Na Beatrice Masaki - Tabora
Jeshi la polisi mkoani Tabora limepokea pikipiki 13 kutoka kwa Inspekta Jenerali Said Mwema zitakazosaidia harakati za
kukabiliana na vitendo vya uhalifu
katika mkoa huo.
Akikabidhi pikipiki hizo kamanda wa polisi mkoa wa Tabora,
ACP Anthon Rutha amesema kuwa,pikipiki hizo zitagawiwa kwa wakaguzi wa kila
tarafa wa wilaya za Igunga ,Uyui,Urambo ,Sikonge,Nzega na Tabora mjini kwa lengo la kusaidia ulinzi na usalama wa wananchi.
Kamanda huyo wa
polisi wa mkoa wa Tabora ametoa wito kwa
wakaguzi wa kila tarafa kuzitumia pikipiki hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na si kuzitumia kwa
matumizi binafsi na kuwataka wazitunze
vizuri kwani kwa kufanya hivyo , kunaweza kusaidia kudhibit uhalifu kwa
wakati na kuimarsha amani mkoani hapa.
Akipokea pikipiki hizo kwa niaba ya wakaguzi wa tarafa mkoani hapa mkaguzi wa
polisi Joseph Matui wa tarafa ya Tabora kaskazini amesema kuwa, pikipiki hizo
zitawasaidia kufika maeneo ambayo wananchi wanahitaji kujua mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na juu ya ulinzi na usalama wa mali zao.
Matui amewataka wananchi kuonesha ushirikiano kwa
askari jeshi la polisi pindi wanapofika katika maeneo yao na pika wawe tayari kuwafichua wahalifu.
No comments:
Post a Comment