WAZIRI WA Ushirikiano
wa Africa mashariki na mbunge wa jimbo la Urambo mkoani Tabora (CCM) Samwel Sitta amewataka wana-CCM kuheshimu
maamuzi yaliyotolewa na mahamaka kuu kanda ya Tabora ya kutengua ubunge jimbo
la Igunga.
Sitta alisema kwamba
mahakama imefanya kazi yake kwa kutoa uamuzi huo kwani hiyo ndio ilikuwa uamuzi
ila alitaka chama cha mapinduzi kujipanga upya kama
itakata Rufaa ama laa
Aliyasema hayo jana mjini
Tabora wakati akikabidhi vifaambalimbali ikiwemo Kompyuta mbili na printa zake kwa Vijana
wakatoliki (VIWAWA) vyenye thamani ya shilingi milioni mbili na nusu ambazo
aliwataka kuzitumia kwa makini na uadilifu mkubwa ili viweze kudumu.
Akizungumza mara baada ya
kukabidhi vifaa hivyo alisema, kwa kuwa Mahakama inamamlaka yake kisheria wana
CCM hawana budi kuyaheshimu maamuzi hayo kwani mahakama imefanya kazi yake
inavyotakikana.
“Kama kunamtu anaona
hukumu hiyo haikutenda haki anaweza kwenda mahakamani kukata rufaa, lakini mimi
nashauri nivyema tujipange upya tuingie ulingoni” alisema Sitta.
“Hapa mimi sina maoni juu
ya jambo hilo bali chamsingi ni vyema tukakaa kutafakali yaliyotokea huko
Igunga, ili basi tukiona inafaa kukata rufaa sawa, nakama tuingie ulingoni yote
ni sawa” alisisitiza Bw. Sitta.
Kuhusu ufisadi ,Sitta
ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alisema yeye kama
kiongozi wa serikali ni vema akafuata maadili ili hata anaahidi kutoa mchango
wake kwa watu hawezi kutoa kwa harakaharaka, kwani maadili yanaweza kumbana.
“Unajua sisi viongozi wa
Serikali pesa zetu ni lazima uzitoe polepole ukifanya haraka utaitwa
fisadi”alisema waziri Sitta.
Kwa upande wake mkuu wa
itifaki wa VIWAWA jimbo kuu la kanisa katoliki ,John Pinini alisema kwamba Ni
kiongozi wa kuigwa, na kuwaomba viongozi wengine wa serikalini kuwa na moyo kama huo kwa kumtolea Mungu.
Sitta ametoa kauli hiyo
siku mbili baada ya Mahakama Kuu ya
kanda ya Tabora kutengua ushindi wa mbunge wa jimbo la Igunga Dkt,Peter
Dalali Kafumu, kufuatia mahakama hiyo kukubaliana na hoja za upande wa
mlalamikaji dhidi ya CCM Joseph Kashindye kwamba uchaguzi huo uligubikwa na
vitendo vya rushwa.
Ilielezwa kwamba Katika
moja ya mikutano ya kampeni ya uchaguzi huo mdogo wa jimbo la Igunga
uliofanyika mwaka jana, Rage alipita mitaani huku akiwatangazia wananchi kuwa
mgombea ubunge wa Chadema amejitoa hivyo wasijisumbue kumpigia kura na badala
yake wamchague mgombea wa CCM.
Mwisho
No comments:
Post a Comment