Wednesday, December 26, 2012

WATU 40 WANAUSURIKA KIFO KATIKA AJILI JIJINI MBEYA

ZAIDI YA ABIRIA 40 WALIOKUWEMO KWENYE BASI LA NEW FORCE WAMEPONA KUFA BAADA YA  BASI HILO KUGONGANA NA LORI LA MIZIGO AINA YA FUSO MAENEO YA PIPE LINE INYALA ,JIJINI MBEYA MAPEMA LEO ASUBUHI. BASI LA NEW FORCE LILIKUWA LINATOKEA MBEYA KUELEKEA DAR ES SALAAM. 

Hili roli aina ya fuso ndilo lililosababisha ajali hiyo kwani lilikuwa lilikuwalinalipita gari lingine bila ya kuangalia kama gari nyingine inashuka mlima na ndipo lilipokutana na basi hilo
Hii ndiyo hali halisi ya ajali hiyo dreva wa fuso kakimbia baada ya kusababisha ajali hiyo
Mtoto Samwel akisimulia jinsi ajali hiyo ilivyotokea kwani yeye alikuwa nyuma ya dereva  amesema yeye mkanda ndiyo uliomuokoa kwani mama aliyekuwa jirani yake hakufunga mkanda ameumia vibaya sana 
Baadhi ya majeruhi wameruhusiwa baada ya kupata matibabu.
Badhi ya abiria waliokuwa kwenye basi hilo wakisubiri usafiri mwingine toka katika kampuni ya new force
 




                        


Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufani ya Mbeya, Dk. Hamfrey Kiwelu, aliyesimama amesema wamepokea majeruhi 24 na kati ya hao 17 wameruhusiwa baada ya kupata matibabu na majeruhi 7 wamelazwa hospitalini hapo kuendelea na matibabu.         Picha na Mbeya Yetu Blog

No comments:

Post a Comment