Monday, December 24, 2012

ALEX MSAMA ATOA MSAADA KATIKA KITUO CHA YATIMA

Mkurugenzi wa Msama Promosheni, Alex Msama (kushoto) akikabidhi vitu mbalimbali kwa mwakilishi wa kituo cha watoto yatima cha Chamazi Group, Haruna Mtandika ikiwa ni sehemu ya mapato ya fedha zilizopatikana na tamasha la Pasaka, kwa ajili ya sherehe za sikukuu ya krisimasi na mwaka mpya. Katikati ni mratibu wa tamasha la Pasaka kutoka Baraza la Sanaa la Taifa,Malimi Mashiri 
Mkurugenzi wa Msama Promotions,  Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada kwa vituo vya yatima jijini Dar es Salaam
 Mratibu wa tamasha la Pasaka kutoka Baraza la Sanaa la Taifa, Malimi Mashiri akizungumza na waandishi wa habari  baada ya kushuhudia zoezi la kukabidhi vyakula mbalimbali kwa katika vituo vya kulelea watoto yatima.
  Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Msimbazi Center, Consolata Pius akipokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa  Mkurugenzi wa Msama Promosheni, Alex Msama (kulia) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe za sikukuu ya krismasi, vitu hivyo vimetokana na mapato yaliyotokana na tamasha la Pasaka.
 Alex Msama akiwa na watoto wanaolelea katika kituo cha Msimbazi Center
DAR ES SALAAM, Tanzania

 MKURUGENZI wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama ametoa msaada wa vyakula katika vituo viwili wenye thamani ya sh.milioni 2.8.

 Akizungumza katika hafla maalum ya ugawaji misaada hiyo, alisema ametoa misaada hiyo ni sehemu ya ahadi yake katika tamasha la pasaka. Alisema kuwa kwa sasa amekabidhi vyakula kama, mchele, maharage, unga wa ngano, unga wa sembe na mafuta.  Misaada hiyo imekabidhiwa kwa vituo vya msimbazi Center na Yatima Group ya Mbagala Chalambe. 

Msama alisema kwa sasa amekabidhi katika vituo hivyo ambavyo vipo Dar es Salaam na atafanya hivyo katika mikoa tofauti. Kwa upande wa mlezi wa kituo cha Yatima Group Haruna Mtandika, alimshukuru Msama kwa msada huo ambao umesaidia kituo chake. " 

Namshukuru sana Msama kwa kuweza kusaidia kituo chetu aswa katika kipindi hiki cha siku kuu"alisema Mtandika.  Kwa upande wa Afisa Sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Malima Mashili, alimpongeza Msama kwa kutimiza ahadi zake kwa walengwa.  Alisema Basata inawataka wengine waige anavyofanya Msama kwa kuweza kutimiza ahadi zake katika tamasha. 

Kwa upande wa kituo Mlezi wa kituo cha Msimbazi Center Imakulata Pius, alisema mshukuru sana Msama na kuwataka wengine waige mfano huo. "Naomba na wengine waige mfano huu wa kampuni hii kuandaa tamasha na kutoa kile walichoaidi katika matasha wanayofanya"alisema Pius.

No comments:

Post a Comment