Monday, December 10, 2012

VIONGOZI WA SADC WATUA DAR KUHUDHURIA KIKAO CHA DHARURA


Rais Yoweri Museveni wa Uganda (kulia) akisalimiana na  Makamu wa Rais wa Tanzania Dr. Gharib Bilal  (kushoto)  alipowasili jana katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa dharura  wa Jumuiya  ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) 
 Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Msumbiji Mhe. Armando Guebuza  akipokewa na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataia Mhe. Bernard Membe
 Rais Joseph Kabila wa DRC akipokewa na Waziri wa Uvuvi Dr, David Mathayo.

 Makamu wa Rais wa Zambia Dr. Guy Scott  akifurahia jambo na Waziri wa  Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe aliyempokea
 Balozi wetu nchini Msumbiji Shamim Nyanduga (kulia) akiongea na baadhi ya maafisa wa SADC
 Kikundi cha matarumbeta cha Mount Usambara kinachoongozwa na Mzee Hoza kikitumbuiza uwanjani

 Bendera za nchi zinazojumuisha nchi za SADC zikipepea. Picha zote na Manakombo Jumaa-MAELEZO

Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika, SADC, wameanza mkutano wao wa dharura jijini Dar es salaam nchini Tanzania.  Kikao cha Asasi ya Ulinzi, Siasa na Usalama ya SADC inayojulikana kama TROIKA kilianza jana Ikulu jijini Dar es salaaam chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete.

 Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe amesema  kikao hicho cha TROIKA kimewakutanisha marais Jakaya Kikwete, Hifikepunye Phohamba wa Namibia na Jacob Zuma wa Afrika Kusini. 

Amesema mara baada ya kikao hicho cha TROIKA viongozi hao watajumuika na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye pia ni mwenyekiti wa mkutano wa kimataifa wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, pamoja na Rais Armando Guebuza wa Msumbiji ambaye ni Mwenyekiti wa sasa SADC. 


Viongozi hao kwa pamoja watajadiliana kwa kina matatizo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Madagascar na Zimbabwe ambapo watawasilisha mapendekezo yao katika mkutano mkuu wa viongozi wote 14 wa SADC utakaofanyika leo jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment