Monday, December 31, 2012

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe:“Kama Mwenyezi Mungu atampa uhai na afya njema hadi mwaka 2015, Dk Slaa anatosha na Chadema, tutampa fursa nyingine ya kupeperusha bendera ya chama kwenye nafasi ya urais ninataka wanaotumia ugombea Urais kama kete ya kuleta mtafaruku ndani ya Chadema watambue hivyo.”

 Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe Akiunguruma Karatu
 Mbunge wa Arumeru Mashariki-CHADEMA,Joshua Nasari akiunguruma Karatu jana mbele ya Umati Mkubwa
Sehemu ya Umati mkubwa wa Wana Chadema Karatu wakiwa kwenye mkutano wa hadhara jana
--
CHAMA  cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema),kimetangaza kuwa Katibu Mkuu wake, Dk Willbrod Slaa atapewa fursa ya kuwania nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, mwaka 2015.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza hatua hiyo jana,alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mpira,mjini Karatu mkoani Arusha, huku yeye akijiweka kando kuwania nafasi hiyo.

Hata hivyo,Dk Slaa mwenyewe alipoulizwa iwapo ana nia ya kugombea urais mwaka 2015, alisema: “Kwani mwaka 2010 nilijitangaza mwenyewe?,Iwapo wanachama wa Chadema watanipendekeza, nitafikiria kufanya hivyo.”Kwa Habari zaidi

No comments:

Post a Comment