Na Mwandishi wetu Tabora.
Baadhi ya
wakulima wa zao la tumbaku mkoani Tabora wamelalamikia hatua ya baadhi
ya maafisa wa ngazi ya wilaya wa Jeshi la Polisi kujihusisha kununua zao
la tumbaku na kubeba kwa kutumia magari ya jeshi hilo.
Wakizungumza
wakati wa kutoa hoja mbalimbali zikiwa ni changamoto zinazowakabili
wakulima hao katika mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha kikuu cha wakulima
wa tumbaku kanda ya magharibi mkoani Tabora,moja kati ya vikwazo
wamevitaja kuwa ni pamoja na baadhi ya maafisa wa Polisi wilaya ya
Sikonge kujihusisha na ununuzi wa zao la tumbaku.
Mmoja kati
ya viongozi wa chama cha msingi Ugunda wilayani Sikonge alisema baadhi
ya maafisa wa Polisi wilayani humo wamekuwa ni chanzo cha kuchangia
utoroshaji wa tumbaku ambayo ilipaswa kuuzwa katika chama hicho na
badala yake maafisa hao hununua na tena kwa kuibeba kwa kutumia magari
ya Polisi.
Aidha
wamethibitisha kuwa kitendo hicho pia kimekuwa kikidumaza nguvu ya vyama
vya msingi kwakuwa wakulima wanaowauzia tumbaku maafisa hao wa Polisi
mara nyingi wamekuwa wakikwepa kulipa madeni wanayodaiwa na vyama hivyo
vya msingi.
Akizungumza
katika mkutano huo mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa baada ya
kupokea malalamiko hayo amesema Serikali ya mkoa wa Tabora haitakubali
vitendo vya aina hiyo huku akiwataka viongozi hao wa vyama vya ushirika
kuorodhesha majina halisi ya maafisa hao wa Jeshi la Polisi ili waweze
kushughulikiwa.
No comments:
Post a Comment