye  makumbusho ya Kwihara nje kidogo ya mji wa Tabora, sehemu ambayo makumbusho hayo yana historia ya kipekee kwa mkoa na taifa kwa ujumla.

Akizungumzia muitikio wa wanafunzi  kujiunga na chuo ni mzuri kwani  kila wanapochukua wanafunzi kila muhula idadi huwa inaongezeka kulingana mahitaji halisi,ambapo sifa zilizowekwa ni wanafunzi
waliohitimu kidato cha nne hadi cha sita.

Malengo na matarajio ya chuo:

Mkurugenzi huyo Shabani Mrutu, alisema chuo hadi sasa kinakamilisha majengo yake tawi la Tabora,ambayo yanatarajiwa kukamilika ndani yamiezi Tisa ujenzi huo unatarajia kukamilika kwa gharama ya zaidi ya sh
milioni 800.

Alisema malengo mengine ni kusajili  kozi nyingi zaidi kwenda NECTA,sanjari na kusajili chuo kiweze kutoa elimu ya juu kutokana na kozi zilizopo.

Aidha malengo mengine ni kuweza kusajili wanafunzi watakaofikia  1000,kuongeza matawi nchini ili chuo kiweze kutoa huduma bora zaidi kwa jamii tena kwa gharama nafuu na kutoa elimu bora yenye ushindani
katika soko la ajira.

Kuhusu changamoto zilizopo:

Kuhusu changamoto zilizopo mkurugenzi huyo alisema chuo kimekuwa  kikikabiliwa na changamoto kadhaa ambazo ni uelewa wa jamii katika vyuo binafsi kwani imejengeka fikra potofu vyuo binafsi wahitimu huwa
hawawezi kupata ajira na kwamba fikra hizo ni potofu kwani vyuo binafsi na vya serikali vina nafasi sawa ilimradi viwe na usajili unaotambulika serikalini. “Ipo dhana ya namna hiyo lakini tumekuwa tukijitahidi sana kutoa elimu kwa wazazi na zaidi ufaulu na ksaidia wanafunzi kujiajiri na kuajiriwa kumekuwa kukitusaidia kuondoa dhana hiyo potofu.” Alisema.

Alitaja changamoto nyingine kuwa uelewa mdogo wa wazazi juu ya kozi ya “Hotel Management,” kuwa ni kozi ya kihuni kiasi cha kuleta wanafunzi kiduchu, ili hali si kweli ni kozi nzuri na ina uwanja mpana wa ajira na uhuni ni tabia ya mtu binafsi.

Aliongeza changamoto nyingine ni hali ya kipato cha wazazi na walezi  na jamii kwa ujumla kwani imekuwa moja ya changamoto ya chuo kushindwa kufikia malengo yake hasa kutokana na ulipaji mgumu wa ada kwa
wanafunzi,kwani “Wakazi wa mkoa wa Tabora wengi wao ni wakulima kwa asilimia kubwa hivyo wengi husubiri kipindi cha msimu kimalipo ama mvua inaponyesha vyema.”alisema.

Alisema hali hiyo hupelekea chuo kutofikia malengo yake ya kujiendesha  hasa ukizingatia chuo hakina ufadhili wowote zaidi ya kujiendesha chenyewe.

Alisema chuo pia kinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vifaa na  hasa vinapopatikana huwa ni vya bei ya juu,huku  vifaa vya kozi za utalii navyo huwa ni tatizo kubwa kupatikana.

Mkurugenzi huyo alitoa wito na ushauri kwa jamii kuendelea kukiamini  chuo cha Musoma Utalii,kwani toka kimeanzishwa kimeweza kutoa wahitimu bora kwa asilimia 90 wamefanikiwa kujiajiri na kuajiriwa kote nchini.

“Tunaomba wazazi na jamii kwa ujumla kuendelea kuleta wanafunzi ili  waweze kupata elimu bora yenye kutambulika kitaifa na kimataifa.” Aliongeza.

Aidha aliomba pia wazazi kuendelea kuchangia fedha za kwenda mafunzo  ya vitendo ,(Study Tour), kwani chuo kina ratiba ya kutembelea Mbuga za wanyama mara tatu (3) kila mwaka ikiwa ni sehemu mojawapo ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watanzania kwa ujumla.

Alisema ana imani endapo chuo kitakamilika ujenzi wa majengo ya yake ana imani mkoa wa Tabora ambao ni mkoa wenye historia ya kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni utapiga hatua ya kimaendeleo na kutoa ajira zaidi.

Mrutu anaongeza kuwa ni dhahiri mkoa wa Tabora una fursa nyingi sana  lakini bado hakuna jitihada za makusudi na hasa elimu kwa vijina wetu kusoma ili kukabiliana na ushindani wa shirikisho la afrika mashariki kwa sasa.

Hata hivyo mkurugenzi huyo amesifu kasi mkuu wa mkoa wa Tabora,Fatma  Mwassa katika usimaizi na kutoa vipaumbele ya elimu mkoani hapa kwani dalili za mbadiliko ya elimu zimeanza kutoa picha ya mafanikio mazuri tuendako.

Mrutu anaongeza kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora,Fatma Mwassa amekuwa  mstari wa mbele zaidi katika kusukuma gurudumu la elimu kwa kuweka mikakati madhubuti ya watoto hasa wa masikini waweze pata elimu itakayosaidia kuondokana na umasikini.

Mkurugenzi huyo anasema kwa sasa chuo cha Musoma Utalii ni kimbilio la  wanyonge kwani kimaonekana ni mkombozi zaidi.

No comments:

Post a Comment