Msanii
wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikwa na wasanii wenzake mara
baada ya kuanguka jukwaani juzi ndani ya uwanja wa Sheikh Amri katika
tamasha la wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wale wa filamu.
Msanii
wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikiliwa na wenzake
wakimshusha chini ya jukwaa mara baada ya kuanguka alipopewa nafasi ya
kuwasalimia mashabiki wake
HALI
ya msanii wa filamu nchini,Juma Said Kilowoko maarufu kama Sajuki
imeelezwa si ya kuridhisha mara baada ya msanii huyo juzi kuanguka
jukwaani mara baada ya kuishiwa na nguvu wakati alipopewa kipaza sauti
kuwasalimia mashabiki waliofurika kumtizama.
Tukio
hilo lilitokea juzi jumapili katika tamasha la wasanii wa filamu na
wale wa muziki wa kizazi kipya lililofanyika ndani ya uwanja wa michezo
wa Sheikh Amri Abeid wakati msanii huyo alipopandishwa jukwaani
kuwasalimia mashabiki wake.
Mara
baada ya msanii huyo kupandishwa jukwaani alipewa kipaza sauti ili
aweze kuwasalimia mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida
alifanikiwa kutamka neno moja tu”ahhh" na kisha kudondoka chini ya
jukwaa lakini kabla ya kutua chini alidakwa na wasanii waliokuwa pembeni
yake.
Hatahivyo,wasanii
hao walimkalisha chini ya jukwaa hilo ili aweze kupumzika na kisha
baada ya muda mfupi walimshusha chini ya jukwaaa hilo ili aweze kupata
muda wa kupumzika zaidi.
Akihojiwa
na gazeti hili muda mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki kwa
sauti ya upole alisema kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana
nguvu na anahitaji matibabu zaidi.
”Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana sijisikii vizuri”alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi
Hatahivyo,baadhi
ya mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani hapo walionyeshwa kustushwa
na hali ya msanii huyo huku wengine wakiwatupia lawama nzito baadhi ya
wasanii wa filamu nchini walioambatana na msanii huyo kwa madai kwamba
wanamtumia ili wapate pesa ihali mwenzao ni mgonjwa.
Wakihojiwa
kwa nyakati tofauti mashabiki hao kwa jazba walisema kwamba msanii huyo
alipaswa kupewa muda mwingi wa kupumzika kuliko kuambatana na wenzake
mikoani kwani hali hiyo inamchosha zaidi.
“Hawa
watu wa Bongo movie ni watu wa ajabu sana huyu mtu anaumwa sana sisi
tunashangaa wanaambatana na mtu mgonjwa mikoani wampe muda apumzike na
si kumtumia kwa kupata pesa”alisikika shabiki mmoja akiongea kwa jazba
CHANZO: http://woindeshizza.blogspot.com
No comments:
Post a Comment