Na Lucas Raphael.Nzega.
ZAIDI ya Wanafunzi 1500 wa
shule ya msingi Nyasa mbili iliyopo
wilayan i Nzega Mkoani Tabora wanakabiliwa na uhaba wa
matundu ya vyoo.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jana mwalimu mkuu wa shule hiyo George
Alphonce alisema kuwa shule hiyo ina wanafunzi
1520 huku ikiwa na matundu ishirini ya
vyoo ambayo haya tosherezi kwa matumizi ya
wanafunzi hao.
Alisema kuwa kwa idadi
hiyo shule inaupungufu wa matundu 40 ambapo
kwa sasa wanafunzi hao hutumia tundu
mmoja wanafunzi 76 nje ya utaratibu
wa kawaidi ,utaratibu wa kawaida inapaswa tundu
mmoja wanafunzi 20.
Alisema kuwa tatizo hilo ni
la muda mrefu kutokana na kuongezeka
kwa wanafunzi kila mwaka tofauti na
wale wanao hitimu elimu ya msingi ya Darasa la
saba.
George alisema kuwa wanafunzi kwa kipoindi
hiki wanap[ata shida kujisaidia katika matundu hayo hali ambayo wanajikuta
wakiwa katika wakati mgumu na kusababisha mazingira ya kusoma kuonekana kuwa
magumu kutokana na uhaba huo wa matundu.
Alisem,a Jitihada inayofanika kwa kushilikiana na
kamati ya shule pamoja na wazazi wapo katika harakati za kukamilisha matundu ya
vyoo nane ambayo yatasaidia kupunguza msongamano huo.
Alisema wazazi na walezi wamejitokeza kupambana na
tatizo hilo ili kuhakikisha wanafunzio hao wana soma katika mazingira mazuri.
George aliomba serikali kuingilia kati suala hilo
kuhakikisha wananfunzi wana soma katika mazingira stahiki ili kuwawezesha
kufanya mazuri katika mitihani yao ikiwa na kukarabati miundombinu mbalimbali
ya masomo katika shule za msingi.
Aliongeza kuwa wazazi wajitokeze kwa wangi
kusaidia serikali katika kuboresha mazingira ya kusoma watoto wao ikiwa na
kuchangia michango m,b alimbali ya shule.
Mkuu wa wilaya ya Nzega ,Bituni Msangi alisema
kuwa jitihada zinaendelea kuwa hamasisha wazazi na walezi katika kuchangia
maendeleo na kutatua matatizo ya wanafunzi ambayo yapo katika uwezo weao ikiwa
na kuboresha mazoingira ya masomo pamoja na vyoo.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa taarifa hiyo itafuatiliwa kwa
Ofisa Elimu wilaya ili suala hilo liweze kufuatiliwa kwa ukaribu ikiwa na
kukagua mazingira mbalimbali ya shule hizo pamoja na vyoo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment