Thursday, January 17, 2013

WENGINE WAENDE KUJIFUNZA MBOLA .DKT MGIMWA

Na Lucas Raphael,Uyui

Serikali imesema kuwa inaangalia uwezekano wa kusambaza teknolojia na mbinu zilizotumika katika kijiji cha millennia cha Mbola mkoani Tabora, zitumike katika vijiji vyote hapa nchini, ili kuweza  kuutokomeza umasikini kwa haraka na kutimiza malengo 8 ya milenia.

Waziri Fedha Dk. William Mgimwa, aliyasema hayo katika kijiji cha Ilolangulu, wilaya ya Uyui mkoani Tabora, alipokuwa akizungumza na wakazi wa kijiji  16 vya millennia mbola , ambapo aliwapongeza kwa kazi nzuri na jinsi walivyoupokea mradi huo, ambao leo umekuwa wa mfano.
Alisema kwamba ni vema wananchi wakahakikisha miradi yote iliyotekelezwa chini ya mradi wa vijiji vya millennia mbola inatunzwa vizuri ili iwe daraja la kufundishia vijiji vingine nchini katika utekelezaji wa malengo 8 ya milenia .

Waziri Mgimwa, aliyefika kijiji hapo kwa ajili ya kujifunza na kujionea jinsi mradi huo shirikishi wa kijiji cha Milenia unavyooendeshwa na Umoja wa mataifa ulivyoweza kupambana na umasikini kwa wakazi wa vijiji 16 vya wilaya ya Uyui.

Awali Mratibu wa mradi wa kijiji cha Milenia cha Mbola mkoani Tabora, Dk Gerson Nyadzi, alisema kuwa wakazi wa kijiji hicho wameweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo baada ya kuwezeshwa na serikali na mradi wa kijiji hicho kwa kupewa pembejeo ili kuweza kuondokana na umasikini uliokithiri iliyowawezesha wakulima kulima na kuvuna zaid ya maguni 20 hadi 40 kwa heka moja ya mahindi .

Mapema Mwenyekiti wa kijiji cha Ilolangulu Ali Magoha, alisema kuwa mradi wa kijiji cha millennia unaojumlisha vijiji 16 umefanikiwa kwa kutimiza malengo yote 8 yaliyokusudiwa kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 85.
Alitaja manufaa ambayo wameweza kupatikana toka mradi wa vijiji vya milenia mbalo ulipoanza ni pamoja na  ujenzi wa nyumba za kisasa za matofari ya kuchoma na bati ,uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka .

Pia alisema kwamba mradi huo umesaidia kupunguza tatizo la vifo vya watoto chini ya miaka 5 na vifo vya akina  mama wajawazito.
Alisema hapa awali vifo hivyo vilikuwa wastani wa watoto 3 nadi 5katika kipindi cha miezi mitatu na kinamama 5 kwa kila mwezi lakini kwa sasa wastani huo ni kwa kipindi cha miezi 6 na wakati mwingine hakuna kabisa.
Magoha alisema kwamba hatua hiyo imefikiwa baada ya wananchi kupata elimu juu ya kutumia vyandarua na kuua mazalia ya mbuhivyo kupunguza kasi ya maradhi yan malaria katika eneo hilo..
Mwenyekiti huyo wa serikali ya vijiji vya mrai wa vijiji vya milenia mbola akizungumzia swala la elimu alisema kwamba kwa sasa kiwango cha wanafunzi wanaoacha masomo imepungua tangu mradi huo umeanza na kuwa sasa wanafunzi wengi wanamaliza masomo ua darasa la saba .
Alitaja mbinu hizo ni pamoja na kutoa chakula kwa wanafunzi na kuhamasisha michezo mashuleni hivyo wakuwavutia watoto wengi kujiunga na shule .
Kuhusu suala la maji alisema kwamba wanaendelea vizuri ambapo wastani wa asilimia 60 ya wakazi wa eneo hilo wanapata maji safi na salama tofauti na ilivyokuwa awali .
Mwisho


Naye Mbunge wa jimbo la Tabora kaskazini Shaffin Sumar, aliishukuru serikali kwa kuendelea kuchochea maendeleo katika vijiji vyote 16 vya millennia kwa kuanza mchakato wa kupeleka umeme katika vijiji hivyo  vyote ili kusaidia kukua kwa maendeleo ya haraka.
 
Mwisho.
 

No comments:

Post a Comment