Kampuni
ya Fichuka Development Agency Ltd, leo tarehe 21/12/2012 inatambulisha
mfumo mpya kabisa wa usambazaji wa kazi za wasanii ambao umepewa jina
la MFUMO RAFIKI (Code number) na utaanza kutumika rasmi kuanzia tarehe
23/12/2012 siku ya uzinduzi wa BUM KUBAM DVD utakaofanyika katika ukumbi
wa New maisha Club ikiwa ni sehemu pia ya kuutambulisha mfumo huu mpya,
tunaanza na msanii wa muziki wa
kizazi kipya aina ya Hip hop Tanzania Nikki wa Pili katika Makala (Documentary) ya wimbo wake iliyopewa jina la BUM KUBAM DVD.
kizazi kipya aina ya Hip hop Tanzania Nikki wa Pili katika Makala (Documentary) ya wimbo wake iliyopewa jina la BUM KUBAM DVD.
Bum Kubam
inafungua njia ya mpya na ya kimaslahi kwa wasanii wa Muziki pamoja na
Filamu nchini Tanzania, ikiwa ndio sekta pekee ambayo inakisiwa kuwa na
uwezo mkubwa wa kutoa ajira kwa Vijana na rika lolote lakini ajira hizi
hazikuonyesha kuzaa matunda lakini ujio wa MFUMO RAFIKI (Code Number)
uliofanyiwa utafiti kwa kina kwa lengo la kuokoa kizazi hicho katika
kupambana na Maharamia.
Teknolojia hii
mpya imegharimu kampuni fedha nyingi ikiwa katika utafiti pia
kuutengeneza mfumo wa mauzo kwa kutumia mfumo wa Digitali ambao ni wa
kwanza kabisa kufanyika Afrika pengine hata Ulimwenguni, hadi leo
unatambulishwa kwenu wanahabari na umma kwa ujumla, kama tulivyosema
awali kuwa makala ya Bum Kubam ni kazi ya kwanza lakini baada ya mwezi
pia tutangaza kazi inayofuata kwa mfumo kama huu wa mauzo.
Kwa utafiti uliofanywa kwa zaidi ya miaka mitatu na muasisi/mkurugenzi wa kampuni ya Fichuka Develoment Agency Frank
John akishirikiana na wataalam kutoka sehemu mbalimbali waligundua
kwamba sababu za wasanii kutonufaika na kazi zao ni, kuwepo kwa bidhaa
Bandia (Fake) sokoni, kukosekana njia rahisi ya msanii kujua mauzo
halisi ya kazi zake, kutopatikana kwa kazi ya msanii
No comments:
Post a Comment