Rais Kikwete akiweka udongo katika kaburi la
marehemu Siraju Juma Kaboyonga.
Rais mstaafu Ali Hassani Mwinyi akiweka udongo
katika kaburi la Marehemu Siraju Juma Kaboyonga wakati wa mazishi yake
Baadhi ya waombolezaji wakielekea makaburini
wakati wa mazishi ya mbunge wa zamani wa Tabora mjini, marehemu Siraju Juma
Kaboyonga katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo ameungana na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini (CCM), Hayati Siraji Juma Kaboyonga.
Marehemu Kaboyonga ambaye amezikwa kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam, alifariki dunia usiku wa Jumanne ya wiki hii kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka 63.
Miongoni mwa waombolezaji walioshiriki mazishi ya leo ya Marehemu Kaboyonga, ambaye mpaka kifo chake alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), alikuwa Rais wa Awamu ya Pili ya Uongozi wa Tanzania, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi.
Marehemu Kaboyonga alikuwa Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini kwa tiketi ya CCM kati ya mwaka 2005 na 2010 na katika salamu zake za rambirambi jana, Rais Kikwete alimwelezea marehemu kama mtumishi wa umma wa mfano wa kuigwa ambaye uwezo wake wa uongozi ulijionyesha dhahiri wakati wa kipindi chake cha ubunge na kwenye nafasi nyingine za umma alizopata kuzishikilia katika maisha yake.
No comments:
Post a Comment