Monday, December 31, 2012

TUZO HII NI KWA WADAU WOTE WA FULLSHANGWEBLOG NA KUKARIBISHA MWAKA MPYA 2013


Mkurugenzi wa Fullshangweblog.com Bw. John Bukuku kushoto akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki katika maonyesho ya World Travel Market (WTM)Nchini Uingereza mwezi Oktoba mwaka huu katikati ni Meneja Masoko wa Bodi ya Utaii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena.
.........................................................

Mwaka huu Fullshangwe imefanikiwa kupata Tuzo ya kutangaza utalii wa ndani wa Tanzania kimataifa mwaka 2011 nchini Uingereza inayoitwa TANZANIA TOURISM BOARD WEB TRAVEL MAGAZINE AWARD 2011, Fullshangweblog.com kupitia kwa mkurugenzi wake Bw. John Bukuku ilipokea tuzo hiyo katika maonesho ya utalii ya kimataifa ya dunia World Travel Market (WTM) yaliyofanyikaneo katika eneo la Exel jijini London nchini Uingereza kuanzaia Oktoba 5 mpaka 8 2012, ambapo Fullshangweblog.com ilikuwa moja ya makampuni yaliyoshiriki katika maonyesho hayo katika kupasha habari.

FULLSHANGWEBLOG.COM inaushukuru uongozi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) inayoongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji Dk Aloyce Nzuki, Mkurugenzi wa Masoko Devotha Mdachi , Meneja Masoko Bw. Geofrey Meena na wafanyakazi wote wa bodi hiyo, pamoja na wadau wake wote kwa kutambua mchango wa FULLSHANGWE.BLOG kama web magazine iliofanya kazi nzuri ya kutangaza utalii wa ndani mwaka 2011 na kuitukukia tuzo hiyo, ninawashukuru sana kwani maana ya tuzo hii ni kwamba tunamaliza mwaka 2012 kwa mafanikio.

Kuna baadhi yamambo niliyokumbana nayo katika kazi zangu za kila siku ” Kuna matukio mengi niliwahi kukutana nayo katika shughuli zangu za kutafuta habari mengine yalikuwa ni ya kukatisha tamaa sana, lakini sikukata tamaa niliendelea kukaza buti kadiri mungu alivyonijalia, Lakini mengine yalikuwa ni ya mafanikio yenye kutia moyo.

Katika kazi hii nimekumbana na mambo mengi “Kuna wakati marafiki zangu wa karibu walinikatisha tamaa na kuniuliza kwamba ninafanya nini mbona sieleweki hasa wakati nilipojitambulisha katika mikutano mbalimbali kwamba nawakilisha WWW.FULLSHANGWEBLOG.COM wengi hawakunielewa hata kidogo nini ninachokifanya, hata hivyo niliendelea na juhudi zangu mpaka walipoanza kutambua na kuelewa kwamba nilikuwa nafanya nini”

Siku moja nilisafiri kuelekea nyanda za juu kusini mkoani Iringa nilifika katika wilaya Mufindi Mafinga nilikutana na kisa ambacho pia nilikiripoti kwenye mtandao, kisa hiki kilikuwa hivi.

MAPANDA HOTEL WANASEMA LAPTOP COMPUTER INAKULA UMEME KULIKO PASI NA FRIJI!

Nimeingia katika hoteli hii ya Mapanda Hotel and Guest House mjini Mafinga ili niweze kupata kifungua kinywa lakini pia niweze kufanya kazi zangu kwenye kompyuta yangu ya mkononi, lakini sikupata kifungua kinywa wala kufanya kazi yoyote, Kilichonipoza ni kutumia Kompyuta yangu (Laptop) Meneja wa Hoteli hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alinifuata na kuniambia kwamba siwezi kuendelea kutumia kompyuta yangu kwa kuwa inakula sana umeme ni sawa tu na friji au pasi ya umeme, hivyo ningeweza kumaliza umeme wao wa LUKU, nikajaribu kubembeleza lakini meneja huyo alinikatalia kabisa..

Binafsi sikujali sana wala sikukubaliana na hoja yake manake nilijua kwamba umande na umbumbumbu umewajaa kwenye ubongo wao katika teknolojia ya Kompyuta hivyo kwao wao Kompyuta ya mkononi au Laptop ni sawa usiku wa giza, Ikabidi niondoke hapo lakini bahati nzuri nikapata Internet Cafe inayoitwa 3A Traders Internet Cafe hapo nikafanya kazi yangu vizuri kabisa

Nawatahadharisha ndugu zangu mnataka kuja na kompyuta zenu hapa Mafinga msijisumbue kwenda hapo Mapanda Hotel kwani yanaweza kuwapata yalionipata mimi.

MATUKIO YA KUKUMBUKWA
Kati ya matukio ambayo ni ya kumbukumbu kubwa ni tukio la kuzama kwa September 10, 2011 ambalo mtandao wa Fullshangweblog.com uliripoti kwa ufupi na kuvuta hisia za watembeleaji wengi MELI ya Spice Islander imezama usiku wa kuamkia leo ikiwa safarini kuelekea Pemba ikitokea bandari ya Malindi Unguja.

Meli hiyo inasemekana ilikuwa na abiria wapatao 610 ambapo juhudi za kuokoa majeruhi wa ajali hiyo bado zinaendelea hivi sasa.

Akizungumzia ajali hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Ussi amesema tukio hilo limetokea saa 8:30 za usiku.

Haji Ussi amesema meli hiyo iliondoka katika Bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima, lakini katikati ya safari ikapata hitilafu na kusababisha kubinuka na hatimaye kuzama kabisa.

Lakini pia tukio linguine lililovuta hisia za watembeleaji wengi lilikuwa ni kifo cha Mwigizaji Maarufu nchini Marehemu Steven Kanumba watu wengi walikuwa wakitembelea mtandao ili kupata taarifa mbalimbali juu ya msiba huo.

NINAJISIKIA VIZURI KUWA BLOGGER

Nimekuwa nikifurahia kazi yangu na kuipenda sana kwani katika kazi yangu hii ya kupasha habari imenikutanisha na watu wengi maarufu, wasio maarufu lakini ni muhimu katika jamii na wakati mwingine ninaposafiri katika mikoa mbalimbali na vijiji na nje ya nchi, kitu kikubwa kinachonifurahisha ni matukio halisi ninayokutana nayo, kwani nakutana na habari mabazo zinagusa hisia za wasomaji na watembeleaji wa mtandao na pia zinanifanya kujifunza mambo mengi yanayotokea duniani pia napata habari zaenye uhalisia wa maisha ya mtanzania na matukio yenye kuvuta hisia kwa wasomaji wetu, jambo ambalo linanifanya nijisikie vyema zaidi ninapopata nafasi ya kupiga picha na kuandika habari za kijamii kutoka vijijini katika mikoa mbalimbali na mataifa mbalimbali hii ni kutokana na mvuto wa picha na habari zenyewe lakini pia ninapata changamoto za kimawazo na jinsi ya kujikwamua katika maisha ya kila siku.

SHUKURANI KWA WADAU
Mwisho ninawashukuru wadau wote waliofanikisha hapa kwa njia yoyote ile mafanikio ya mtandao wa FULLSHANGWEBLOG.COMsi kwa juhudi zangu binafsi juhudi binafsi, bali pia ni juhudi za wadau wote ambao tulishirikiana nao na tunaendelea kushirikiana nao kwa moyo wa dhati, ni matumaini yangu kwamba tutaendelea kushirikiana kwa karibu ili tuweze kuendeleza juhudi za kujenga nchini yetu nzuri ya Tanzania na kupasha habari zaidi kadiri tutakavyojaliwa na Mwenyezi Mungu katika mwaka ujao wa 2013

Lakini naomba nitaje baadhi ya taaisisi, mashirika na wadau kadhaa waliotusaidia na wanaendelea kutusaidia kwa kututumia habari na matukio mbalimbali, ninatoa shukurani kwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Idara ya Habari Maelezo, Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Kitengo cha habari Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Habari Ofisi ya Makamu wa Rais, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Kitengo cha habari Ofisi ya Bunge, Vitengo vya habari Katika Wizara mbalimbali, Mashirika, Makampuni binafsi, Idara za serikali na wadau mmoja mmoja waliotusaidia kupata habari mbalimbali muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.

Nitakuwa siyo mwingi wa fadhila kama sitawashukuru kaka zangu Muhidin Issa Michuzi na Maggid Mjengwa, kaka zangu walionitangulia kwa umri na kazi ya kublogu ninawashukuru kwa ushauri wo ninaoweza kuuita maalumu pia kwa msaada wao katika kunielekeza mambo mengi juu ya uelewa wa kublogu, ambao nimekuwa nikipewa wakati wote, nashukuru sana kaka zangu naomba tuendelee na moyo huohuo na mungu atatutangulia katika yote, Lakini pia niwashukuru mablogger wenzagu Michuzijunior wa Jiachieblog au Ahmed Michuzi kama anavyojulikana, Mroki Mroki, Zainul Nzige, Carthbert Kajuna, Othman Michuzi, Abdalla Mrisho, Josephat Lukaza na Mwanamke blogger mkongwe Mamaa Shamimu Mwasha wote ninawapenda sana

Mwisho napenda kumshukuru dada yangu, mwandishi wetu na mpiganaji Gladness Mushi wa FULLSHANGWEBLOG.COM mkoani Arusha, ninakushukuru dada yangu kwa kuipigania FULLSHANGWEBLOG na kuitambulisha kwa nguvu mkoani Arusha kutokana na habari nyingi za kijamii ambazo umekuwa ukizituma kutoka huko, tuko pamoja na FULLSHANGWE inakuangalia kwa macho mawili Mungu akubariki sana na uwe na afya njema ili tuendeleze kazi

No comments:

Post a Comment