KUVUJA KWA MAJI YANAYODAIWA YA SUMU KUTOKA MGODI WA NORTH MARA KWA ZUA HOFU.
Na Anthony Mayunga-Mara
Na Anthony Mayunga-Mara
HOFU imewatanda wakazi wa vitongoji vya Kwinyunyi na Kegonga A,kijiji
cha Matongo wilayani Tarime kufutia maji yanayodaiwa kuwa ya sumu
kutoka bwawa la mgodi wa African Barrick North Mara kuvuja na kuingia
eneo la jamii.
Kuvuja kwa maji hayo kunadaiwa ni kutokana na kuwa ujenzi wa bwawa hilo ambalo kampuni hiyo inadaiwa kurithi kutoka kwa kampuni zingine zaidi ya 2 zilizotangulia kujengwa chini ya kiwango.
Baadhi ya wananchi wakiwemo wajumbe wa serikali ya kijiji hicho waliliambia Mwandishi wa habari hizi kuwa tatizo hilo limeishafikishwa Nemc na mamlaka zingine.
“Kilio chetu ni cha muda mrefu sana …lakini serikali imekuwa ikipiga chenga kukishughulikia hatujui ni kwa nini … 2009 watu ,mifugo na mazingira walipata madhara kutoka Mto Tighite mpaka leo ni chenga tu”alisema mjumbe wa serikali ya kijiji jina tunalo.
Alikwenda mbali sana na kudai kuwa mamlaka za serikali zimekuwa zikichangia jamii kudhurika na kujenga mahusiano mabaya kati yao na mwekezaji”matatizo ya maji ya sumu si ya leo lakini wanatupuuza matokeo wananchi wanaichukia kampuni”alisema.
Alibainisha kuwa desemba 20 ,2012 wataalam mbalimbali kutoka Mwanza na Dar es salaam wa Nemc na bonde la ziwa Victoria walishuhudia matatizo hayo na wananchi wakapaza sauti ,wakachukua vipimo lakini hawakuwahi kutoa majibu.
Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo jina limehifadhiwa asema kuwa bwawa hilo linavuja kwa sababu waliotangulia walilijenga bila kuweka
hata mipira mizito .
“Hili ni tatizo lazima liangaliwe kwa umakini maana linagusa maisha ya viumbe hai…maana kilichokuwa kinafanyika hapa ni kiini macho kwa kampuni kuleta mawe yanayopasuliwa kwa baruti na kumwaga hapa…hayawezi kudhibiti maji yanayovuja”alisema mfanyakazi huyo.
NEMC.
Mkurugenzi wa utekelezaji na uzingatia wa Nemc Dk,Robert Ntakamulenga alipouliza kwa njia ya simu amekiri kuwa tatizo hilo lipo na wanafuatilia.
“Kwa sasa siwezi kusema hatua gani zimechukuliwa na ofisi…lakini wiki ijayo kikosi kikubwa kitakwenda huko chini ya uenyekiti wa Ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira”alisema .
Alisema kikosi hicho kitashirikisha sekta ya madini,maji na uongozi wa wilaya ya Tarime kwa lengo la kuona tatizo na namna ya utatuzi wake”nadhani baada ya hapo ndipo tutakuwa na cha kusema”alisema.
Hata hivyo mmoja wa wataalam wa Mazingira kutoka Nemc jina limehifadhiwa alisema kuwa tatizo la mgodi huo litaendelea kusumbua na kuleta madhara kwa kuwa uanzishaji mradi haukuzingatia upanuzi baadae.
“Mgodi umeanza miaka mingi sana…haukuzingatia upanuzi wake na sasa unazidi kuongezeka bwawa la kuhifadhia majji ya sumu lilichimbwa wakati mradi ukiwa mdogo sasa inakuwa kazi kuhimili maji hayo…lazima yatavuja na yataendelea kuvuja,the big challenges” alisema.
Alisema kwa sasa kampuni hiyo inataka kuongeza eneo la bwawa kwa kuwa hilo limejaa na linavuja,lakini huo uzalishaji unaendelea,na kudai timu hiyo huenda ikapata ufumbuzi.
Kwa upande wa kampuni ya African Barrick Gold mine North Mara Saimoni Shayo ambaye anashughulikia mahusiano alipoulizwa hatua ambazo wamechukua kudhibiti hali hiyo ,alikwepa kulisemea kwa madai kuwa
wanaopaswa kulizungumzia ni Nemc na bonde la Ziwa Victoria. “Kimsingi hatupendi kulisemea sisi kwa kuwa tunafanya kazi kwa mjibu wa sheria za nchi na matatizo yameishazifikia mamlaka hizo, nadhani hao wakwambie, lakini ninachojua hakuna maji yanayotiririka”alisema.
Hata hivyo ziara ya wataalam wa Nemc na wengine desemba 20,2012 ilikuwa ni kukagua eneo ambalo mgodi ulilenga kupanua bwawa hilo kwa madai kuwa walishaongea na wananchi ambao walikana kukutana na kampuni hiyo.
Badala yake walikutana na tatizo la maji yanayotiririka na kuchukua vipimo ambavyo majibu yake hayajatolewa.
Mei 2009 maji yanayodaiwa kuwa ya sumu kutoka mgodi wa Gokona yalivuja na kuingia mto Tighite na kusababisha madhara makubwa kwa watu, wanyama, wadudu na mazingira.
Kamati tatu za bunge za Ardhi,Madini na afya chini ya Job Ndugai(kwasasa naibu Spika)zilitembelea eneo hilo na kutoa maagizo mbalimbali,hata hivyo wananchi hawajawahi kupewa ripoti nini kilibainika na wafanye nini.
No comments:
Post a Comment