Staa wa
Vichekesho na Filamu Bongo, Said Mohamed Ngamba ‘Mzee Small’ akiwa amelazwa
hospitali kutokana na maradhi yanayomsumbua.
KWENU
mnaohusika na sanaa ya filamu Bongo. Mnajitambua sina haja ya kuwataja
mmojammoja kwa majina, nitamaliza ukurasa bure.
Mimi najua
mpo poa, mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Binafsi niko poa, naendelea
na majukumu yangu ya kila siku ikiwamo hili la kuwaandikia barua.
Barua yangu leo moja kwa moja
nailekeza kwa nyinyi wote ambao watu sasa hivi wanawatambua kwa jina la mastaa
wa filamu katika soko la Bongo, Bongo Movies.
Kikubwa ni
kwamba, natambua mchango mlionao katika kusogeza gurudumu la maendeleo ya nchi.
Natambua umuhimu wenu wa kuwatibu watu kisaikolojia kupitia filamu zenu
mnazozifanya.
Hongereni kwa
hilo.Katika taaluma yangu ya uandishi wa habari, mara kadhaa
nimeshuhudia uwezo wenu katika kufanikisha mambo yanayowahusu, iwe ni sherehe
au misiba.
Eeeh, kwenye
sherehe basi mnalipuka na kushangweka kwelikweli. Kwenye misiba, mnahakikisha
mnamsindikiza mtu anayewahusu kwa hadhi anayostahili.
Hoja hapa ni
kwamba, hadhi ile ambayo mnajitutumua hadi kwenye misiba, kwa nini tusioneshe
kwa mkongwe wa sanaa nchini, Said Ngamba ‘Mzee Small’? Tunashindwa nini? Mbona
pesa zipo?
Kwa nini
tusimsaidie mzee wetu ambaye tunaimani alikuwa chachu ya vijana wengi kuingia
kwenye sanaa?
Mzee wetu
anasumbulia na ugonjwa wa kupararazi. Anashindwa kufanya shughuli zake za sanaa
ambazo ndiyo chanzo cha pato lake la kila siku.
Binafsi
nilisikitishwa na kupongeza kitendo cha Rais wa Shirikisho la Filamu nchini
TAFF, Saimon Mwakifwamba kuingilia kati na kuanza kutembeza ‘bakuli’ la
michango kwa ajili ya kumsaidia mzee huyo.
Nilisikitika
kwani sikuona haja ya yeye kuingilia kati suala hilo ambalo naamini lilikuwa
chini ya uwezo wenu, mnaweza bwana! Kikubwa ni kipi haswa? Mbona mna ‘mauwezo’,
msinifanyie hivyo bwana.
Kwani kuna tatizo
gani tukiweka nukta katika starehe hata kwa siku moja, tusipige kilevi siku
hiyo halafu tujichangishe fedha za kumpa sapoti mwenzetu kwenye kipindi hiki
ambacho anaumwa?
Hakika hili ni
dogo, tukiamua tunaweza tena haliwezi kuharibu bajeti zenu hata kidogo.
Ni yule yule,
Mkweli Daima.
Joseph Shaluwa
No comments:
Post a Comment