Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kati Vuai Mwinyi,alipowasili katika shere za Ufunguzi wa Jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,liliopo Tunguu,Wilaya ya Kati Unguja,katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya ufunguzi wa jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,lililopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja jana,katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Utumumishi wa Umma na Utawala Bora Haji
Omar Kheir.
Omar Kheir.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma,(IPA) Harusi Masheko Ali,alipotembelea madarasa ya kusomea,baada ya ufunguzi rasmi wa Jengo la Chuo hicho uliofanyika jana Tunguu, Wilaya ya Unguja, katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akifuatana na Waziri wa Utumumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheir,(kushoto) pamoja na Viongozi wengine baada ua kulifungua jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,lililopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja jana,katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Baadhi ya Viongozi na Wananchi walioalikwa katika sherehe za Ufunguzi wa jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,zilizofayika jana huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja, wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Rais wa Zanzibar,alipokuwa akitoa hutuba yake katika kusherehekea shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi na Wananchi walioalikwa katika sherehe za Ufunguzi wa jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,zilizofayika jana huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja, wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Rais wa Zanzibar,alipokuwa akitoa hutuba yake katika kusherehekea shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akiwahutubia Wananchi, katika sherehe za ufunguzi wa jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,lililopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja jana,katika shamra shamra
za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Maalim Abdalla Suleiman,(wa pili Kulia) na Waziri wa Utumumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheir,(kushoto) .Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
…………………………………………………….
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein ametowa wito wa Taasisi za
Serikali na Taasisi Binafsi kukitumia Chuo cha Utawala wa Umma ili kuwajengea uwezo wafanyakazi wao kwa manufaa ya Taifa.
Amesema kuwa Chuo hicho kitaweza
kuwajengea uwezo ujuzi ubunifu uwandilifu na kuweza kuwa watumishi bora
wa taifa na jamii kwa ujumla . Hayo aliyasema leo huko Tunguu
Mkoa wa kusini Unguja wakati alipokuwa akifungua Jengo Jipya la Chuo
cha Utawala wa Umma ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za sherehe ya
miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Amesema kuwa madhumuni makubwa
yakujenga vyuo hivyo ni kuleta mabadiliko yenye lengo la kupata ustawi
bora wa maisha kwa Wazanzibar na kuwa na wafanyakazi wenye taaluma
inayostahiki .
Pia amesema kuwa chuo hicho kitaweza kutowa wanafunzi waliobora wenye misingi imara ya utawala bora na kuweza kujua haki na majukumu ya kazi zao. Aidha
Dkt Shein ameuomba uwongozi kujitahidi kuwa na wakufunzi ambao
wataofundisha katika chuo hicho kuwa na sifa zinazokubalika ili chuo
hicho kiweze kutoa wanafunzi bora .
Halikadhalika
aliutaka uwongozi kuwajengea mazingira mazuri wakufunzi wa chuo hicho
ili wasiweze kuvunjika nguvu katika utendaji wa kazi zao . Jumla
ya shilling bilioni 1milioni mia moja na saba tayari zimeshatumika
mpaka sasa kwa ajili ya Ujenzi huo na hivi sasa zinahitajika shilingi
milioni elfu 3 kuweza kuinua Jengo hilo kuwa la ghorofa moja. Jengo
la chuo hicho linatarajiwa kuwa na sehemu nyengine mbali mbali
zikiwemo za kuegesha magari,mkahawa, mabweni na uwanja wa michezo .
No comments:
Post a Comment