Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokelewa na viongozi wa Kanisa la
Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha kwa ajili
ya kuongoza harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ukarabati wa kanisa
hilo,iliyofanyika leo Mkoani humo.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (wa tatu
kushoto) akiongozana na Askofu wa Kanisha hilo la Lutherani usharika wa
Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha,Askofu Akyoo.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akihutubia muda mfupi kabla ya kuanza kwa harambee ya kuchangia ujenzi
wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani
Arusha.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea
ahadi ya mchango kutoka kwa mmoja wa wamini wakati wa harambee ya
kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya
Meru Mkoani Arusha.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiondoka
kanisani hapo baada ya kumalizika kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa
Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
=========== ========= =========
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa amesisitizia tena kuwa tatizo la
ajira kwa vijana ni jambo la hatari kwa usalama wa nchi,wakati alipokuwa
katika harambee ya kuchangia ukarabati wa kanisa la kilutheri usharika
wa Akyeri Meru mkoani Arusha, Mh lowassa ameonya kuwa suala hilo
lisiposhughulikiwa haraka litasababisha hali ya hatari.
''tunashuhudia maandamano katika
mataifa ya ulaya vijana wakidai hali bora ya maisha pamoja na ajira.hali
hiyo tusipoangalia inaweza kutokea hapa nchini kwetu.
huko nyuma niliwahi kusema kuwa
makanisa, mashirika na watu binafsi wasaidie juhudi za serikali kutatua
suala hilo''alisema Lowassa.
Lowassa ambaye katika harambee
hiyo aliongozana na marafiki zake, ambapo yeye na familia yake pamoja na
marafiki zake wamechangia kiasi cha shilingi millioni 33.2.
Zaidi ya shilingi millioni 160 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana katika harambee hiyo.
Kwa upande wake askofu Akyoo wa
jimbo la Meru alimsifu Lowassa kwa uchapakazi wake popote
alipokuwa.''Wakati ulipokuwa Waziri Mkuu ukimsaidia rais tulishuhudia
uwezo wako mkubwa katika kufuatilia majukumu yako''alisema na kuongeza
kuwa Lowassa ni mtu wa ibada
No comments:
Post a Comment