Monday, December 17, 2012

SHULE YA SEKONDARI ANGAZA MKOANI LINDI YAKABIDHIWA MSAADA WA MAKTABA NA BENKI YA NBC


 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (kushoto) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Thomas Sowani wakikata utepe kuzindua jengo la maktaba ya Shule ya Sekondari Angaza lililokarabatiwa na NBC katika hafla iliyofanyika Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Meneja wa NBC Lindi, Godfrey Chilewa , Mkuu wa Sekondari ya Angaza, Upendo Muro, Mkurugenzi wa Read International Tanzania, Montse Pejuan na Meneja Mahusiano ya Kijamii wa NBC, Robi Matiko-Simba. NBC imetumia jumla ya shs milioni 70 kukarabati shule sita za sekondari katika mikoa tofauti nchini.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (katikati) akitoa maelekezo kuhusu somo la hisabati kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Angaza, Zainab Chikira (kushoto)n na Bahati Adam (kulia) katika hafla ya uzinduzi wa jengo la maktaba ya shule hiyo lililokarabatiwa na NBC, hafla iliyofanyika shuleni hapo, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki
 Meneja Mahusiano ya Kijamii wa NBC, Robi Matiko-Simba (katikati), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Angaza, katika hafla ya uzinduzi wa jengo la maktaba ya shule hiyo lililokarabatiwa na NBC, hafla iliyofanyika shuleni hapo, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki.
 Meneja Huduma kwa Jamii wa Benki ya NBC Tanzania, Jane Dogani (kushoto) na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (katikati) katika hafla ya uzinduzi wa jengo la maktaba ya
shule hiyo lililokarabatiwa na NBC, hafla iliyofanyika shuleni hapo,Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki. Wengine ni maofisa wa NBC, walimu na viongozi wa Mkoa wa Lindi.
Meneja wa NBC Tawi la Lindi, Godfrey Chilewa (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Angaza, katika hafla ya uzinduzi wa jengo la maktaba ya shule hiyo lililokarabatiwa na NBC, hafla iliyofanyika shuleni hapo, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki. NBC imetumia jumla ya shs milioni 70 kukarabati shule sita za sekondari katika maeneo tofauti nchini.

No comments:

Post a Comment