Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo
cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Raymond Mbilinyi, (kushoto) akifurahia
jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji Huru Tanzania (EPZA)
Dkt. Adelhelm Meru muda mfupi mara baada ya kukutana na ujumbe wa
wawekezaji kutoka nchini china mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo
cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Raymond Mbilinyi, (kushoto) akifurahia
jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji Huru Tanzania (EPZA)
Dkt. Adelhelm Meru muda mfupi mara baada ya kukutana na ujumbe wa
wawekezaji kutoka nchini china mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Juhudi za serikali kutangaza
vivutio vyake vya uwekezaji zinazidi kuzaa matunda baada ya ujio wa
ujumbe wa watu sita wa kampuni ya Anhui Foreign Economic Construction ya
nchini China kuja nchini kujionea na kujua fursa mbalimbali wanazoweza
kuwekeza hapa nchini.
Akiongea na waandishi wa habari
kuhusiana na ujio huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC), Bw. Raymond Mbilinyi alisema ujumbe huo ni wa wawekezaji
wakubwa kutoka China wanaotaka kuwekeza hapa nchini kwa ushirikiano na
serikali ya Tanzania.
“Hii ni fursa nyingine ambayo nchi
inapata kupitia uwekezaji, hawa ni wawekezaji wakubwa ambao wamekuja
kwa lengo la kuangalia fursa mbalimbali hapa nchini,” alisema Bw.
Mbilinyi mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa ujumbe
huounaoongozwa na mwenyekiti wake wa bodi, Bw. Jiang Qingde umeshaonana
na Rais Jakaya Kikwete na kuzungumza naye mambo mbalimbali juu ya ujio
wao hapa nchini.
“Ni kampuni yenye uzoefu wa hali ya juu katika sula la uwekezaji,” alisema.
Akielezea zaidi alisema mpaka sasa
wamewekeza katika nchi zipatazo 20 katika bara la Afrika hivyo kuja
kwao hapa nchini ni ishara kuwa Tanzania pia ina mazingira mazuri ya
uwekezaji na kwamba jitihada za TIC kutangaza fursa za uwekezaji hapa
nchini zinazaa matunda.
Alisema kuwa wawekezaji hao wana uzoefu mkubwa katika sekta za madini, viwanja vya ndege, na nishati ya umeme.
Alisema kwa upande wa viwanja vya
ndege tayari kampuni hiyo imeweza kuwekeza katika katika nchi 15 katika
bara la Afrika, na kuongeza kuwa wana uzoefu wa kutosha katika suala la
uwekezaji katika maeneo mengi ya Afrika.
Alisema kuwa uzoefu walionao
wawekezaji hao utasaidia sana katika sula la kukuza uchumi wa nchi na
kuongeza ajira hapa nchini kwa kuwa uwekezaji wao ni wa maeneo mengi kwa
wakati mmoja hivyo ni fursa ya kipekee kwa nchi katika kutengeneza
ajira kupitia sekta ya uwekezaji toka nje.
“Kuna tatizo la ajira kwa vijana
wetu, hivyo kuwepo kwa fursa za uwekezaji hapa nchini ni jambo jema kwa
serikali yetu kuondokana na tatizo hili kwa kiasi kikubwa,” alisema Bw.
Mbilinyi na kuongeza kuwa TIC itaendelea na juhudi zake za kutangaza
vivutio vya uwekezaji Tanzania kwa wawekezaji wa ndani na nje.
Tanzania ina mahusiano mazuri ya kijamii na kiuchumi na watu na serikali ya China.
Kampuni mbalimbali toka nchi hiyo
ambayo inapiga hatua kubwa kiuchumi kwa kasi zimekua zikifanya kazi hapa
Tanzania kwa miaka kadhaa hasa katika sekta ya ujenzi wa vitu
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment