KATIBU TAWALA WA MKOA WA TABORA KUDRA MWNYIMVUA WAKITETA JAMBO NA VIONGOZI WA VIJIJI VYA MILENIA DR GEORGE SEMPEHO NA MWENYEKITI WA HALASHAURI YA WILAYA YA UYUI SAID NTAHODI NA DR NYANZI |
DR GEORGE SEMPEHO AKITOA MAELEZO KABLA MGENI RASMI HAJAFUNGUA MKUTANO HUO WA WADAU WA VIJIJI VYA MELINIA KATIKA UKUMBI WA MTEMI ISKE MWANAKINYUNGI |
VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI MKONI TABORA WAKIONGOZWA NA MKUU WA WILAYA YA UYUI LUCY MAHENGA |
KATIBU TAWALA MKOA WA TABORA KUDRA MWINYIMVUA AKIFUNGUA MKUTANO WA SIKU MBILI WA WADAU WA VIJIJI VYA MILENIA MBOLA MVP |
Na Lucas Raphael,Tabora
Milenia
Mradi wa Kijiji cha millennia –
Mbola unatarajia kuhitimishwa rasmi
mwaka 2015 na hivyo kijiji hicho kitabaki kuwa kijiji cha mfano ambapo mbinu
zilizotumika katika kuboresha maisha kwa wakazi wa kijiji hicho zitatumika
kuendeleza vijiji vingine hapa nchini.
Akizungumza
na kujadiliana na wadau kuhusu hali itakuwaje baada ya awamu ya pili ya mradi
huo kukamilika ifikapo mwaka 2015, mkuu wa wilaya ya Uyui Mkoani Tabora, Lucy
Mayenga, amesema serikali inajivunia uwepo wa mradi huo kwani ni kielelezo
madhubuti cha maendeleo.
Alisema kuwa
mradi huo umeweza kufanya mambo mengi ya maendeleo kwa wakazi wa kijiji cha
millennia cha mbola mkoani Tabora, ambapo huduma za kijamii zinazotolewa katika
kijiji hicho ni nzuri.
Alisema
serikali na halmashauri zinapaswa kujifunza kupitia mradi huo, kwani imebainika
kuwa mradi yote iliyotekelezwa katika kijiji hicho imejengwa kwa gharama nafuu
huku miradi inayotekelezwa katika sehemu nyingine ikiwa na gharama kubwa.
Naye mratibu
wa mradi wa vijiji vya milenia nchini, Dk. George Sempeho, amesema kwa kuwa
mradi huo unafikia tamati hivi sasa, UNDP imeona itakuwa vyema kufanya tathmini
na kuacha mradi huo ukiwa endelevu badala ya kuuacha holela na hatimae kufa.
Naye
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya
Uyui mkoani Tabora, Said Ntahondi, amesema kuwa kijiji hicho kimekuwa na
maendeleo makubwa na kwamba mara zote mradi huo, umekuwa ukitumia njia
shirikishi ambazo zimesaidia kufikiwa kwa maendeleo hayo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment