Tuesday, December 18, 2012

MKUU WA MKOA WA MWANZA ENG EVARISTNDIKILO ANENA KWENYE AMANI NA UTULIVU KUNA MAENDELEO

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo alipokuwa akifungua Mkutano wa RCC tarehe 14 Dec. 2012 Kwenye Ukumbiwa Chuo cha Benki Mwanza
Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Bibi Isabela Marick akisoma Muhtasari wa kikao kilichopita cha RCC.
Mada kutoka Mamlaka ya Usuluhishi na Upatanishi kuhusu masuala ya kazi nayo iliwasilishwa.
Mhe. Mbunge Ndassa wa Jimbo la Sumve akichangia moja ya mada kwenye Mkutano wa kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mwanza.
 Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa RCC wakiwa wamesimama, kukumbuka kifo cha aliye kuwa Kamanda wa Polisi wa MKoa wa Mwanza kabala
--
Na: Atleya Kuni- Mwanza.
Kikao cha kamati cha Ushauri cha Mkoa wa Mwanza (RCC),  mwishoni mwa juma hili wamekutana katika Ukumbiwa Chuo cha Benki jiji Mwanza nakujadili mambo kadha wa kadha yahusuyo maendeleo ya Mkoa Mwanza, Akifungua kikao hicho Mkuu wa Mokoa wa Mwanza Eng. Evaristi Ndikilo, Alisema lengo la kikao hicho ilikuwa kutahmini ni kwa jinsi gani wameweza kutekeleza yale yote walio azimia katika kikao  kilichopita cha tarehe 03 June 2012.

 Sambamba na kuangalia mambo mengine Mkuu wa Mkoa hakuacha kuendelea kuhubiri suala la Amani, alisema mtu anapo fikiria kuanzisha vurugu ajiulize anaanzisha vurugu kwa manufaa ya nani kwani tunapokuwa na vurugu hata shughuli za maendeleo haziwezi kufanyika kwa ufasaha.

Alihimiza juu ya kila halmashauri kuongeza vyumba vya Maabara kwa kila shule ilikufanya wanafunzi kupenda masoma ya sayansi, alisema kila Shule ihakikishe inajenga maabara tatu za sayansi yaani Baiolojia, Fizikia na Chemistry.

Kwa upande mwingine Mkuu huyo wa Mkoa alihimiza Ufugaji nyuki, Alisema suala la ufugaji nyuki halihitaji Mtaji Mkubwa kama wengine wanvyo fikiria, bali unapokuwa na Msitu tu basi nyuki wenyewe watakuja kuwekeza hapo, anachopaswa kufanya nikuandaa mizinga yako basi nyuki watakuja kuingia lakini pia tutakapofuga nyuki itasaidia katika utunzaji wa Mazingira.

Kufuatia tishio la njaa kwa baadhi ya Wilaya za MKoa huo Mkuu huyo wa Mkoa aliwahimiza wakulima na Viongozi wa Halmashauri kuhakikisha wanawahiza wakulima kutilia mkazo katika kilimo cha Mtama, kwani kitasidia sana katika kuepukana na njaa.

Wakichangia katika kikao hicho baadhi ya wajumbe wa Kikao hicho walipendekeza, Maghala ya Chakula yaliopo Wilayani Kwimba, yatumiwe na Serikali katika kuhakikisha yanakuwa ni sehemu mojawapo yakuhifadhia chakula cha Njaa, na kuacha kutegemea Bohari ya Shinyanga pekee kwani Imekuwa na usumbufu sana pindi njaa inapotokea.

Katika kikao hicho mada mbalimbali ziliwasilishwa, mada hizo ni pamoja na Hali ya kilimo na muelekeo wa Msimu wa ulimaji na upandaji, ambapo mtoa Mada katika mada hiyo, katibu Tawala Msaidizi wa Uchumi Bw. Ndaro Kulwijira alisema kwa Mkoa wa Mwanza Msimu wa Kilimo huanza Mwezi wa Nane hivyo ni vema wakulima wakalijua hilo na wakaanza maandalizi ya mapema katika kilimo.

Kwa uapande wake Afisa Mipango wa Sekretariti wa Mkoa wa Mwanza Matia Levi, mabye alitoa mada juu ya zozi la Sensa, alisema kwaujumla zozi hilo katika MKoa wa Mwanza lilienda vizuri, nakwamba Wananchiwasubiri kusikia Matokeo yatakayo tolewa na Rais wa Jamuhuri mwishoni mwa Mwezi Desemba.
 
Akifunga mkutano huo, Mkuu wa MKoa wa Mwanza ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Kikao hicho, alionya baadhi ya wajumbe wanao kimbia kuhudhuria kikao hicho na akasema kwamba kama kuna mtu anashindwa kuhudhuria vikao halali namna hii, basi kuna kila haja yakuangalia kwa upya nakutahmini sheria zinataka nini, Ndugu zangu haiwezekani mtu tu kwa sababu zake aache kuhdhuria Vikao hivi vya Kisheria tena bila hata ya taarifa halafu kesho na kesho kutwa aje atusumbe kwamba haelewi kilicho jadiliwa.

Akashauri pengine kanuni zipitiwe na Sheria ziangaliwe kwa upya ili kama ni hatua za kinidhamu dhidi ya mtu huyo ziweze kuchukuliwa RCC ndicho kikao kikubwa kabisa cha maamuzi katika ngazi ya mkoa na kipo kwamujibu wa sheria namba 19 ya mwaka 1997 juu ya uanzishaji wa Sekretarieti za Mikoa na kuhuishwa na tangazo la Novemba 2011 lililo sainiwa na Mhe. Rais.

No comments:

Post a Comment