Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Michezo la Taifa
(BMT), Kanali mstaafu Idd Kipingu akimkabidhi nahodha wa timu ya Azam FC, Abdul
Mgaya kombe la Ubingwa wa michuano ya
Uhai Cup 2012 baada ya timu hiyo kuifunga Coastal Union ya Tanga kwa penalti
3-1 katika mchezo wa fainali ya vijana chini ya miaka 20 uliofanyika leo kwenye
Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Katikati ni Rais wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Leodgar Tenga.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah akimkabidhi zawadi ya
mfungaji bora wa mashindano ya vijana chini ya miaka 20 ya Uhai Cup, Ramadhani
Mkipalamoto wakati wa fainali ya michuano hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa
Karume jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe
lao.
Golikipa wa Azam FC, Aishi Salum akiokoa moja ya hatari
zilizoelekezwa langoni mwake.
Mshambuliaji
wa Coastal Union, Twaha Shekue akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Azam
FC, Samwel Mkomola.Picha Kwa Hisani ya Habari Mseto Blog
No comments:
Post a Comment